Wanafunzi wa Sekondari Bagamoyo watembezwa peku

Binti Msichana

Senior Member
Oct 9, 2016
109
247
Katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi wa shule ya sekondari Dunda ilinayomilikiwa na serikali kwa nyakati tofauti miezi kadhaa iliyopita wamekuwa wakivuliwa viatu vyao na walimu wa nidhamu na kulazimika kutembea umbali mrefu bila ya viatu huku miba , jua , mawe, misumari na vyupa vikifaidi miguu yao hali inayopelekea wazazi wao kupeleka malalamiko katika ngazi mbalimbali za uongozi wa Bagamoyo.

Hali hii imewafanya wanafunzi wengi kuvunjika moyo kwenda shule kwa kuwa kwa nyakati tofauti wamekuwa wanavuliwa viatu kisha wanarudishwa majumbani kwao ati viatu vyao havitakiwi na uongozi wa shule.

Vitendo hivi vya walimu hawa vimekuwa vikikinzana na juhudi za Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu John Pombe Magufuli kuhakikisha kila mwanafunzi katika shule za serikali anapata elimu bure bila ya malipo wala bughuza za aina yeyote.

Iweje walimu hawa wakiwa na akili timamu tena bila kushirikisha uongozi wa juu wanaamua kuwafukuza watoto wa masikini huku wakiwavua viatu kwenda majumbani kwao ati kwa sababu viatu vyao si sare ya shule, je wamepata kibali kutoka kwa kamishina wa elimu wa kufanya unyanyasaji huu kwa wanafunzi ?

Je bodi ya shule imebariki uamuzi wa walimu hawa wa kuwavua viatu wanafunzi na kuwafukuza waende majumbani kwao ?

Inakuaje mkuu wa shule anashirikiana na walimu hawa kufanya madudu haya kwa wanafunzi ?

Je walimu hawa wanawajengea mini wanafunzi hawa katika maisha yao ?

Kwani kuwavua viatu na kuwalazimisha kutembea peku kunawafanya wachukie shule na kujisikia wanyonge , vilevile ni kinyume cha haki za watoto na binadamu kwa ujumla.Hali hii hupelekea kukata tamaa na kushindwa kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.
 
Hivi mleta mada una akili nzuri kweli? Nini hiki umeandika hapa dogo fuata utaratibu vaa uniform za shule hakuna atakayekubugudhi.
 
Usihalalishe madai ya kijinga kama haya na dhamira njema ya mhe rais kuhusu elimu bure.

kwanza hao walimu wa shule hiyo wana huruma sana. wanafunzi wanavaa viatu vya rusha roho shuleni halafu wao wanaishia kuwavua na kuwatembeza peku tu? walipaswa kuwafukuza kabisa.

hiyo shule ni moja ya shule ambazo wanafunzi wake wamepinda mno. bange wao, ufuska wao, kutovaa sare wao, n.k

acha kutetea uovu ww, timiza wajibu wako kama mzazi/mlezi/mwalimu.
 
Acheni kumwona mzembe mtoa mada,mimi nilikuwa nasoma Dar huwezi amini nilikuwa naenda na kandambili shule,tatizo halikuwa langu ila kuwa na wazazi wasio na elimu na wasiojua faida yake,baadae nilipoingia sekondari nlienda likizo moja kijijini kwetu nikakuta watoto wanaenda pekupeku shule nikaona ni afadhali na mie niliyekuwa naenda na Ndala au yeboyebo,hapo njia mbadala aitwe mzazi awajibishwe na mtoto aendelee na masomo ukizingatia wengine wapo darasa la saba sasa.
 
Back
Top Bottom