Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Yaani we acha tu, udini mwingi lakn matendo ni yaleyale tu. Kuna jamaa yangu nar ni msabato wa jmosi tu lkn kitimoto kama kawaida tunapiga tu.
Wana complication sana hao vyuoni.
Kuna jamaa yangu ni msabato na anaishi na demu wake geto moja.linapofika swala la kufanya mitihani au presentation jumamosi alikua anagombana sana na ma doctor.siku moja nikamwambia mbona unaishi na mwanamke na mnazini huoni hiyo ni dhambi au dhambi ni kufanya kazi jumamosi?amenichukia mpaka leo.wakati mwingine haya mambo ya imani tunajichanganya sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikirejea Ibara ya 19 ya Katiba yetu ya JMT ya Mwaka 1977 inatoia Uhuru wa Mtu Kuabudu.......

Hali kwa Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji ni Tofauti kwani wanafunzi wapatao 8 wamefukuzwa Chuoni hapo kwa madai ya kutofanya mitihani iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi Sabato kwamba kwa kanuni za Chuo hicho hiyo si sababu ya kumfanya mwanafunzi asifanye mitihani

Wanafunzi hao wapo mitaani kwa sasa wakisaka msaada wa kisheria

  1. Je yamkini wakati wanafunzi hao wanapokelewa hilo halikuwekwa bayana?
  2. Mbona Mitihani isiwe Jumapili?
  3. Wapi Uhuru wa Kuabudu kwa mujibu wa Katiba JMT na sheria?

Je mnawashauri nini wanajamvi?

Ni lazima tujifunze kuvumiliana inapokuwa swala la Imani, kwa wa sabato this is very serious na Imani yao sio ya leo wala Kesho ni kongwe sana, ni ujinga na sio u Tanzania kutovumiliana kwenye vitu vya msingi
 
SDA ina ukongwe gani...?? Unataka kutuambia kuwa hiyo imani ya huyo mama Ellen ndio special...???
Hivi nyinyi watu nani kawaloga
 
Una mdharau mwanamke ?
Vyuo vya kisabato vipo waende huko. Ni sawasawa uende kusoma shule yenye misingi ya kiislamu ukatae kujifunza Quran, au usome za kikristo ukatae kusoma biblia, kujifunza sala na kufanya mtihani wake.
Kama umefata elimu hakuna kitakachokusumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
UNAPOSAJILI CHUO AU SHULE KWENYE TAASISI ZA UMMA ZENYE MAMLAKA WANAULIZA MITAALA YA DINI? AU WANUFUATA SHERIA ZA USAJILI
Sijajua, mwenye kujua atueleweshe. Lkn kuepuka hayo kama wewe ni mfata dini mzuri ni bora kuchagua chuo/shule ambayo taratibu zao hazitakukwaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waulize washenzi Wasabato wa SAUT nini kiliwakuta
Unamaanissha hakuna uhuru wa kuabudu kama katiba ya nchi isemavyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo uhuru una Mahala pake....Hebu waende wakafanye huo ushenzi wa Kisabato na u-extrimist wa Ellen G White kwenye taasisi yyte ya Kikatoliki uone moto wake...Waulize historia iliyowakuta Wasabato SAUT ndo utajua.....

Huo ujihad wenu pelekeni huko huko kwenye makambi yenu ya ngono

Hii mada ni ya mwaka 2013! Naomba tafadhali msiwe mna-update mada za zamani na za namna hii ikiwa tu zina maudhui ambayo ni makali. Hizi mada huwa zinafaa tu kujadiliwa wakati wa tukio lenyewe halafu baada ya hapo mnaachana nazo, mada inakuwa haijafungwa ila inajifunga yenyewe.

Hata hivyo naomba nitoe angalizo kuwa as long as Jumammosi huwa haipo kwenye schedule za masomo na wala mitaala ya vyuo haisemi kuwa siku hiyo inaweza kutumika kwa ajili ya masomo au mitihani, ni mtu asiye na hekima tu anayeweza akaingia kwenye mgogoro na watu kwa ajili ya siku hii. Uhuru wa kuabudu ni muhimu sana kwa binadamu, sawa tu kama ilivyo hewa katika maisha ya viumbe hai. Mimi kwa kweli kama nina mamlaka halafu ukatokea kiongozi ukaingia kwenye mgogoro na wanafunzi na ambao unauhusiana na imani yao ya kuabudu, sekunde ni kubwa unakuwa umeshasafisha kila kilicho chako ofisini. Machafuko makubwa ambayo huwa yanakuwa triggered na issues za imani huwa hayasababishwi na vitu vikubwa sana, ni mambo madogo madogo tu kama haya. Tuseme mimi ni msabato, Jumamosi ninatakiwa niende kwenye Ibada, wewe unalazimisha niingie darasani kufanya mtihani? Huu ni uungu mtu, mtu anapewa madaraka halafu anajiona yuko juu ya kila kitu. Tabia mbaya sana!
 
Tusijadili mada za zamani? Waambie mods wazifute

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msituletee ushenzi wenu....SDA ina ukongwe gani...?? Unataka kutuambia kuwa hiyo imani ya huyo mama Ellen ndio special...???
Hivi nyinyi watu nani kawaloga

Mimi wala sio msababato, haukuwa na haja ya kutukana twaweza tu kupishana bila kutoa lugha za kuuzi
 
Kuna jamaa yangu ni msabato na anaishi na demu wake geto moja.linapofika swala la kufanya mitihani au presentation jumamosi alikua anagombana sana na ma doctor.siku moja nikamwambia mbona unaishi na mwanamke na mnazini huoni hiyo ni dhambi au dhambi ni kufanya kazi jumamosi?amenichukia mpaka leo.wakati mwingine haya mambo ya imani tunajichanganya sana.

Ukweli mchungu sana ulimwambia, mwenyewe huwa sielewi vyema hili jambo la sabato. Kuna mademu wa kisabato wanapigwa miti sio kidogo huku kitaa na wana wanakula mademu sio kidogo tena kwenye hizi kwaya usiseme mazeee.
Anyway, hao jamaa waache ujinga buana, mbona wanakuwa kama sio waliompokea kristo. Hivi huwa hawaisomi ijili ya paulo kwa wakolosai na kwa waefeso. Amekataa mambo ya kushikilia sheria za Musa ili kristo alikuja kwajili yetu na yeyote atakayemuamini aokolewe. Sasa mambo ya kushikilia amri ya kutunza siku ya sabato tu alfu amri zingine kama uzinzi na uasherati unafanyika.
Binafs, natambua haki ya kuabudu imani yoyote ili mradi haivunji katiba ya JMT. Waaache unafiki hai vijana wafanye mtihani, na uking’ang’ania utunzaji wa sabato ni sawa na kukataa Neema aliyotuletea Kristo.

Happy dude
 
Hahaha tufike wakati tuwe serious na future zetu maana dunia hii sio kisiwa cha mtu au watu wachache ni cha watu wengi na viumbe kama vyote, swala la kugomea shughuli za taasisi au jamii kwa kigezo cha imani na ukijua fika ulipotaka kujiunga na hiyo taasisi au jamii fulani ulikubaliana na miogozo, taratibu na sheria zake sidhani kama ni hekima na busara au werevu wa kujiwekea vikwazo binafsi ukihisi utasonga mbele vyema. Ni jambo la hatari hao wanafunzi au vijana wenzetu wamefanya na wanahitaji kupewa adhabu kali zaidi ya hiyo ikiwezekana.

Kama wanataka kupata kipaumbele cha yale wanayoamini au kusimamia wanatakiwa kuunda umoja wao kwanza na kufanya utambuzi wa maandishi kwa taasisi usuka juu ya tamaduni zao kama ombi na pale wakishapewa uhalali wa hitaji lao hilo ni rahisi kutoshiriki shughuli za kijamii kama hilo walilogoma/kukahidi kushiriki ikiwa ni Jumamosi maalimu kwao kuabudu. Hata shule ya sekondari niliyosoma walitumia utaratibu wa kuanzisha umoja wa ASSA na uongozi wa shule ukaafikia kuwapa kipaombele cha Jumamosi kuwa excluded na shughuli zote hata wakati wa kufunga walithaminiwa. Hata Uyaudini (Israeli) kuna utaratibu maalum na unaotambulika. Wawajibishwe na wajirekebishe.
 
Ya kaisari apewe kaisari na ya Mungu apewe Mungu, waache kuchanganya dini na taaluma, vyuoni si mahala pa kudumu ni sehemu za kupita tu na kila sehemu kuna taratibu zake, kila mtu kila sehemu akisema afanye kwa jinsi anavyoamini unadhani kuna la maana litaendelea kweli?
Hakuna taratibu zilizo kinyume na katiba. Soma Biblia kutoka 20 kifungu cha 8,9 10 nakuenderea, inawaamuru wasabato siku hiyo wasifanye kazi yyte.
 
Hatuwezi kuvumiliana katika kila jambo,kuna mambo mengine lazima tuambiane ukweli,
Ni lazima tujifunze kuvumiliana inapokuwa swala la Imani, kwa wa sabato this is very serious na Imani yao sio ya leo wala Kesho ni kongwe sana, ni ujinga na sio u Tanzania kutovumiliana kwenye vitu vya msingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona wapinga kristo mmejipanga hapa mnachekelea kuona watumishi wa Mungu wakisimamishwa masomo kwa sababu ya kutaka kuwalazimisha kufanya/kutenda kinyume na maagizo/amri za Mungu.

Kabla hamjaendelea kuropoka ni vizuri mkajisomea maandiko matakatifu na kuyaelewa. Wengi wenu mnaonekana hamuijui Sabato wala hamzijui amri kumi za Mungu kwakuwa mnatumia amri zilizochakachuliwa na mwanadamu.

Kutoka 20:8-11 unasema hivi:
"8Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, 10lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu".

Hiyo ndiyo amri ya Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu, sasa ikitokea kuna mtu mmoja ama wawili wamekwenda kinyume na amri hiyo ama amekwenda kinyume na amri nyengine ya Mungu kati ya zile kumi hiyo haihalalishi uvunjifu wa amri nyengine ama kuwafanya wengine wawe wakosaji ama kushurutishwa kukiuka maagizo ya Mungu kwakuwa wengine walikiuka.

Najua yapo baadhi ya madhehebu ya kikristo yanachuki kubwa sana na Kanisa la Waadventista Wasabato kwa sababu wanazozijua wao wenyewe lakini hilo halijawahi kuwa tatizo kwa Wasabato hata mara moja kwakuwa hiyo sio kazi yao ya kuwahukumu watu.

Kwa wananfunzi Wasabato walioko katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, mimi napenda kutumia fursa hii kuwatia moyo kwamba muendelee kuwa na imani thabiti kwakuwa hayo mnayokutana nayo ni majaribu ya shetani ili kujaribu kupima imani yenu, na kamwe Mungu hatawatupa mkono na hatimaye mtafanikiwa kuhitmu masomo yenu na kupata shahada zenu, aidha hapo mlipo kwa sasa ama mahali pengine.

Napenda niwakumbushe kisa cha Pastor Dkt. Herry Mhando ambaye alifukuzwa shule ya sekondari akisoma masomo ya A Level kwa kukataa kufanya mitihani siku ya Sabato takatifu lakini Mungu alisimama nae na akafanikiwa kusoma hadi kiwango cha kupata shahada zake kadhaa kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambulika na kuheshimika sana duniani.

Pia niwashuhudie kuw mimi binafsi pamnoja na wanafunzi wenzangu tuliwahi kukumbana na mazingira hayo ya kulazimishwa kufanya mitihani siku za jumamosi wakati tukihangaika kujitafutia elimu katika ngazi za elimu ya juu lakini tulisimama imara na hatimaye Mungu akatushindia. Kwahiyo hili linalowatokea sio mara ya kwanza na haitokuwa mara ya mwisho kutokea kuwa shetani anafanya kazi kwa njia mbalimbali na mbinu mbalimbali. Jambo la msingi na la muhimu sana kwenu ni kuendelea kumtegemea Mungu na kufanya mambo yenye kumpendeza Mungu kwani kwa hakika mtashinda tu!
Tusiite watu wapinga kristo ilihali wanamtafuta.
 
Msabato haruhusiwi kutoka jasho na asitembee umbali zaidi ya jiwe litakapododoka baada ya kulitupa toka mlangoni kwake. Ukiwa Dar kuna joto na mtu anatokwa na jasho bila hata ya kutoka nje, hivyo ni dhambi. Kama mtu anatoka nyumbani kwake hadi kanisani ambapo ni mbali na kwake, anatenda zambi. Hivyo kama kuna mazambi hayo mengi itakuwa ni upuuzi kutofanya mtihani ati utatenda dhambi
Hao si wasabato ni wachafuzi wa imani kazi yao kuchafua maana ya sabato. Hawana tofofauti na wale wanaosema waislamu ni magaidi.
 
Kwanza kabla ya mjadala kuendelea, ningependa kujua ni vitu gani ambavyo si ruhusa kwa SABATOS kuvifanya siku ya jumamosi, tukisha jua hilo then, tutaweza kuuweka mtihani katika kundi gani, baadae kutoa maamuzi, karibu..
Hivi mfano ameugua yuko hoi hapelekwi hosp. Mbona ingekuwa Ijumaa au Jpili waumini wake wangefanya mitihani. Hao ni halali kutimuliwa chuo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom