Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,442
- 3,353
Wakienda na hela wazazi/walezi na wewe ukiwemo ungesema walimu wanaanzisha miradi ya kuwachuna wanafunzi. Mimi naona ni vizuri TuTatizo hizo kitu zinaharibika mapema ni bora wangeeleza kuwa waende na hela wanunue huko huko zitakapohitajika
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkakati mzuri katika wakati kama huu Elimu imetumika kukabiliana na tatizo | |||||||
mkuu,ni unga kama ule wa ugali lakini ni limao,yani kwa kifupi ni maji ya limao yamefanyiwa namna yakawa unga ,ni mweupe
Kama uonavyo chumvi ya unga..
Uongozi wa shule hii wana shida kubwa sana mahali.
Wanasema wanafunzi hawatatoka wala kutembelewa na wazazi.
Je, waalimu nao hawata onana na watu wengine au na familia zao pia zifugiwe au wafungiwe waalimu tu?
Sanitizer nusu lita kwa mtu mmoja ni nyingi sana kwa muda mfupi wanaokaa shuleni sabuni za maji ndiyo muhimu sana kuliko sanitizer.
Kutembea na barakoa wakati wote siyo vizuri kiafya watawaumiza watoto wa watu wapate shida za mfumo wa upumuaji.
Limao ya unga sidhani kama ina virutubisho au kemikali muhimu zinazosaidia kuongeza Vitam C na wala kuondoa ute kwenye koo, shule iwaagize waje na pesa ya kununua malimao mabichi ambayo pesa wanapewa shule na kuwagawia wanafunzi limao bichi moja kila siku.
Tangawizi mbichi ndiyo bora zaidi hivyo shule ifanye kama hapo nilivyo shauri kwenye limao halisi siyo ya unga.
Mwisho waalimu wapunguze uoga, kama wanaogopa waache kazi wabakizwe waalimu vijana wenye afya wawafundishe wadogo zao badala ya kuwanyanyapaa na kuwatesa na makemili na mabarakoa kila saa.
Serikali itoe muongozo maana maagizo kama haya ni vurugu tupu, kuna wanafunzi wenye shida za ulcers na nyinginezo za tumbo au kuna wale wenye allergy na sanitizer flai wasije kulazimishwa haya makemikali ya sanitizer na malimao feki, watoto wasije wakarudi nyumbani matumbo yashatoboka na madonda ya tumbo.