herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,345
Wasalaamu wanajukwaa!
Hivi karibuni Tanzania Commission for Universities - TCU ilibadilisha kwa kupanga upya viwango, vigezo na sifa vya udahili wa wanafunzi kujiunga na vyuo vikuu kwa upande wa wahitimu wa Diploma na wale walohitimu kidato cha sita au Form six.
Viwango hivyo vipya vimebadilishwa gafla na TCU na kutaka vitumike tena kipindi ambacho wanafunzi tajwa hapo juu wamekwisha fanya mitihani yao ya mwisho na wanasubiria matokeo.
Wanafunzi wengine wengi tuu walikwisha fanya application HESLB na kulipia ada ya udahili wakitumia viwango vya awali hawa wamedhulumiwa fedha yao.
Wanafunzi wote waloathiriwa kwa namna yoyote ile kimwili na kisaokolojia kwa uamuzi huo wa TCU kubadilisha viwango vya udahili kwa haraka ni muda sasa kufungua kesi mahakamani dhidi ya TCU kwa kufanya dhulma ya fedha za wanafunzi waliokwisha fanya application.
Ni wakati sasa kudai na kuitafuta HAKI yao mahakamani sababu TCU wamefanya uzembe na dhulma kwa wanafunzi hawa hivyo yafaa waburuzwe mahakamani na kuwajibishwa kwa uzembe huo ulosababishwa usumbufu na matatizo makubwa kwa wanafunzi.
TCU wawajibike kwa hili na inapaswa walipe kwa kurudisha zile fedha na gharama nyingine zote zilizotumiwa na wanafunzi wakifanya application pamoja na muda walotumia.
Hilo likifanyika itakuwa ni fundisho kwa TCU na taasisi nyingine zinazoendesha Elimu ya juu kuacha kufanya maamuzi ya haraka kwa kukurupuka na kuwaumiza wanafunzi.
Tunahitaji Elimu bora na haitopatikana kwa kuhangaika na vitu visivyo na maana kama kubadilisha viwango vya kujiunga na elimu ya juu sababu tatizo la elimu ya Tanzania ni mfumo mzima wa elimu kuwa mbovu kuanzia Primary level to High education pamoja na mitaala inahitaji kufanyiwa marekebisho ili iendane na high rate of growing science and technology in the world.
Sababu walizotoa TCU kubadilisha hivi viwango ni kuwa wahitimu wa vyuo vikuu kutokuwa na ubora unskilled na kukosa creativity inapelekea waajiri kulalamika.
Hili tatizo naomba TCU inayoongozwa na wasomi waliotukuka wafahamu haiwezi kutatuliwa kwa kubadilisha viwango vya kujiunga na vyuo vikuu sababu wahitimu kukosa competence kwenye soko la ajira halisababishwi na viwango kuwa vidogo kujiunga chuo kikuu.
Wadau wa elimu tunataka mshughulikie matatizo makubwa yanayoendelea kuua elimu yetu kufanya iwe bora na yenye kuleta tija kwa jamii na taifa sio kufanya maamuzi ya hovyo yanayozidi kuua Elimu.
Maamuzi haya mabaya mfahamu kuwa yanazidi kutupeleka gizani tunahitaji ELIMU BORA itayokuwa mwanga kwa jamii ya watanzania.