Wanafunzi Wa Sekondari Washindwa Kusoma Na Kuandika Sentensi Za Darasa La Kwanza!

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,817
Wanafunzi Wa Sekondari Washindwa Kusoma Na Kuandika Sentensi Za Darasa La Kwanza!

Wanafunzi 14 wanaosoma katika Shule ya Sekondari Mgololo iliyoko Wilaya ya Mufindi, Iringa, wamebainika kuwa hawajui kusoma wala kuandika baada ya kutungiwa mtihani unaofanywa na wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili wa Kiswahili wa kusoma na kuandika. Mtihani huo ulifanywa na wanafunzi wote wa shule hiyo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa shule hiyo, Jumanne Nyaulingo amemwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kulalamika kupelekewa wanafunzi ambao hawajui kusoma wala kuandika na akipendekeza warudishwe shule ya msingi.

Nyaulingo anasema alifikia hatua hiyo baada ya wanafunzi wa kidato cha pili kufanya mtihani na baadhi yao kuandika kwenye mitihani hiyo maneno yasiyosomeka, “Yaani walichoandika ni kama Kilatini, hivyo tukashauriana kuwa yawezekana kuna wanafunzi ambao hawajui kusoma na kuandika na njia pekee ya kuwabaini ni kuwatungia mtihani rahisi unaofanywa na madarasa ya awali katika shule za msingi,” alisema.

Wanafunzi hao wamegawanyika kaitka vidato mbalimbali kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne. Akasema kati ya hao 14, wanne ni wanafunzi wa kidato cha kwanza waliofaulu vizuri mitihani yao; lakini pia wazazi kwenda shuleni hapo kulalamika iweje watoto wao wafaulu wakati hawajui kusoma wala kuandika.

Nyaulingo alisema kutokana na hali hiyo, alipeleka malalamiko kwa DED na Mkuu wa wilaya kulalamikia hatua ya kupelekwa wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika, “Nimepeleka majina ya wanafunzi 10 ambao wako kidato cha pili hadi cha nne ambao hawajui kusoma wala kuandika, lakini sijajibiwa barua yangu… badala yake mtendaji wa kata ameelezwa suala hilo na DED amekuja shuleni hapo akanitaka nishauriane na walimu wa shule za msingi na shuleni hapo ili tuwasaidie wajue kusoma na kuandika. “Mimi nimekataa kwa vile hapa shuleni sina walimu wenye ujuzi wa kumfundisha mtu ajue kusoma na kuandika, mimi naletewa walimu ambao ni wataalamu wa masomo ambao wana Stashahada na Shahada. “Hiyo kazi ya kumfundisha mwanafunzi kusoma na kuandika inafanywa na walimu wa elimu ya awali,” alisema mkuu huyo wa shule.

Alisema binafsi baada ya kubaini kuwapo kwa wanafunzi hao shuleni hapo, alipendekeza warudishwe shule ya msingi, lakini ikaonekana kuwa sera ya elimu hairuhusu mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi na kufaulu, haruhusiwi kurudi tena shule ya msingi, “Hata kwenye mikutano ambayo tulifanya hapa na wazazi tulishauri warudi lakini ombi hilo limekataliwa na mamlaka husika,” alisema Nyaulingo.

Kuhusu wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao walifaulu na wazazi wao wakaenda kulalamika shuleni hapo, alisema baada ya wanafunzi hao kufaulu wazazi wao walisita kuwapeleka shule na ndipo mtendaji wa kata akatishia kuwashtaki.

Alisema baada ya tishio hilo wazazi hao kila mmoja kwa wakati wake alienda na kijana wake shuleni hapo kulalamika kuwa analazimishwa ampeleke mtoto wake sekondari wakati anajua fika kuwa ataharibu fedha zake kwani mtoto wake hajui kusoma wala kuandika, “Mtendaji aliwaambia awe anajua au hajui kusoma aliwataka watoto hao wawepo shuleni, lakini wazazi wakawa hawataki na baadaye waliwaleta nami nikataka kujiridhisha kwa kuwaandikia maneno ya darasa la kwanza ili wayasome lakini walishindwa,” alisema.

Alimtaja mwanafunzi Happy Mwango aliyetoka shule ya Msingi Makungu ambaye alama zake za kufaulu ni 166 kati ya 250. Mwanafunzi huyo alishindwa kusoma sentensi zifuatazo “Bibi anakula chakula. Mama analima bustani."

Mwanafunzi huyo alipelekwa shuleni hapo na mzazi wake Januari 3, mwaka huu. Mwanafunzi mwingine ni Rachael Mbilinyi aliyekuwa anasoma shule ya msingi Lugema.

Mtihani wa darasa la saba alifaulu kwa alama 106, lakini alishindwa kuandika maneno haya, "Shangazi, Popo" na pia alishindwa kusoma sentensi hii, "Babu ni mgonjwa sana."

Tilani Mbogela aliyetoka shule ya Msingi Makungu alishindwa kusoma sentensi, "Shangazi Ni mgonjwa," wakati Raymond Lukandema aliyetoka shule ya msingi Makungu na aliyefaulu mtihani wa darasa la saba kwa alama 144 naye alishindwa kusoma sentensi hiyo.

Chanzo: HabariLeo
 
Mkuu Sijui nieleze vipi lakini wanajf napenda tukubali kuwa nchi hii ina matatizo makubwa na ya msingi na bila haya kushughulikiwa tusishangae haya tunayoyaona. Tume kuwa na tabia ya kufunika mambo na hata kuyarahisisha ili yafanane na ya wengine duniani. Katika thread yangu ya siku za nyuma "Should poverty eradication be the no.1 priority for Tanzania now?" nilikuwa nabainisha kuwa kwa matatizo tuliyona hatuweza kwenda mbele kwa kutumia mikakati ya kawaida. Tunahitaji tukubali kuwa we are stuck and the centre can no longer hold. We need a fundamental change. Hawa watoto wako sekondari lakini kumbuka hawajawahi kufaulu au kufeli kwani hawakuwahi kufanya mtihani- nasema hivyo kwani ili kufanya mtihani wa nadharia ambao siyo oral lazima ujue kusoma na kuandika. Sasa hawa hawajui kusoma wala kuandika na wapo shuleni wanabadili milango kila baada ya mwaka. Kwa kawaida Sipendi kutumia lugha mbaya lakini hivi kwa kauli ya huyo anayema kuwa sera hairuhusu hawa warudi msingi ametumia nini kufikiri na je, wapo wanaofikiri?

Mimi sioni tatizo kwa watoto hawa naona tatizo kuwa hii hatustushi - Mambo yanaendelea - Business As Usual na huenda wapenzi wetu watatuongeza tena kuwa tumevunja rekodi ya idadi ya watoto wanaomaliza sekondari.

 
Jamani! Kama anashindwa kusoma alama tajwa hapo awali,Je? Kiingereza atasikiaje ingali write ya kiswahili ndiyo hivyo? HIYO NDIYO FAIDA YA SERIKALI LEGELEGE YA JAMHURI YA MUUNGANO. Na mbado!!
 
Mambo ya sera za ccm zinatekelezeka. Matokeo ya 2010 na kuendele ya form 4 ndo mwanzo wa mazao yanayoingia. Garbage in,garbage out
 
Usiulize maks walipataje, uliza kwanza walimu wa shule walizosoma wanafunzi hao wakoje?
WAlimu wao hawana makosa kwani nao pia wanashangaa balaza la Mitihani NECTA kutoa matokeo kua wamefaulu!
Hii pia ilitokea kwenye kata yangu(naihifadhi jina) kuna mtoto alifaulu vizuri sana baada ya matokeo ya darasa la saba kutoka lakini cha ajabu yeye mwenyewe alikua anashinda ndani kwa kuogopa aibu,wazazi,wanafunzi wenzake na walimu walibaki wanashangaa kwani kijana huyo alikua hajui hata kuandika jina lake,na aliferi darasa la nne mara mbili baadaye wakamuachia tu amalize.Hakupewa msaada wowote kwenye mtihani lakini alifaulu!.Wenzake wakawa wanamzomea kias kwamba alikosa amani kabisa pale kijijini.Na isitoshe wazazi walikataa kabisa kumsomesha kwan uwezo wake waliuujua.
Je,hapa utamlaumu nani?.Nadhani NECTA nao kuna uzembe fulani unafanywa wala si walimu tu!
 
wakuu tukubaliane elimu bongo uharo mtu wanafunzi wanapewa majibu na wasimamizi wao ili linaeleweka halina kificho ni mkakati wa kila wilaya na kila afisa analijua hilo.shule inayofelisha huandamwa na ukaguzi mpaka wakome
 
Dah bora nilihamishwa kutoka hyo shule Makungu ila hata hivyo kwa wakati ule hakukuwa na utumbo km huo enzi za Mungai
 
Si ndo mnazitaka hizi?Serikali shule zake imeshindwa kupeleka hata samani watoto wanakaa kwenye mawe kama gomamli/mijusi na wengine chini wanagonoka kama wako yoga club sasa imeanza kupenyeza siasa kwa walioweza ambao madarasa yana hadi AC halafu wapambe wanakenua eti Private sector inajenga tabaka nchini.Let that be a challenge for your hustle ili umudu 7.5M za Feza schools otherwise usilete ngonjera za tabaka mara oooh.
 
Nakung'ong'enaza usimwambie mwingine "hata mwana pale magogoni ngeli haipand fresh na ana phd " sawa kaa nalo hao watakuja tu kuwa viongoz wazur baadae kusoma kutawafata wakishakuwa na mafanikio
 
Mm naona tatizo ni mitihani ya dalasa la saba ndio tatizo, mpaka hesabu unachagua majibu unategemea nn!
eti tu serekali inakwepa gharama za usahishaji wa hiyo mitihani, wanatumia mashine maalum! Kwa hiyo ni rahisi kwa wajinga wengi kukopi na kupesti!

kuhusu waalimu wanachangamoto nyingi za kukosa ushirikiano wa wazazi na hata jamii kwa ujumla!

hutakuta watoto hususani wanao ishi madhingira magumu, wazazi na walezi wamewageuza vitega uchumi majumbani au walezi wa wadogo zao!
watoto kama hao maudhirio yao yanakuwa sio mazuri, unakuta mtoto kwa mwezi anakuja shule siku moja au haji kabisa hadi miezi 3 ! Mtoto kama huyo ata asome miaka 20 atawezaje kujua kusoma na kuandika? na wazazi wakiitwa huwa hawaji

kwa hiyo inakuwa ngumu kwa waalimu wa awali kukaa na mtoto wanamna hii unamrudisha madarasa mpaka anaanza kuota madevu, inawabidi wawapeleke hvyo hvyo ili wamalize la saba waendelee na maisha yao! Ndipo wanapo kutana na hiyo mitihani ya kuchagua! Tena unatakiwa kuweka alama ya hvi - kwenye herufi ya jibu
 
Back
Top Bottom