Wanafunzi wa mwalimu Nyerere watishiwa maisha Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wa mwalimu Nyerere watishiwa maisha Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakke, Mar 25, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=2][/h]
  Wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere, (MNMA) mjini hapa wamekuwa wakitishiwa maisha na watu wasiyojulikana kutokana na kuacha nywele na mabega wazi.
  Wakizungumza na NIPASHE jana wanafunzi hao walisema kwamba wamekuwa wakipokea vitisho kutoka kwa watu wasiyojulikana wanapokwenda chuoni na kurudi katika hosteli wanayoishi huko Mtaa wa Maisara kisiwani Unguja.
  Wanafunzi hao waliyataja maeneo ambayo yamekuwa yakitumiwa na watu hao kutoa vitisho dhidi yao ni maeneo ya Bububu, Darajani na Mkunazini Mkoa wa mjini Magharibi Zanzibar.
  Walisema kwamba wamekuwa wakizomewa na kutishiwa maisha yao kutokana na kutembea bila kufunika vichwa na mabega pamoja na kuvaa nguo zinazobana mwili.
  “Tangu tumeanza masomo tumekuwa tukiishi bila amani kutokana na vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi tunaofanyiwa wakati sote ni Watanzania.” Walilalamika wanafunzi hao walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar.
  Wanafunzi hao walitoa mfano juzi katika makutano ya barabara ya Bububu na Chuo hicho watu wasiyojulikana waliandika maneno ya vitisho kwa rangi nyekundu na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa wanafunzi hao.
  “Faida ya muungano ongezeko la ngono Zanzibar, hatutaki muungano Zanzibar.” Yalisomeka maandishi hayo.
  Akizungumza na NIPASHE, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Mushi Jackson, alisema kwamba bado hajapokea malalamiko ya wanafunzi wake kutishiwa maisha.
  Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria wanafunzi wa vyuo hawatakiwi kuvaa sare isipokuwa wanatakiwa kuvaa nguo za heshima wanapokuwa katika mazingira ya Chuo.
  Hata hivyo Kamishina wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisema kwamba watafanya uchunguzi kuhusiana na vitendo hivyo.
  Hata hivyo haliwataka wanafunzi hao kuripoti matukio kama hayo polisi ili uchunguzi uweze kufanyika na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
  Chuo hicho kimezinduliwa mwaka huu huko katika Mtaa wa Bububu, na wanafunzi 300 asilimia 95 ni wanafunzi kutoka Tanzania bara.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,079
  Trophy Points: 280
  c wavae kieshima, wanajitakia wenyewe, kwanini wasivae vizuri? wanajitakia wenyewe.
   
 3. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini wavae viguo vya kubana miili yao na kuacha vifua wazi?
   
 4. s

  shabani mitambo Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunapaswa kukaa chini na kulitafakari kwa kina jambo hili sis kama wanazuoni
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwanini wasiwavamie watalii wanaotembea na vichupi kila kona? Iko siku watamshambulia mtalii - mweusi (e.g toka Afrika kusini) halafu ndio wataona cheche.
   
 6. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hapo umenena lakini kwa Serikali yetu hakuna kitakachofanyika mpaka hapo watakaposikia Chuo kimechomwa moto na hao mjahidina feki wakati Nguruwe twala wote bila ubaguzi
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hao waliowatishia wanafunzi ni kuwa hawana la kufanya. Kama ingelikuwa wako katika ajira wasingepata muda wa kufanya mambo ya kipuuzi.
  BTW - Hizi nambari hapo juu zimekaa vipi? Wanafunzi 300, 95% (wanafunzi 285/15) wanatoka Bara. Kulikuwa na haja ya kuwapeleka huko? Nahisi wangekaa huku huku Bara wangepunguza gharama za maisha, hasa ukitilia maanani kuwa Zanzibar maisha magumu zaidi kuliko hapa Bara.
   
 8. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kweli. ukienda kwa warumi........

   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Chonde chonde watoto wa mama salma hao kueni makini.
   
 10. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kuna mchangiaji kasema jambo hili tulitafakari kwa kina. Ni kweli.

  Wa-Zanzibar wanataka kuifanya visiwa hivyo kama nchi ya kiislamu wakati si kweli. Serikali ya Mapinduzi inaunga mkono vitendo vyovyote vya kuwakandamiza wa bara. Nguo za kubana isiwe hoja, mbona mtu mke akitembea bila hijabu na akiwa ni wa bara wanakunja uso kama wamekula shubiri? Wasichana wangapi wazenj wanavaa "vi-tube" au vikaptula vya jeans toka kiunoni vina urefu wa kama 15 - 20 cm, kisha juu wanavaa baibui (pindo zote za nguo za ndani zinaonekana) hawasemi?

  In parallel na sisi wabara tuanze kuwatisha wale wazanzibar wanaovaa juba madarasani pale UDOM?
   
 11. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haya tena jana ilikuwa CBE, leo ni chuo cha kumbukumbu ya mwl Nyerere. Huu ni uhuni tu wanatafuta visingizio vya kuwanyanyasa wanawake kijinsia. Hivi wewe mwanaume, mtu mzima na akili zako timamu huwezi kuona nywele za mwanamke ukatulia? zina nini? acheni tabia za kishetani hizo!!! badala ya watu kujishughulisha na masuala ya msingi ya kuwapatia mapato na kupunguza makali ya umaskini mnaenda kuangalia mwanamke gani hajafunika nywele au kavaa nguo ya kubana???? Unajua ujinga ndo unaotusumbua au pengine kutokuwa na mwanga mpana kwenye matukio ya kimataifa. Hata hizo nchi zinazolazimisha wanawake wao vajifunike gubigubi bado wanatumia nguvu na raslimali nyingi kuwalazimisha wanawake wakubali. Chukulia Iran kwa mfano, wanawake wa huko wanajulikana kuishi double life, yaani wanavaa gubigubi mchana na kawaida usiku hasa wanafunzi wa vyuoni na mapambano yao na polisi wa itikadi yanaendela hadi leo. Saudi arabia kuna kitu kinaitwa morality police, hawa siku zote wako vitani na wanawake, hivi karibuni walisababisha vifo vya wanafunzi wa kike pale jengo la shule ya kike lilipowaka moto wanafunzi walikimbia nje bila hijab cha kushangaza police waliwarudisha kwenye jengo linalowaka moto ili wavae kwa kujistili kabla ya kukimbia moto!!!! pia wiki chache zilizopita police hao wameingia vitani na wanafunzi wa kike na kuwamwagia maji ya washa washa na kuwababisha majeruhi. Mifano ipo mingi tu inayoonyesha kuwa hizi sheria za kikatili na kishetani dhidi ya sehemu moja katika jamii ni uhuni uliopitiliza na matokeo yake ni mapambano ndani ya jamii yasiyokoma. Ukiona watu wanatanguliza vitisho vya kuua au kumshambulia mtu kwa sababu tu hawakubalini na kile anachokifanya au sema basi ujue kuwa katika hali hiyo hakuna uungu bali ni ushetani tu unaotawala
   
 12. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na mawazo yako.
   
 13. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Aisee inatisha yaani wasichana wasijiokoe kisa wapo kichwa wazi?
   
 14. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuna mambo mtu huwezi amini lakini ndo ukweli wa dunia yetu ya leo. Soma hii habari iliyoripotiwa na BBC news
  Friday, 15 March, 2002, 12:19 GMTSaudi police 'stopped' fire rescue

  [​IMG]The Mecca city governor visited the fire-damaged school


  Saudi Arabia's religious police stopped schoolgirls from leaving a blazing building because they were not wearing correct Islamic dress, according to Saudi newspapers.In a rare criticism of the kingdom's powerful "mutaween" police, the Saudi media has accused them of hindering attempts to save 15 girls who died in the fire on Monday.
  About 800 pupils were inside the school in the holy city of Mecca when the tragedy occurred.

  [TABLE="width: 154"]
  [TR]
  [TD][​IMG]15 girls died in the blaze and more than 50 others were injured


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  According to the al-Eqtisadiah daily, firemen confronted police after they tried to keep the girls inside because they were not wearing the headscarves and abayas (black robes) required by the kingdom's strict interpretation of Islam.One witness said he saw three policemen "beating young girls to prevent them from leaving the school because they were not wearing the abaya".
  The Saudi Gazette quoted witnesses as saying that the police - known as the Commission for the Promotion of Virtue and Prevention of Vice - had stopped men who tried to help the girls and warned "it is a sinful to approach them".
  The father of one of the dead girls said that the school watchman even refused to open the gates to let the girls out.
  "Lives could have been saved had they not been stopped by members of the Commission for Promotion of Virtue and Prevention of Vice," the newspaper concluded.
  Relatives' anger
  Families of the victims have been incensed over the deaths.
  Most of the victims were crushed in a stampede as they tried to flee the blaze.
  The school was locked at the time of the fire - a usual practice to ensure full segregation of the sexes.
  The religious police are widely feared in Saudi Arabia. They roam the streets enforcing dress codes and sex segregation, and ensuring prayers are performed on time.
  Those who refuse to obey their orders are often beaten and sometimes put in jail.

  Habari ingine kutoka BBC
  8 March 2012 Last updated at 16:36[h=3]Share this page[/h]
  327
  [h=1]Women 'injured' in Saudi university protest[/h][​IMG]Women face restrictions in many aspects of their lives in Saudi Arabia
  Continue reading the main story[h=2]Related Stories[/h]

  An investigation has been launched after at least 50 women were reportedly injured when a protest at a university in Saudi Arabia turned violent.
  Hundreds of women took part in the protest against discrimination and mismanagement at the King Khalid University, in Abha, on Wednesday.
  Dozens were said to have been injured after security forces and religious police moved in to break it up.
  The university said some of the students had attacked staff.
  The BBC's Arab Affairs Editor, Sebastian Usher, says that images of the women shouting in protest against the university authorities were posted on social media and networking websites.
  The women are reported to have been injured either by the security personnel or in the crush of bodies.
  There have been several protests at Saudi universities, or involving recent female Saudi graduates over the past year, mainly complaining about a system that is biased against them.
  The kingdom has also moved to improve rights for women recently - allowing them the right to vote and participate in future municipal elections.
  The students were angry about bad management, that rubbish was allowed to pile up at the university and at the lack of basic facilities for women.


   
 15. SR senior

  SR senior JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 342
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  hakuna cha kutupotezea muda kutafakari hapo...jibu linajulikana, wao wanapeleka mavazi yao ya kishenzi kwenye miji ya wastaarab, wa2 wana tamaduni zao nanyi ni wageni kwann msiheshmu mlichokikuta? Leo hii vyuo kibao vimekataza mavazi ya kuhamasisha ngono zembe waache yawakute, usiposikia la mkuu utavunjika guu!!!
   
 16. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,139
  Likes Received: 7,391
  Trophy Points: 280
  ......Do as Roman do
   
 17. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu usiseme watalii tu...
  Kuna kile chuo cha Tunguu, nadhani kwa Zenji ndio chuo chenye kuongoza kwa kutoa Malaya...
  Kuna watoto wa Kimalawi wanasoma pale ni balaa, maji mara moja tu kama njegere za mbeya...
  Utawakuta bwawani hawana hata hela ya kinywaji wamevaa nusu uchi...
  Wakati wa likizo za mid-semester hawana pa kwenda wengi wao wanawekwa vinyumba pale unguja au kuja dar...

  Kwenda kusakama watoto wa kwenye chuo cha MNMA ni siasa chafu cha vikundi vya kiitikadi hapo zenji...
  Na ni upuuzi wa watu wachache wanaopewa support na tuvikosi twa serikali ya mapinduzi (kimyakimya)
   
 18. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Afu ukitaka kujua ni wanafiki, huku wanasema wafunike afu hapohapo ukiingia kwenye huduma zote (za umma na za binafsi), unakuta
  TANGAZO KUUBWA...."TAFADHALI ONDOA NINJA LAKO" au "TAFADHALI VAZI LA NINJA HALIRUHUSIWI HAPA"!!

  Basi nilikuwa nacheka tu mie, hawa jamaa hawajitambui nadhani hilo ni tatizo kubwa sana kwao kuliko "Tanganyika"
   
 19. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Nadhani inafika wakati tukubali kwamba huu utamaduni wa magharibi umekuwa na nguvu kubwa sana.. Hivyo kujaribu kuuzuia na kubaki na utamaduni wa uarabuni inakuwa ngumu.. Matokeo yake kunakuwa na matokeo hasi ambayo sio mazuri kwa jamii yetu.. Hii kuwatishia na kuwataka wanawake kuvaa hijjab pamoja na lile suala lingine la kuchoma bar na hoteli zinazouza pombe ni matokeo ya fikra hizi hasi.. Utawezaje kuchukua hatua hiyo wakati asilimia 95 yao wanaangalia filamu za kimagharibi..? Wanaangalia muziki wa kimagharibi..? Most of their idols wako Magharibi..? Mwisho wa cku wanajikuta wamevutika kimavazi na mengineo yafananayo na kusahau utamaduni wao..
  Lakini swali jingine la kujiuliza.. Utamaduni wao ni upi..? Utamaduni wetu ni upi..? ulianzia wapi..? Wakati huo mababu zetu walipokuwa wanafunika sehemu ya mbele 2.. Au baada ya kuja Wazungu/waarabu ndo tulipoanzia kuhesabu tumepata utamaduni wetu mpya..?
   
 20. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mavazi ya kishenzi kwenye mji wa wastaarabu? Wastaarabu ndio kina nani hao? Hao wanaochomea watu nyumba, wanaowabagua wenzao, au wewe unaelewaje neno wastaarabu?
  Wazenji hamna lolote nyie ni wanafiki tu, dhambi mloiona ni kuacha nywele nje? Je lile katazo la kwenye Quran ambalo mtu ukilifanya mbingu na ardhi zinatetemeka hilo kwenu halali tu.
  Tatizo lenu ni Watanganyika siyo mavazi, wabaguzi wakubwa nyie.
   
Loading...