Wanafunzi wa leo na simu za mikononi, ufaulu utaongezeka kweli?

thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,447
2,000
Hivi jamani huko mashuleni hasa secondary huwa hakuna siku ya ukaguzi wa kushtukiza maana unakuta mwanafunzi anaenda na simu shuleni bila wasi wasi na wengine unakutana nao kwenye daladala wanachat tu..

Hivi kwa mwendo huu ufaulu utaongezeka kweli...hasa hizi shule za kata yaani ni shida tupu...Walimu mko wapi au mnaona jambo hili ni sawa??
 
prince john john

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
1,668
2,000
Kama mzazi umeshindwa kumpokonya simu Mtoto Wako unataka mwalimu ampokonye ili iweje....?

Simu anachajia nyumbani wewe upo wap kumpokonya..

Vocha anaingiza nyumbani wewe upo kumpokonya..

SMS zinaingia nyumbani wewe upo kumpokonya..

Na hadi kupigiwa anapigiwa nyumbani wewe upo wap kumpokonya....
Kila mtu afanye kazi yake
 
hilo nalo jipu kwa wazazi ila wakati mwingine huwezi kugundua kama mwanao anasimu kwani wakati mwinngine mtoto anahongwa na watu na simu inatumika tu chumbani akiwa nyumbani...ww kama mzazi unaweza kujua mtoto wako ana mpenzi au La??
 
thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,447
2,000
Walimu wenyewe wanaomba namba, wataanzaje kuwazuia!!!
walimu wengi siku hizi ndo wanafanya ufaulu unashuka kwani wamezidi sana kusumbua wanafunzi kuwataka kimapenzi na wanafunzi wakishajua tabia yako huwezi kumfanya lolote hata kama ukimkuta anasimu
 
thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,447
2,000
Mkague mtoto huko chumbani kwake!
Saidieni kulea, tusilaumu walimu kila kitu!
sema mwanafunzi ni mjanja siku zote hata ukisema umkague huwezi kumshika kiurahisi...sema kuna familia zingine wanachanngia kuharibu watoto wao bila wao kujijua. unakuta mtoto yupo primary lakini anamiliki simu kali kisa kwao mambo safi wanaenda na dunia ya leo...
 
saimile

Member
Aug 11, 2017
26
45

Ni kweli!
Na walimu nao wame choshwa na nidhamu ya wanafunzi wa siku his I!
Ukijifanya kuwashauri wanakuzushia hili , ukiwapa adhabu ndo kabisaa unagombana na jamii nzima!
 
tonier

Senior Member
Mar 6, 2014
157
225
Mtoto halelewi na mwalimu pekee hata wazazi wana jukumu la kuwaangalia watt, malezi ya watoto ni changamoto kwa pande zote cha msingi wazazi tujitajidi kuwaangalia watoto wetu jaman tusiwaachie walimu peke yao.
 
thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,447
2,000
Mtoto halelewi na mwalimu pekee hata wazazi wana jukumu la kuwaangalia watt, malezi ya watoto ni changamoto kwa pande zote cha msingi wazazi tujitajidi kuwaangalia watoto wetu jaman tusiwaachie walimu peke yao.
well said
 
Chris14

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
3,084
2,000
walimu wengi siku hizi ndo wanafanya ufaulu unashuka kwani wamezidi sana kusumbua wanafunzi kuwataka kimapenzi na wanafunzi wakishajua tabia yako huwezi kumfanya lolote hata kama ukimkuta anasimu
Mkuu fanya utafiti wa kina. Hii conclusion yako iko shallow sana. Ilitakiwa uangalie ktk angle tofauti mfano; waendesha bodaboda, wazazi, walezi, walimu na jamii ya watu inayowazunguka.
 
thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,447
2,000
kweli wazazi wanatakiwa kushirikiana na walimu kuwalea watoto lakini pia serikali yetu inapaswa kuwajali walimu kwa kuwaongezea mishahara ili kuwapa moyo wa kufanya kazi kwani mwalimu ndo kila kitu katika jamii....
 
saimile

Member
Aug 11, 2017
26
45
Mtoto halelewi na mwalimu pekee hata wazazi wana jukumu la kuwaangalia watt, malezi ya watoto ni changamoto kwa pande zote cha msingi wazazi tujitajidi kuwaangalia watoto wetu jaman tusiwaachie walimu peke yao.
Umenena!
Wazazi tumejisahau sana, na inafikia mahali tunawaogopa watoto!
Tuwe wakali kwa tabia mbovu kwa wanetu ili walimu nao watimize wajibu wao!
Ila walimu wasichukulie udhaifu wa watoto wakawazamisha kabisa!
 
thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,447
2,000
Mkuu fanya utafiti wa kina. Hii conclusion yako iko shallow sana. Ilitakiwa uangalie ktk angle tofauti mfano; waendesha bodaboda, wazazi, walezi, walimu na jamii ya watu inayowazunguka.
Hahahaha sijatoa conclusion hapo nimezungumza kwa upande wa walimu ila hata hao wengine pia wanahusika kwani ndo wanaohonga simu huhuhuhu
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,590
2,000
fundisheni watoto kujitambua hayo mengine mbwembwe tu.. ni kazi ngumu kupambana na utandawazi kwa kuwanyanganya vitu ila wakijitambua watatumia kwa usahihi na mazingira sahihi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom