Wanafunzi wa shule kutoka usiku shuleni

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,149
6,989
Napenda kuuliza wanaofahamu kuhusiana na sheria za elimu, huwa naona watoto wa baadhi za shule wakitolewa usiku, wengine kuanzia saa mbili na kuendelea. Hii imepitishwa na wizara ya elimu, au shule husika huamua tu?

Kwa mtizamo wangu;

1.Kuna hatari nyingi zinazowakabili watoto hawa, hasa wengi ni wa wadogo, kama wa darasa la saba, kwa kuwa wengi wanakaa mbali na shule.
2.Watoto wanachoka sana, kwa wataalamu wa afya wanatuambia mtu kufanyakazi ni masaa 8, kupumzika masaa 8, kulala masaa 8. Kwahiyo huyu mwanafunzi anapata mda gani wa kupumzika?
9.Vile vile wataalamu wa afya wanasema mtoto apate mda wa kucheza ni haki yake. Na pia imesikia mpaka Jumamosi wanakwenda shule.

Ningeomba ufafanuzi, pengine huwenda mimi ndio sielewi, kuhusu huo utaratibu, wa kubaki shule mpaka zaidi ya saa 12 jioni, kwa masomo.
 
Back
Top Bottom