Wanafunzi wa Kitanzania waliokuwa wakisoma Ukraine wote waondoka salama


Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amewahakikishia watanzania kuwa wanafunzi 150 waliokuwa wamebaki nchini Ukraine wapo salama na wamefanikiwa kuvuka na kukimbilia Nchi jirani Za Poland, Hungar , Romania na Denmark.

Akiongea na vyombo vya habari Jijini Arusha,alisema taarifa alizopata hadi Leo (Jana) ni kwamba wanafunzi hao waliokuwa wakisoma chuo kikuu kilichopo mpakani mwa Ukraine na Russia Cha Sumy wamefanikiwa kuvuka salama bila kuwa na ulinzi wowote.

"Hadi Leo asubuhi taarifa nilizonazo kutoka Ukraine ni kwamba wanafunzi wote 150 waliokuwa wakisoma chuo kikuu Cha Sumy kilichopo mpakani mwa Ukraine na Russia wameshavuka Kuelekea nchi jirani baada ya kupatiwa ruhusa ya kuondoka"alisema

Alisema awali wanafunzi wote waliokuwa wakisoma nchini Ukraine ni 300 na baadhi yao walishaondoka na kwenda nchi za jirani na 23 Kati yao walifanikiwa kurejea nchini.

Waziri Mulamula alisema serikali ya Tanzania imekuwa ikipata ushirikiano mzuri na ubalozi wa Russia pamoja na watanzania waishio nchini humo katika kufanikiwa kuondoka Kwa wanafunzi hao

"Serikali ya Russia imetuhakikishia kuwa iwapo wataondoka Ukraine watasaidia kuvuka salama na kufika wa aendako na mpaka Sasa niwahakikishie kuwa juhudi za kidipromasia zinaendelea na mpaka Sasa hatujampoteza mwanafuzi hata mmoja au kujeruhiwa "alisema

Kuondoja Kwa wanafunzi hao wa kitanzania ni kukimbia machafuko yanayoendelea nchini Ukraine baada ya majeshi ya Russia kuivamia Nchi hiyo .

Ends ..

Anataka wajeruhiwe apate kisingizio cha safari
 
Wanafunzi waliokwama Sumy wamewasili salama mjini Moscow nchini Russia na wanatarajiwa kuanza kuondoka alhamis na ijumaa kurudi Dar es salaam, Tanzania.

Source: BBC Dira ya Dunia!
 
Tunaishukuru Serikali na Balozi zetu za Nordic countries. Leo wanafunzi wa Kitanzania wameondoka wote kwa Mabus kutoka Sumy mida ya mchana. Asante Mhe. Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom