gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,283
- 3,274
Huu sio muda wake,zaidi yakulalamika hujashauri chochote ni kwa namna gani wanafunzi watarudi nyumbani salama.Haya malalamiko hayana msaada wowote kwa sasaHili ni tatizo halikupaswa kutokea hata kidogo, ni uzembe tu wa nchi za Afrika.
Nchi za Magharibi ikiwemo USA, Australia, Canada zilitoa angalizo kwa Raia kuondoka wiki kadhaa kufuatia taarifa za kiintelejensia. Marekani ilitaarifa kila hatua kiasi kwamba viongozi wa Ukraine walitilia mashaka, leo imedhihirika ni kweli.
Tanzania haikufanya juhudi za kuondoa Raia mapema bali kuwataka watulie na wafuatae maagizo ya maeneo wanayoishi, maeneo tarajiwa ya vita.
Hili lilikuwa jambo la kusikitisha na kuhuzunisha
Yametoke yaliyotokea, tunaposikia hakuna escort, kama ni kweli, kuna maswali ya kujiuliza
Kama Taifa tubadilike, intelejensia za kubaini vibaka na Wapinzani na mabango hazitusaidii katika dunia ya leo inayokwenda kasi.
Tunatumia akili nyingi kwa mambo yasiyo na maana, yanapotokea ya kutumia akili, ima hatuwezi au tumechoka.
Kwa hili, uongozi wa utakwepaje lawama?
JokaKuu Pascal Mayalla