Wanafunzi wa Kunduchi Girls wafanya mgomo kwa zaidi ya siku 2. TAKUKURU yaanza kumchunguza Mmiliki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

Anwaniya Simu:”UCHUNGUZI” Mtaa wa Jamhuri,
Simu Nambari: 262323315 S. L. P 1291,
Nukushi: 26232332 41101 DODOMA,
BaruaPepe: dgeneral@pcc.go.tz TANZANIA.
Tovuti: www.pccb.go.tz
Unapojibu tafadhalitaja:

TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI


Machi 9, 2021


MKURUGENZI WA TAASISI YA MUNAZZAMAT DAWA AL ISLAMIYA (MDI) - TANZANIA ACHUNGUZWA KWA MAKOSA YA RUSHWA

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – Makao Makuu, inafanyia uchunguzi malalamiko dhidi ya Viongozi wa Taasisi ya Munazzamat Dawa Al Islamiya (MDI) inayomiliki baadhi ya shule nchini ikiwemo Shule ya Kiislamu ya Wasichana – iitwayo KUNDUCHI ISLAMIC GIRLS ya Jijini Dar Es Salaam.

Bila shaka baadhi yenu mlisikia na kuona malalamiko ya baadhi ya wazazi na wanafunzi wa shule hiyo ambayo yalirushwa katika Taarifa ya Habari ya Kituo kimoja cha Televisheni hivi karibuni yakiulalamikia uongozi wa Shule ya Kiislamu ya Wasichana ya KUNDUCHI kwamba pamoja na mambo mengine imekuwa ikishindwa kuwalipa mishahara na posho nyingine, walimu na wafanyakazi wa shule hiyo. Malalamiko mengine ni pamoja na yafuatayo:

Viongozi wa shule ikiwemo Bodi ya Wadhamini ya Shule – inalalamikiwa kwa kusababisha madeni kwa walimu na wafanyakazi wa shule hiyo ambapo inadaiwa kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2021, walimu na wafanyakazi wa shule ya Kiislamu ya Kunduchi wanaidai taasisi ya MDI kiasi cha shilingi Milioni mia nne na sita (406,000,000/=) ambayo Mkurugenzi wake hajataka kuwalipa.

Lalamiko lingine ni kwamba, Mkurugenzi wa MDI akishirikiana na Mkurugenzi mpya wa Elimu wa Shule ya Kunduchi wamekuwa wakiingia mikataba mibovu ya kuikodisha shule hiyo kwa wamiliki mbalimbali bila kufuata utaratibu.

Lalamiko lingine ni uongozi wa MDI kukwepa kulipa Kodi halali za Serikali na hivyo kuisababishia Serikali hasara na kwamba mapato ya shule yamekuwa yakiishia mikononi mwa wajanja wachache ndani ya taasisi ya MDI.

Lalamiko jingine ni kwamba viongozi wa MDI wametangaza kuwaondoa kazini walimu na wafanyakazi wote wa Shule ya Kiislamu ya Kunduchi bila kuwapa malipo yao kwa madai kuwa hiyo ni amri kutoka katika uongozi wa mkoa.

Vilevile, inalalamikiwa kwamba tangu mwaka 2017, ipo BODI YA WADHAMINI inayoongoza shule hiyo, lakini haijasajiliwa katika Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo - RITA.

Kwamba Bodi hiyo ya Wadhamini kwa kushirikiana na viongozi wa MDI, wamejipa mamlaka ya kuidhinisha malipo yote ya akaunti ya shule - jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Viongozi wa Shule pamoja na Bodi ya Wadhamini wanadaiwa kufanya miamala ya fedha isiyo na uwazi.
  • Ndugu WanaHabari,
Kupitia taarifa hii tunapenda umma ufahamu kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Makao Makuu ilishaanza kufanyia uchunguzi malalamiko haya ambayo baadhi ya tuhuma zinaangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007. Mpaka sasa yafuatayo yameshafanyika:

Tumeshafanya mahojiano na baadhi ya walalamikaji,

Tumekusanya baadhi ya vielelezo na pia

Tunaendela kuwaita na kuwahoji walalamikiwa ambapo leo hii Machi 9, 2021 tumemhoji MKURUGENZI WA TAASISI YA MUNAZZAMAT DAWA AL ISLAMIYA (MDI) TANZANIA BW. ALLY MAGOGA

Ndugu WanaHabari,


Lengo la uchunguzi huu pamoja na mambo mengine ni kutaka kufahamu ukweli wa malalamiko haya ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

DOREEN J. KAPWANI
AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU
KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU


---
Pia soma > Mkurugenzi wa Munazzamat dawa Al Islamiya unaibipu PCCB
 
Back
Top Bottom