Mindi ulichoongea ni cha ukweli, maslahi yanamfanya mtu afanye kazi kwa bidii na kujitoa lakini si kama hali ilivyo sasa na sio kwa walimu tuu hata kwa wafanyakazi wa sector nyingine hakuna mwenye hari ya kujitoa kufanya kazi wakati nyumbani hakueleweki!!Mkakati wowote ambao unaweza kupata angalau nafasi ya kufanikiwa, lazima uanze na walimu. maslahi yao, makazi yao, mafao yao. hilo la kwanza. vyoo bora, madawati na vyumba vya madarasa vifuatie, maktaba na maabara pia. lakini kwanza mwalimu. maana hata chini ya mti, mwalimu aliyehamasika atapiga kazi na atafanikisha kwa kiwango kikubwa tu. lakini hata uweke kila mwanafunzi awe na laptop, kama mwalimu hana morali ni kazi bure tu. Ni "kujilisha upepo". hayo maagizo hayana maana yoyote. Ni UMAGUFULI na UMAKONDA katika ubora wake.
Kweli kabisa Shyshii, niliongelea walimu kwa sababu naona Magu amekomaa na "elimu bure" na "madawati" akahesabu kwamba ameshamalizana na sekta ya elimu. kumbe kuna mambo kibao, na pia vipaumbele vyake siyo sahihi. Madawati yamemwagwa kama njugu, matokeo yake hakuna hata vyumba vya kuyawekea. hapo unajiuliza kama si bora wangeanza na vyumba kwanza? maana mkakati wa Maji walianza kuboresha mabomba ili maji yakiongezeka yawe na mahali pa kupita!!Mindi ulichoongea ni cha ukweli, maslahi yanamfanya mtu afanye kazi kwa bidii na kujitoa lakini si kama hali ilivyo sasa na sio kwa walimu tuu hata kwa wafanyakazi wa sector nyingine hakuna mwenye hari ya kujitoa kufanya kazi wakati nyumbani hakueleweki!!
Hakuna mwenye hamu ya kufanya kazi wakati anajua hakuna chochote mpaka mwisho mwezi ambapo hata huo mwisho wa mwezi ana kamshahara kanakatwa kwenye mkopo.
Hata waliokuwa wanajitolea kufanya kazi Jmosi sasa hakuna anayetaka anaona bora apambane na hali yake kwenye vitu vingine vitakavyomuingizia hela.
Kwahyo wanapotoa matamko yao wafikirie na hao walimu au wafanyakazi kuwaongezea au kuboresha maslahi yao la sivyo itakuwa mambo ya Passive Resistance ya kugeuza miche au kuchemsha mbegu zisiote na mwisho wa siku hakuna kinachoendelea.