Doppelganger
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,858
- 748
Nikushauri tu mwandishi.jaribu kuandika lengo la andiko lako kabla ya kufanya masimulizi ya wapi ulisoma n.k,Utangulizi wako hauendani na andiko zima.
Jana kama wengi wetu tuliamka salaama sana nakuenda kwenye mishe mishe za maisha kama kawaida. Lakini kunamdau alitupa taarifa ya kilichokuwa kinaendelea IFM. Tunashukuru kwa taarifa. Na baadaye niliona kwa macho kwenye ITV taarifa ya saa 2 usiku wanafunzi walivyokuwa wamefunga barabara na kuingia kwenye feri zaidi ya wanafunzi 600. Kweli ummoja ulinipa matumaini sana lakini cha ajabu ni pale nilipoona wanafunzi walipoanza kutembezewa mkong'oto na polisi hadi wengine kutemebelea magoti. Niliona ajabu sana tena nilitokwa na machozi hadi naandika hapa sijalala nikifikiria jinsi ya kuwasaidia hawa wadogo zetu aka waliokimbia hand education nakuingia kwenye soft education. fuatilia post zangu hapa
kwanini nasema hawa jamaa walikimbilia kwenye soft education kwa kuwa wao akili zao zinawaza sana kuwa karibu na fedha ndio maisha. Lahasha mimi siamini, lakini cha ajabu zaidi hawa wataalam wa balance sheet akili zao zote nazani zimekaa kubalance zaidi nje ya kufikiria nini cha kufanya hata kwenye jambo ambalo ni ngumu kwenye maisha yao. Pengine naungana na mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Msingwa wameruhusu akili ndogo kuongoza akili kubwa. Hii halina ubishi kwa chuo kama IFM chukulia jana tu walivyokuwa wameng'ang'ania kwenye feri zaidi ya wanafunzi 600 lakini bila kujua kuwa mbele au feri ilkuwa kwenye maji (bahari).Je kweli waliona madahara ambayo yange wapata? na matokeo yake shemeji zao aka polisi waliwakamua kama hawana akili nzuri maana hawakuwa na pakukimbilia.
kwa nini nasema hivyo? Je, wazazi walio na watoto wao wakiume/wakike wanao rawitiwa, kubakwa, na pengine kupigwa nondo unazani wanajisikiaje kusikia matukio kama haya? Je, IFM hakuna wazazi walio olewa/kua. hakuna wachumba wanaosoma pale wakiwa na wenza wao nje ya chuo? Je, akisikia kuna mambo kama haya je, jamii inawachukuliaje? sipendi kuamini kama mimi hapa nilivyo na huzuni ila ninaimani ni wengi sana tena mamia ya watanzania wanahuzuni kama mimi hapa kutokana na nilichokiona jana na kukisika masikioni mwangu. Swali, Je, tunaandaaa jamii ya aina gani on the future?
mimi sio mwanataalum wa uandishi naomba niende kwenye point. Kwanza kabla sijaja kwenye nini kifanyike naomba tu kama kuna mzazi/mlezi/mchumba/mme/mke/kaka/dada/mjomba nk. humu anamtoto yuko IFM basi kuna haja ya kuniunga mkono wale watoto walitakiwa kuchapwa viboko kama sio kibao. Kwa nini nasema hivyo? Chukulia sisi tulikuwa tunasoma Mbeya Technical college (MTC) miaka ya nyuma huko leo hii Mbeya University of Science and Technology (MUST). Sikuweza kuona ujinga kama huu, hata pale UDSM, sijawahi sikia ujinga kama huu. sikatai vibaka wapo sawa kila sehemu ya nchi yetu kama si Afrika kwa ujumla.Mwanataluma nijuavyo mimi ni askari kwa akili aliyonayo anaweza fanya upeleleza, anaweza kujilinda yeye kama yeye, anaweza fundisha jamii kutoka na taaluma yake? Je, kwa kinachotokea IFM twaweza pata nini sisi wanajamii? ni maadili au? sinakumbukumbu sana kama sijakosea hata mwezi haujapita nilisikia redioni watoto wakike wanaandamana kupinga kuzuiliwa kuvaa nguo fupi sijui ni IFM au nichuo kingine lakini kumbukumbu zangu ni kama IFM leo hii ndio wanakuja na ujinga kama huu kuna haja yakubaidilika kabisa kiakili, maadili hata kimuonekano.
Sisi kipindi kile tunasoma pale MTC tulikuwa na ummoja wa hali ya juu sana ninaimani kama kuna wanaMTC humu watakubaliana na mimi haswa wa miaka ya nyuma sio leo. Chuo cha MTC kiko kama 4km kutoka Inyunga barabara ya mbeya Tunduma nakiko nje ya mji yaani kwa kifupi naweza sema ni porini. lakini sijawahi sikia mwanafunzi kapingwa nondo, kabakwa, karawitiwa. wizi wa kuibiwa kwenye mabweni ulikuwa wa nadra sana tena wezi walikuwa wanashiirkiana na wanafunzi wenzetu. Lakini ninakwambia hata kama suruali au kiatu kimeibiwa zaid ya mwezi kilikuwa kinapatiaka kwa njia nitakazo zitaja hapo mbeleni.
binafsi nakuunga mkono kwa point yako ya kupinga hao wanachuo kujazana kwenye kivuko kwa lengo lao la kushinikiza madai yao. uko sahihi kabisa. tatizo langu topic yako iko vipande vipande...ungeiweka pamoja katika para. pili sioni kama ni sawa kulinganisha mazingira ya Mbeya na Dar...mazingira na watu ni tofauti katika maeneo hayo mawili. otherwise concern yako ni sawa!
Mkuu nimekusoma, usiwajibu wale wote watakao kuwa wanauliza maswali ya ku'kuprovock'. Jibu maswali/ hoja zenye mlengo wa kutaka kueleweshwa tu!umesoma post zangu na kuzielewa au? mbona mnapenda kuatafuniwa kila kitu?
kaeleza mengi tu. ila kwa kifupi anahubiri sera ya jino kwa jino!
kwaa kusema mazingira ya mbeya na Dar ni tofauti sijamaanisha kwamba wanachuo wa IFM hawapaswi kujiwekea mfumo wa ulinzi. nina maana tofauti kabisa. hebu rudia kusoma topic ya mhusika na comment yangu, utaelewa!kwa hili hakuna kujitetea kwa kusema "mazingira hayafanani" basi kama ni hivyo nyie hamfai kuwa wapiganaji, kwa mpiganaji hakuna cha mazingira. mimi nilikuwa Tanga Technical zamani, tulikuwa tunapaita Kiungani, hapakuwa na askari wa kulinda shule lakini eneo la shule hakatizi mtu, anaweza kufa, na mabweni hayafungwi mulango tukiwa madarasani.
kwanza napenda nitoe historia ya MTC kidogo MTC ni chuo kilichokuwa kinaundwa na kozi zifuatacho: Mechanical, Electrical, Civil, na Architecture engineering japo ilikuwa ni elimu ya Fundi mchundo lakini ilikuwa nielimu ya Chuo kikuu kwa 75%. kwanini nasema hivyo? kwa sababu wanafunzi walikuwa huru sana hatukuwa na uniform za kuvaa tulikuwa tunaishi maisha ya raha mastarehe kama kufikwa (kuleta mwamke/msichana) ilikuwa ni ruksa na ilikuwa ni fahari kwa mkuu wetu wa chuo kipindikile Mzee Zuberi. Masomo yalikuwa magumu sana na tulikuwa tunaandaliwa sikuendelea na shule bali kwenda kufanya kazi. Maana kipindikile kwenda Chuo Kikuu bila na kuwa na B ya mathematics na at least masomo yako wastani wake lazima uwe C huwezi pata. Nje ya hapo kuapata hata cheti ilikuwa ngumu umesoma miaka yako 3 kwa kuruka viunzi kila term na mitihani yake ukifail nyumbani na mwishoni sasa unakusanya material yote ya mwaka wa kwanza unafanyia mtihani wa kwa masaa 3. Si hivyo tu ukipata "A" 5 kati ya masomo 6 ukafail moja hupati cheti na ukirudia mtihani ukafail mara 2 basi cheti hupati milele, ilikuwa ni bora kupata "D" zote iliuweze kuchukua cheti. Lakini istoshe kuipata hata 'D" haikuwa rahisi maana range yake D=(50-69), C=(70-79) B=(80-89) A=( 90-100)haikuwa rahisi sana wadau kuweza kuendelea na chuo kikuu au hata elimu ya juu
Lakini hawa IFM wanaojiita watoto wa mjini naona ndo wametumia mbinu za zamani halafu itakuaje mtoto wa mjini udhibitiwe kirahisi vilewangekuwa wa bush si wangekufa kabisa,hili la matukio ya kulawitiwakidogo ni gumu kulielewa mazingira gani huwa yanatokea haya mattizo labda watueleshe zaidi ili tuweze changia maada.Mtoa maada kanifurahisha inaonekana vijana wa MTC thinking ilikuwa kubwa maana mlijua kuwa mkitangulia tu kuingia ukumbini mgedhibitiwa kirahisi.Mwisho maada yake pia kuielewa inahitaji ufikiri kidogo ukitumia vionjo tu utaishia kusema sijaona kitubinafsi nakuunga mkono kwa point yako ya kupinga hao wanachuo kujazana kwenye kivuko kwa lengo lao la kushinikiza madai yao. uko sahihi kabisa. tatizo langu topic yako iko vipande vipande...ungeiweka pamoja katika para. pili sioni kama ni sawa kulinganisha mazingira ya Mbeya na Dar...mazingira na watu ni tofauti katika maeneo hayo mawili. otherwise concern yako ni sawa!
Lakini hawa IFM wanaojiita watoto wa mjini naona ndo wametumia mbinu za zamani halafu itakuaje mtoto wa mjini udhibitiwe kirahisi vilewangekuwa wa bush si wangekufa kabisa,hili la matukio ya kulawitiwakidogo ni gumu kulielewa mazingira gani huwa yanatokea haya mattizo labda watueleshe zaidi ili tuweze changia maada.Mtoa maada kanifurahisha inaonekana vijana wa MTC thinking ilikuwa kubwa maana mlijua kuwa mkitangulia tu kuingia ukumbini mgedhibitiwa kirahisi.Mwisho maada yake pia kuielewa inahitaji ufikiri kidogo ukitumia vionjo tu utaishia kusema sijaona kitu