Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Oxford wataka Picha ya Malkia Elizabeth iondolewe

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,587
215,181
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wamepiga kura Kuiondoa picha ya Malkia katika majengo ya chuo chao kwasababu inawakilisha ukoloni-Manchester Evening News
1623228088348.png

Moja ya wachangiaji anasema Malkia pia Mkuu wa Jumuia ya Madola ni alama ya wachache wanaojiona bora kuongoza wengi duniani.

Isitoshe hao wasomi wa Oxford ndiyo wanaowafundisha historia kule walikoiharibu historia yao.
 
View attachment 1813190
Moja ya wachangiaji anasema Malkia pia Mkuu wa Jumuia ya Madola ni alama ya wachache wanaojiona bora kuongoza wengi duniani.

Isitoshe hao wasomi wa Oxford ndiyo wanaowafundisha historia kule walikoiharibu historia yao.
Kumekucha!
Mwanzo wa mwisho wa utawala huu!
 
Chuo chenyewe kimejengwa kwa fedha za utumwa na ukoloni, hivyo, kama wanataka kupinga historia ya utumwa na ukoloni, kwanza wajiondoe chuoni.

Otherwise ni mambo ya "Baniani mbaya, kiatu chake dawa"

Nchi nzima imejengwa kwa misingi ya utumwa na ukoloni, leo unaenda kulalamikia picha ya Malkia.

Kama si unafiki ni nini?
 
Wote wasome hapa halafu wainue viuno warudi makwao 🤣🤣🤣🤣
 
Nilisoma jinsi Chief wa Wazulu , Chief Cetewayo alivyo ongoza mapigano kupinga Makaburu na Waingereza kuvamia Afrika ya Kisini. Vita ya kwanza Wazulu walishina kwa kutumia upinde na mishale pamoja na mikuki.

Wazungu walienda kujipanga na walirudi na kikosi kazi chanye bunduki. Waliwauwa Wazulu wengi sana na Cetewayo walimpeleka London. Alifanya maongezi na Malkia Victoria, walimmaliza nguvu. Kutoka hapo alikua puppet wa Wazungu mpaka kifo chake.
 
Noti za fedha za Uingereza zina picha ya Malkia, wametaka picha ya Malkia iondolewe kwenye fedha pia?

Au fedha wanatumia tu lakini wanashikia bango picha?
Hii issue imekaa kimtego, wakukubali kutoa picha kinachfuatia watahoji umuhimu wa familia ya kifalme katika sasa hivi.
 
Ukishakubali kwenda kusoma Oxford umeshakubali mfumo ulioiweka Oxford.

Wanachofanya hapo ni sawa na mbunge kuhoji uhalali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mabadiliko hayawezi kutokea haraka. Angalau wanaishi kwenye nchi inayotuhusi maoni na vijana wameonyesha ujasiri wao.

Dunia imebadilika, zamani noble families waliona wenyewe lakini sasa hivi huhitaji kuwa wa noble family kuwa tajiri. Unaweza kuwa actor na celebrate mwenye pesa kuliko nobles.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom