Wanafunzi wa Tanzania waongoza kwenye uandishi bora wa Insha Afrika Mashariki! Mtanzania awa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mkutano wa 20 wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki umeanza leo asubuhi Ijumaa Februari Mosi, 2019 kujadili masuala mbalimbali.

Viongozi wakuu waliopo katika mkutano huo unaofanyika jijini Arusha, Tanzania ni Rais wa Tanzania, John Magufuli; Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta; Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda.

Katika mkutano huo Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza anawakilishwa na makamu wa kwanza wa Rais, Gaston Sindimwo huku Rais wa Sudan Kusini akiwakilishwa na Waziri wa Biashara, Paul Mayon.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki imeeleza kikao wakuu hao wameanza na kikao cha ndani na saa 8 mchana watafanya mkutano mkuu.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo miongoni mwa ajenda za mkutano huo ni kuidhinisha Kenya kugombea uanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa katika kipindi cha mwaka 2021-2022.

Ajenda nyingine ni kupata taarifa ya mchakato wa Somalia kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupata taarifa ya itifaki ya masuala ya umoja wa forodha.

Wakuu hao wa nchi pia wanatarajia kujadiliana juu ya mchakato wa shirikisho la kisiasa la Afrika ya Mashariki na taarifa mbalimbali za fedha na utendaji wa Sekretarieti.








UPDATES
Jaji Sauda Mjasiri ameapishwa leo Februari 01 2019 katika Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki

Jaji Msafiri anakuwa Mwanamke wa pili kuteuliwa katika nafasi hiyo na atatumikia nafasi hiyo kwa miaka mitano akichukua nafasi ya Jaji Fakihi Jundu

Aidha, Wanafunzi wawili kutoka Tanzania wamefanya vizuri katika Shindano la uandishi wa insha katika ngazi ya kanda ya Afrika Mashariki

Michael Nyaruga kutoka Kibaha sekondari ameibuka kidedea kwa mwaka 2017 huku Innocent Shirima kutoka Moshi sekondari akiibuka kidedea kwa mwaka 2018




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naogopa kutazama maana naweza kuambulia aibu kama ile ya Kampala. Kila mtu mwenye mapenzi mema afumbate mikono yake na kumuomba maanani aiepushe na aibu nchi yetu isije ikatutokea kwa mzee baba kusema hovyo.
HUO NDIO UZALENDO
 
Hii jumuiya ipo ipo tuu huku mipaka yao ikiwa hovyo kuhusu mahusiano ya kibiashara tofauti na Nchi za SADC mipaka ipo wazi kabisa hakuna usumbufu wa kijinga kama Afrika Mashariki...
 
Nipo hapa AICC na washikaji kwa shughuli fulani ya kizushizushi tukiomba mkutano uishe haraka tukale zetu Bata kwa jirani.
 
Tuna fuatiliaje hayo makitu wakati hatuja oga tuna itaji maji kwanza Arusha baada ya hapo ndo tufwatilie Siku ya tano sasa Arusha hakuna maji maeneo yote kwanzia ngulelo
 
Wakuu wa Nchi wote lao moja ,sana wanaenda kuambukizana Sumu tu namna ya kuwabana Raia wao ili waendelee kusalia Madarakani...
 
Burundi imetuma mwakilishi na hoja kubwa ni mgogoro wa Rwanda na Burundi, Jiwe,Slim,Museveni,Kenyatta kama kawaida yao hawajamiss,Salva kiir wa South Sudan katuma mwakilishi kubembeleza kujiunga na Chama kubwa.
 
Naogopa kutazama maana naweza kuambulia aibu kama ile ya Kampala. Kila mtu mwenye mapenzi mema afumbate mikono yake na kumuomba maanani aiepushe na aibu nchi yetu isije ikatutokea kwa mzee baba kusema hovyo.
HUO NDIO UZALENDO
Pale umetinga mgolole kuja hapa kupinga lakini hujui upinge nini. Mnapitia hard times sana.
 
Back
Top Bottom