Wanafunzi wa leo na simu za mikononi, ufaulu utaongezeka kweli?

Kwa nini mnaiangalia simu kwa upande wa mapenzi tu? Kwa sasa simu ni mojawapo ya resources muhimu katika ufundishaji inawasaidia wanafunzi kupata materials online, kushare materials na kudiscuss in groups virtually

Hebu tubadilisje mind set zetu tuwaruhusu wanafunzi wetu watumie simu na pia nashauri kila mzazi amnunulie mwanae simu na shule pawe sehemu huru kwa mwanafunzi kutumia simu kama itakavyokuwa nyumbani. Haiwezekani mwanafunzi asubiri eti mpaka afike chuo ndio awe huru kutumia simu.
 
wanafunzi kama wachawi vile unaweza kumuona yule pale na simu nenda sasa ukamkague ukuti kitu
 
Umeambiwa hakuna kuongezewa mshahara..sasa unataka ujitume ili iweje...ushitukize wanafunzi upoteze muda bure cheo hupati mshahara hupati...fanya kazi kwa utaratibu uku ukianzisha business nyingine au ukibet (walimu wengi wanabet)
 
Simu kwa kipindi hiki (miaka hii) haikwepeki si kwa watoto, vijana na wazee. Muhimu ni kuweka utaratibu wa matumizi tu. Nyumbani kama mzazi unaweza weka utaratibu kwa mfano muda wa simu ni saa masaa mawili tu kwa siku 12 mpaka 2 usiku, siku za kazi na masaa yanaweza kuwa tofauti siku za weekend. Mashuleni wanaweza kuangalia utaratibu unaofaa kama kuna ulazima. Na ni vizuri kuwafundisha watotot matumizi sahihi ya simu. Kuukana ukweli na uhalisia wa sasa nikujitafutia magonjwa yasiyoambukizwa kwa kasi!!!!
 
Hivi jamani huko mashuleni hasa secondary huwa hakuna siku ya ukaguzi wa kushtukiza maana unakuta mwanafunzi anaenda na simu shuleni bila wasi wasi na wengine unakutana nao kwenye daladala wanachat tu..

Hivi kwa mwendo huu ufaulu utaongezeka kweli...hasa hizi shule za kata yaani ni shida tupu...Walimu mko wapi au mnaona jambo hili ni sawa??
Sidhani kama tunapaswa kuwalaumu walimu

Wazazi na jamii ya Leo imeshindwa kutambua umuhimu wa mwalimu acha tuteketeze kizazi chetu,

Mtoto akienda na sim shuleni, mwalimu akamuadhibu, wazazi na jamii wanamsonta mwalimu na hata serikali haimsaidii.

Saiv walimu wanafanywa kituko, akimgusa mtoto nae anaweza akachezea kichapo,

Kimsingi walimu hawaoni haja ya kuingia migogoro na jamii kisa watoto wa jamii.
Saiv mwanafunzi akiwa mtovu wa nidhamu basi hilo linabaki kwa mzazi
 
Nafikiri ukiwepo ushirikiano kati ya mwalimu na mzazi haya matukio ya wanafunzi kumiliki simu na kwenda nazo shule yatapungua. Mfano hawa watoto wa kike anaweza kumiliki simu hata mzazi asitambue kabisa. Pia kama mzazi ni vizuri kukaa na kijana /binti yako na kumueleza umuhimu wa elimu, faida na hasara za kumiliki simu akiwa mwanafunzi.

Nijuavyo mimi ni vizuri kuweka urafiki na familia yako ili wao pia iwe rahisi kukueleza changamoto walizonazo kama watoto. Pia mzazi ni vizuri kufanya mwalimu sehemu ya familia, kwa maana ya kuwa ndiye anyeshinda na mwanao shuleni kwa muda mrefu hivyo ni rahisi pia kujua mabadiliko ya mwanao, na kukushauri njia sahihi ya kuchukua bila kumuathili mwanafunzi.
 
íѕíngєkuєpσ mítαndασ чα kíjαmíí{fαcєвσσk,ínѕtαgrαm,wαѕαp,twítєr...n.k}nαzαní wαngєѕσmα вílα kuwαzα kumílíkí ѕímu ѕhulєní ѕαѕα kwα hαlí ílívчσ ѕαѕα híví mwαnαfunzí hαnα uvumílívu wα kuѕuвírí kwαnzα αmαlízє mαѕσmσ ndíσ αtumíє ѕímu kwαní αnασnα kαmα чupσ ulímwєngu tσfαutí nα wєnzαkє#KUCHATI
 
Kizazi cha Leo kimeshikwa pabaya. Discipline hakuna. Wajapani the first four years in school ni discipline na maadili. No exam. Sisi birthday mtoto Wa miaka 5 lisimu ama li iPad!!
 
Nafikiri ukiwepo ushirikiano kati ya mwalimu na mzazi haya matukio ya wanafunzi kumiliki simu na kwenda nazo shule yatapungua. Mfano hawa watoto wa kike anaweza kumiliki simu hata mzazi asitambue kabisa. Pia kama mzazi ni vizuri kukaa na kijana /binti yako na kumueleza umuhimu wa elimu, faida na hasara za kumiliki simu akiwa mwanafunzi.

Nijuavyo mimi ni vizuri kuweka urafiki na familia yako ili wao pia iwe rahisi kukueleza changamoto walizonazo kama watoto. Pia mzazi ni vizuri kufanya mwalimu sehemu ya familia, kwa maana ya kuwa ndiye anyeshinda na mwanao shuleni kwa muda mrefu hivyo ni rahisi pia kujua mabadiliko ya mwanao, na kukushauri njia sahihi ya kuchukua bila kumuathili mwanafunzi.
Umenena vyema,

Lkn changamoto tuliyonayo nchini ni jamii, serikali na hata walimu wenyewe kuidharau kazi ya ualimu,

Saiv walimu hawana motisha na kazi yao hivyo hawana ata mda wa ziada na wanafunzi.
Wengine hawana jitihada za ziada kwa wanafunzi.

Mwalimu anaingia darasani anafundisha mda wa kipind ukiisha anaenda ofisini kwa shughuli nyingine mda wa kazi ukiisha anaenda kwenye biashara au mambo yake mengine.

Na actually mm naona wako sahihi maana jamii ya Leo watoto hawaambiliki.
Ukimgusa utaishia mahakamani.

Mm nadhani wazazi tubadilike
 
inasadikika hiyo tu mnayolipwa mnafanya kazi nusu siku ko utaratbu unakuja wanataka mfanye kazi kweli
Walimu wanafanya kazi nusu kweli?

Hakuna fani wanayowajibika na kwakuonewa kama walimu,

Kitaalam teacher student ratio inapaswa kua 1:40 respectively lkn kwa TZ ni 1:200 ata na zaidi.

Mwalimu anastahili kua na vipindi 4,5 kwa wiki BT TZ 20 kwa wiki.
Apo bado hajaandalia, hajasaisha na yuko zamu, mshahara haujatoka, serikali wanamfanyia uhakiki, jamii inamponda n.k.

Kiukweli Mungu awabariki walimu wote kwakua wavumilivu na wazalendo wa nchi yetu
 
hilo nalo jipu kwa wazazi ila wakati mwingine huwezi kugundua kama mwanao anasimu kwani wakati mwinngine mtoto anahongwa na watu na simu inatumika tu chumbani akiwa nyumbani...ww kama mzazi unaweza kujua mtoto wako ana mpenzi au La??
Mbona kazi rahisi kujua sema uzembe wa wazazi kuto waangalia watoto wao mpaka usijue huyo analala nyumba ipi? Kwanini usifanye ziala za kushitukiza mara kwa mara chumbani mwake? Jitu lisilete kisingizio cha namna hii we mzazi gani usiejua mwenendo mzima wa mtoto wako japo kwa mutasali?!
 
Mnazisingizia tu simu.mi nimeanza kutumia simu darasa la saba na haijawahi kuathiri elimu yangu mpaka namaliza chuo
 
Kinachonisikitisha ni kuwa watoto hawalali wako kwenye smart phone na game au kuchat usiku kucha
 
Umenena vyema,

Lkn changamoto tuliyonayo nchini ni jamii, serikali na hata walimu wenyewe kuidharau kazi ya ualimu,

Saiv walimu hawana motisha na kazi yao hivyo hawana ata mda wa ziada na wanafunzi.
Wengine hawana jitihada za ziada kwa wanafunzi.

Mwalimu anaingia darasani anafundisha mda wa kipind ukiisha anaenda ofisini kwa shughuli nyingine mda wa kazi ukiisha anaenda kwenye biashara au mambo yake mengine.

Na actually mm naona wako sahihi maana jamii ya Leo watoto hawaambiliki.
Ukimgusa utaishia mahakamani.

Mm nadhani wazazi tubadilike
Kama taifa inabidi tuwaangalie walimu kwa jicho la pili Mkuu!

Mwalimu ana mchango mkubwa sana katika ukuaji wa uchumi katika Taifa lolote lile lenye mpango wa kusonga mbele. Bahati mbaya sana mitazamo ya watu inaona kuwa mwalimu ni yule anayefundisha elimu ya msingi tu na secondary, na hao ndio wanaodharaulika. Tusijue hawa ndio msingi wa Elimu ya juu. Kwa hali hiyo zile shutuma wazipatazo zinawapelekea kujiona sio bora na kupunguza moyo wa kufanya kazi kwa ufanisi na ndio madhara tunayoyaona sasa. Pia wazazi wanapandikiza chuki na maneno mabaya kwa watoto wao kiasi kwamba hata wanafunzi huonyesha dharau za wazi kwa walimu wao. Na siku zote kama mwanafunzi asipompenda mwalimu wake hata somo husika afundishalo huyo mwalimu lazima u fail tu. Miaka yetu kipindi tunasoma mwalimu alikuwa anaheshimika sana.
 
Ni kweli kabisa.

Saiv mwalimu anakosa heshima na msaada,
Kuna tukio moja nililishuhudie,

Mwalimu wa kike alikua akifundisha form three, gafla mtoto wa kiume akajongea mbele ya darasa akitaka kuomba ruhusa kwa mwalimu ili aende nje,
Mwalimu akamkatalia,
Yule mwanafunzi alimshika titi mwalimu kisha akaenda nje,

Yule mwalimu akaacha kufundisha,
Kaenda kamuelezea Mkuu wa shule,
Mwanafunzi yule akaitwa akapewa barua ya kusimamishwa masomo kwa muda (suspension)
But diwani akaingilia kati na kufuta suspension hiyo, mtoto akarudi shule kama kawaida.

Fikiria hali ya huyo mwalimu kuwepo ktk shule hiyo na hata kuingia darasa hilo.

Then mtu anakwambia, mwalimu akamate wenye simu shuleni.

Wazazi tufanyeni jukumu letu.

Ukijudhuria vikao vya wazazi na walimu unaweza ukadhani ni mapambano,

Kwa namna hii nchi yetu haitakua sawa kielimu na kimaadili,
Yani kila mtu anahisi anahaki ya kumkosoa na kumuadhibu mwalimu, kiukweli tunakosea sana.

Ukiona nchi imepiga hatua kimaendeleo ujue ni kazi ya mwalimu.
 
Sasa unafiki hapo huyo mwalimu atakuwa na ujasiri kweli! Na huyo mwanafunzi atakuwa amejengeka katika nini! Hapo mwalimu akimuona mtoto wa mtu akifanya kosa unafikiri atachukua hatua kweli! Hapo mkuu kunahitaji mabadiliko ya hali ya juu sana kwetu wazazi.

Zamani mwalimu akikuona hata uraiani umefanya kosa lisilo stahili atakusubili shuleni. Utaitwa na kuhojiwa, ukipatikana na kosa unapewa adhabu. Na wala mzazi wako hajui kuwa umepewa adhabu na mwalimu na wewe pia unaogopa kusema kuwa umeadhibiwa. Maana mzazi akajua na kugundua kuwa kweli unakosa naye anakupa adhabu. Hivyo nidhamu ilikuwepo na heshima ya mwalimu ilikuwepo.
 
Back
Top Bottom