Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Msabato haruhusiwi kutoka jasho na asitembee umbali zaidi ya jiwe litakapododoka baada ya kulitupa toka mlangoni kwake. Ukiwa Dar kuna joto na mtu anatokwa na jasho bila hata ya kutoka nje, hivyo ni dhambi. Kama mtu anatoka nyumbani kwake hadi kanisani ambapo ni mbali na kwake, anatenda zambi. Hivyo kama kuna mazambi hayo mengi itakuwa ni upuuzi kutofanya mtihani ati utatenda dhambi

Shetani wako naona yupo kazini sasa
 
Na seminarini ukila parachichi la paroko tu shule huna...Nidhamu kwanza. wewe unakwenda kwenye chuo chenye taratibu zake unataka uweke taaratibu zako? Kila mmoja akifanya hivyo kwa kisingizio cha UHURU WA KUABUDU na kwa jinsi hizi dini zinavyofumuka utajakuta hata wengine wanakataza kufanya kazi j3 je, tutafanyaje?.
Hivi nani aliwadanganya kwamba hivi vyuo vina taratibu zake?

Hivi vyuo vimeanzishwa kwa mjibu wa sheria za nchi na siyo sheria za makanisa.

Hivi vyuo vipo kwa ajili ya kugudumia pluralistic society na kwa mjibu wa sheria za nchi hasa katiba ibara ya 19, ni haki ya msingi kuwa na uhuru wa kuabudu.

Tatizo ni pale mnapofikiria mnaweza kutumia taratibu/mitizamo ya imani zenu kuamua wasabato wafanya nini. Hii ni sawa na mtu wa dhehebu lingine kushangaa au kumulazimisha padre kuoa au masisters wa kikatoliki kuolewa. It's insense to judge someone's religion on the basis of your faith.

Pamoja na kwamba vyuo vikuu na taasisi nyingine pale bunge lisipotunga sheria vimepewa mamlaka ibara ya 94 ya katiba ya JMT vijitungie taratibu za kujiendesha. Likini pia taratibu na kanuni hizo sharti zisiende kinyume na ibara ya 74: kwamba zisipingane na sheria nyingine za nchi. Ikiwa hivyo hizo kanuni zitakuwa null and void.

Nisisitize vyuo vya private ambavyo havitrain makasisi, watawa na wachungaji bali vinaandaa walimu n.k from different background hiviongozwi na katekisimu wala biblia. Vinaongozwa na sheria za nchi thus why vinawezwa kufutwa Mara Moja na serikali vikibainika vinafanya mambo ya hovyo.

Uhuru wa kuabudu upo kikatiba na wala siyo matakwa ya chuo au mtu yeyote. Hii ni haki yao.

Ushauru: Niwashauri wasabato sasa ifikie mahala watafute hii haki yao mahakamani. Kenya wameweza kufanya hivyo. Haki hailetwi na aliyekunyang'anya.

I wish you all the best to and this simple problem.
 
Hili suala nikiwa katibu wa mambo ya nje na ushiriliano wa vyuo TEKUSo nilitatua kwa hekima.
Dr. Mosses aliwambia chuo ni cha moreviani hivyo atakayekuwepo hapo afuate sheria (bylaws) Akishindwa aondoke walishindwa tena Leo naliona
Mlangoni pameandikwa mwanakondoo kashinda na alama ya msalaba kila inapo takiwa kudumisha raratibu zao
Pia baada ya kulisuruhisha wakafanyia joint mass yao kanisani bila shaka amani ilitawala na kuungwa mkono na wanachuo wengi
 
Ushauru: Niwashauri wasabato sasa ifikie mahala watafute hii haki yao mahakamani. Kenya wameweza kufanya hivyo. Haki hailetwi na aliyekunyang'anya.
Shule za Sekondari zinazomlikiwa na Wakatoliki wameshaanza machakato wa kutokupokea wanafunzi wa Kisabato.....They are very distractive kila mahali.....Zamani Shule za Kikatoliki zlikuwa zinawapokea ila sasa wanachujwa sana..itafika mahali "no Admission kwa SDA"

Muende kwenye shule zenu za makambi na lessoni.....msituharibie Taifa bure
 
Uwepo wa hiki kikundi kikiwa bado kina mitazamo ya ya yule mwanamke tutapata shida sana.....

Imagine dini ya Kisabato imeanzishwa na mwanamke....mwanamke yule kwanza alikuwa na historia ya kuwa na magonjwa ya akili..imagine leo hii watu wanafuata mawazo ya mtu alipatwa na kichaa...matokeo take ndio haya ya kugomea mitihani kwenye chuo cha Kikristo...

Cult religiom ni religion ambayo inabdili kila siku doctrine zake...SDA ipo katika kipindi kigumu cha kubadili sura ya mafundisho yake...kwasasa sermon za Kisabato zimechukua mrengo wa Kipentekoste.....Huku nembo ya awali ya mailaika watatu ikibadiloshwa na kuwekwa logo mpya..

SDA ilikuwa hakuna msalaba kwenye kila kitu chao..ila Logo yao leo ina msalaba...linaendelea kujibadilisha taratibu.. ..
Usidajidanganye waliokusudia kuingiza mambo yao wamukwama.
 
Shule za Sekondari zinazomlikiwa na Wakatoliki wameshaanza machakato wa kutokupokea wanafunzi wa Kisabato.....They are very distractive kila mahali.....Zamani Shule za Kikatoliki zlikuwa zinawapokea ila sasa wanachujwa sana..itafika mahali "no Admission kwa SDA"

Muende kwenye shule zenu za makambi na lessoni.....msituharibie Taifa bure
Kwa shule za Sekondari ni sahihi. Kwa sababu mojawapo ya kazi ya shule za sekondari za madhehebu ni kufanya missionary activities. This can not be done at a higher education. Kudhibiti uhuru wa watu hasa wa kuabudi kwa sababu za kijinga chuo kikuu ni upumbavu na kutokuelewa.
 
Ukiitafsiri hiyo ibara ya 19 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa staili unayotumia utajikuta waumini wa dini fulani yenye vipindi vya sala vitano vya lazima kwa kila siku hawatohudhuria lectures, presentations,wala seminars na hata tests... Cha msingi taratibu zilizowekwa na taasisi husika ya elimu ya juu zifuatwe!
 
This can not be done at a higher education. Kudhibiti uhuru wa watu hasa wa kuabudi kwa sababu za kijinga chuo kikuu ni upumbavu na kutokuelewa.
Unafahamu kuwa Chuo kikuu cha Arusha Jumapili ni siku ya kawaida na Jumamosi ni lazima watu wote wawe kanisani na kufundishwa lessoni..??
 
mkuuu hajanielewa hapo mkuu,siyo kama nawachokoza waislamu ,no lengo langu nilikuwa nataka kusema kwamba siku zote iwe jumapili,jumamosi au ijumaaa, na siku zingine a,bazo wapagani waanaabudu. Chuo kama chuo kisiegamie upande wowote mkuu. mtu yoyote aweze kufanya mitihani regardless siku yake ya kuabudu
Ukiona watu wanapanga siku za kutofanyakazi,wakimbie kama ukoma,hao ni wavivu.Waislamu hata siku ya eid ukiwapa mitihani watafanya,Kenya siku ya Eid,waislamu wanapiga kazi kama kawaida,na hawalalamiki.Ijumaa waislamu wanapiga kazi kama kawaida.
 
The same wise hakuna mtu anayefanyishwa kazi jumapili kwa sababu zozote zile. Huo ndo ustarabu na uelewa
Kufanyishwa kazi??? angali mitihani inafanyika kama kawaida....na Wakristo hawaruhusiwi kusali Jumapili..???

Uone tofauti ya Wakristo na Wasabato, Wakristo wana utii na Jumapili hawaendi Kanisani wanahuzuria vipindi
 
Hao katika msururu wa Amri za Mungu iliyo kuu, kwao ni "kuitunza sabato"! Wamefundishwa na kusisitizwa kuwa "ukiishika" sabato hata kama uko mwizi, mseng'enyi na mzinzi basi Mbinguni badoi halali yako
Acha kupotosha mkuu
Heshimu imani za wengine kama wewe unavyoheshimiwa na wenzio
 
Kufanyishwa kazi??? angali mitihani inafanyika kama kawaida....na Wakristo hawaruhusiwi kusali Jumapili..???

Uone tofauti ya Wakristo na Wasabato, Wakristo wana utii na Jumapili hawaendi Kanisani wanahuzuria vipindi
Una matatizo makubwa sana. Kujiandaa kubisha, kulaghai na kukandia; ni ugonjwa. Unaumwa ugonjwa mkubwa sana.
 
Ya kaisari apewe kaisari na ya Mungu apewe Mungu, waache kuchanganya dini na taaluma, vyuoni si mahala pa kudumu ni sehemu za kupita tu na kila sehemu kuna taratibu zake, kila mtu kila sehemu akisema afanye kwa jinsi anavyoamini unadhani kuna la maana litaendelea kweli?
Wewe ndiyo umenena ingekuwa hivyo hata waislam nao wangeigomea ijumaa, lakini cha ajabu waislam ijumaa wanatinga class muda wa swala ukifika wanakwenda kunako mskiti bila shida, hawa wenzetu wanaharibu siku nzima eti Sabato acha wakione cha moto na misimamo yao isiyokuwa na tija kwenye familia zao na ustawi wa kilichowatoa makwao.
 
k
ni siku yao ya kuabudu.labda kuanzia jioni ya 12 ndio mtiahni unaweza fanyika. hiyo ilikuwa kawaida katika udsm chuo kongwe jumamosi test na mitihani ni usiku au jion kabisa.TEKU wanatapatapa watawarudisha hao

kwanza wewe unaonekana ni mmoja wao, unajipa moyo, kama nawewe ni mmoja wao pole! kafie mbele! sikunyingine acha kufanya vitu vya kizembe kama hivyi, kuna wakati shule iache iitwe shule tu!
 
Back
Top Bottom