Wanafunzi wa udaktari mwaka wa tano wafukuzwa chuo Muhimbili

Kereto

Member
Jul 20, 2008
17
1
Chuo kikuu cha afya muhimbili kimewafukuza chuo baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tano na makumi wengine wamesimamishwa masomo kwa miaka miwili kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kutumiwa na chama pinzani(chadema)....inasemekana wanafunzi hao waliandaa na kushiriki katika maandamano ya amani kudai kurudishiwa serikali ya wanafunzi chuoni hapo.

Uongozi wa chuo cha muhimbili ulilazimika kuvunja na kutotambua uwepo wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo baada ya uongozi wa wanafunzi na ule wa chuoni hapo kushindwa kuafikiana juu ya baadhi ya mambo fulani.... Ikiwemo kupitishwa kwa katiba mpya kandamizi kwa wanachuo!

Kitendo hicho kiliwauma wanachuo hadi kufikia hatua ya kuamua kuitangaza kero yao kwa kufanya maandamano ya amani.....hicho ndio kiliwapoza...
 
CHUO KIKUU CHA AFYA MUHIMBILI KIMEWAFUKUZA CHUO BAADHI YA WANAFUNZI WA MWAKA WA TANO NA MAKUMI WENGINE WAMESIMAMISHWA MASOMO KWA MIAKA MIWILI KWA TUHUMA MBALIMBALI IKIWEMO KUTUMIWA NA CHAMA PINZANI(CHADEMA)....INASEMEKANA WANAFUNZI HAO WALIANDAA NA KUSHIRIKI KATIKA MAANDAMANO YA AMANI KUDAI KURUDISHIWA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUONI HAPO.UONGOZI WA CHUO CHA MUHIMBILI ULILAZIMIKA KUVUNJA NA KUTOTAMBUA UWEPO WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUONI HAPO BAADA YA UONGOZI WA WANAFUNZI NA ULE WA CHUONI HAPO KUSHINDWA KUAFIKIANA JUU YA BAADHI YA MAMBO FULANI....IKIWEMO KUPITISHWA KWA KATIBA MPYA KANDAMIZI KWA WANACHUO!!!! KITENDO HICHO KILIWAUMA WANACHUO HADI KUFIKIA HATUA YA KUAMUA KUITANGAZA KERO YAO KWA KUFANYA MAANDAMANO YA AMANI.....HICHO NDIO KILIWAPOZA.....!! NAWASILISHA.
:help:

Time will tell! Serikali ya kidhalimu . Afadhali ya MKOLONI
 
Hakuna gharama kubwa ya kusoma kwenye vyuo kama udaktari. Tanzania imetumia pesa nyingi sana kutoka hawa vijana wakiwa darasa la kwanza wamesoma bure, sekondari, na vyuoni . Sasa wamebakiza mwaka mmoja tunawafukuza je tunajua gharama za kusomesha Dr mmoja?? ni kubwa sana na tuna madaktari wangapi??
 
chuo kikuu cha afya muhimbili kimewafukuza chuo baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tano na makumi wengine wamesimamishwa masomo kwa miaka miwili kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kutumiwa na chama pinzani(chadema)....inasemekana wanafunzi hao waliandaa na kushiriki katika maandamano ya amani kudai kurudishiwa serikali ya wanafunzi chuoni hapo.uongozi wa chuo cha muhimbili ulilazimika kuvunja na kutotambua uwepo wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo baada ya uongozi wa wanafunzi na ule wa chuoni hapo kushindwa kuafikiana juu ya baadhi ya mambo fulani....ikiwemo kupitishwa kwa katiba mpya kandamizi kwa wanachuo!!!! Kitendo hicho kiliwauma wanachuo hadi kufikia hatua ya kuamua kuitangaza kero yao kwa kufanya maandamano ya amani.....hicho ndio kiliwapoza.....!! Nawasilisha.
:help:

hiv kwa nini hatuheshimiani -siku hiz ni vita tu! Hakuna mazungumzo-hii ni mbaya sana
 
hiv kwa nini hatuheshimiani -siku hiz ni vita tu! Hakuna mazungumzo-hii ni mbaya sana

serikali yetu inawaangamiza vijana mashujaa na hodari wa kulipigania taifa,kwa kisingizio cha utovu wa nidhamu, sasa hatujui kesho nani atasimama kututetea mbele ya mafisadi!!
 
Naomba kuuliza wizara ya elimu imepitishwa? Ka imepitishwa naomba kuuliza kwanini.. Walimu wamegoma.. Hawalipwi mishahara huduma za elimu ni duni hakuna vifaa kama madawati vitabu hasa huko vijijini kibaya zaidi wanafunzi wanafaulu darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika..huko vyuo vikuu navyo kuna issue tunasikia dada zetu wanalalamika kua kupata mikopo ile inayotolewa na serikali wanafunzi wengine wa kike inabidi watoe miili yao ili kupata hizo hela sa niambieni kwanini wabunge wakubali kuipitisha hii wizara wakati imeoza ina kasoro nyingi na vitu vingi vinabidi kubadilishwa
 
Hakuna gharama kubwa ya kusoma kwenye vyuo kama udaktari. Tanzania imetumia pesa nyingi sana kutoka hawa vijana wakiwa darasa la kwanza wamesoma bure, sekondari, na vyuoni . Sasa wamebakiza mwaka mmoja tunawafukuza je tunajua gharama za kusomesha Dr mmoja?? ni kubwa sana na tuna madaktari wangapi??

inasikitisha sana, yani tanzania bana kweli nchi ye2 ni shamba la bibi, yani sababu za utovu wa nidhamu ndio iicost serikari mamilioni ya mapesa?, hainijii kbs, kusomesha daktari m1 c chini ya shilingi 33m, leo frm no where, eti kwa kigezo cha nidhamu unakubali kuingia hasara? Afu madai ya walimu eti hayalipiki, madaktari wakidai kuboreshwa kwa huduma za afya nchini ikiwa ni pa1 na vifaa vya kutibia, hilo kwao co la muhimu, huku wanacheza karata tatu kwa kutimua wanafunzi vyuoni, na kunyang'anya lesseni madaktari. Ama kweli la kuvunda halina ubani!
 
Si wampigie simu Kagame aje awachukue wamalizie shule huko Rwanda?

Kama kweli basi inasikitisha mno haya mambo na kuuwa taifa.
 
Serikali ya CCM ipo kati imezungukwa na mabomu ambayo yatalipuka na kuiangamiza 2015, mabomu yenyewe ni (Madaktari na familia zao, Walimu na familia zao, Wanafunzi wa vyuo vikuu karibu wote, Vijana ambao ni wengi wasio jua ya kesho, wazee wa EA pamoja na familia zao, kwa hili serikali ya CCM kupenda kukurupuka katika maamuzi ndiyo kuendelea kujiongezea mabomu ambayo kwa hakika lazima yalipuke 2015.
 
Serikali dhalimu inaendeleza udhalimu wake. Badala ya kukaa meza moja na madaktari ili kumaliza/kupunguza matatizo yaliyokuwepo katika sekta ya afya wameamua kufanya maamuzi ya kuwakomoa madaktari wanafunzi. Walaaniwe wote waliohusika na maamuzi haya ya kipumbavu.
 
Hiyo ndio sawasawa, wegine watajuwa kama wanakwenda pale kusoma au kufanya siasa.
 
Back
Top Bottom