Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,192
- 3,353
Binafsi nikiwa kama muhasibu nijitolee mfano tu. Nimesoma Chuo cha Uhasibu Arusha, pale Njiro. Nimesoma vyote anavyotakiwa kuvijua muhasibu kuanzia ratios, kuandaa financial statements, kufuata sheria za IAS, ukaguzi, ethics za kazini, financial management, nimesoma sheria za kodi na hesabu zake, na vingine vingi tu, hivi vitu nlivyosoma pia havipo tofauti na vinavyofundishwa vyuo vingine kama UDSM, TIA, IFM, Mzumbe, n.k. Sasa hapa nani anaanzaje kumzidi fulani kwamfano?
Kazini sijaona chochote kinachohusiana na elimu ya chuo kinachomfanya fulani wa chuo fulani awe bora kuzidi fulani wa chuo fulani, unajua kwanini?
Nimeshajibu kwamba walochofundishwa chuo A, B, C ndicho nilichofundishwa, sasa utofauti wa huu uongo wa kuiva unatoka wapi, labda kuna vile vyuo kama huko TEKU ndio nasikiaga watu wanafundishwa na walimu wasio hata na CPA wala Masters na walimu hucheleweshewa mshahara
Kwenye kuzidiana sanasana ni jitihada zako binafsi tu za kuwa mchapa kazi maana kuna vipanga wa chuo wakijaga kupiga mzigo kazini vile vitabia vya kutoka toka nje, uvivu, kusingizia kuumwa, n.k vinamfanya mtu mchapa kazi mwenye cheti feki aonekane kaiva.
Binafsi nina expert skills za kutumia compiter kuanzia excel, kupiga window, kutengeneza software, n.k kwa kiwango ambacho kinawashangaza wengi mno ofisini, kuna wakati nachanganywa kwamba mi ni IT, nikiri tu kwamba panapotokega kukwama kwenye computerized accounting basi mimi ndio huwa naitwa, na wengi kuanza kuanzisha mijadala ya kipuuzi kwamba wanafunzi wa chuo nlichosomea wameiva kumbe ni jitihada zangu binafsi maana kuna niliosoma nao formula tu za excel hadi wagoogle na si ajabu hata vyuo vingine hali ipo hivyo.
Kwa hiyo ndio hivyo, huu upuuzi wa wanafunzi wa chuo flani wameiva sijauona kiuhalisia, kazini wanakujaga hapa wanafunzi wa vyuo vinavyodharaulika kimakosa kama CBE wakidhaniwa hawana uwezo ila wakianza kuchapa mzigo wanawatoa knock out wenzao wa vyuo vingine, kazi ni jitihada sio kulala mbongo wa uliposomea.
Chapa mzigo ndio utaonekana umeiva,