"Wanafunzi wa chuo fulani wameiva" Hivi huu upuuzi bado upo?

Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,219
2,000
1583526410446.png
Mimi nashangaaga hii dhana aliianzishaga nani, yani yanageuka hadi kuwa malumbano sasa πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ Sijui wanafunzi wa X wameiva na mwengine anatetea kwamba wanafunzi wa chuo Y wameiva, na ni mara nyingi sana kila mmoja kanywa maji ya bendera.

Binafsi nikiwa kama muhasibu nijitolee mfano tu. Nimesoma Chuo cha Uhasibu Arusha, pale Njiro. Nimesoma vyote anavyotakiwa kuvijua muhasibu kuanzia ratios, kuandaa financial statements, kufuata sheria za IAS, ukaguzi, ethics za kazini, financial management, nimesoma sheria za kodi na hesabu zake, na vingine vingi tu, hivi vitu nlivyosoma pia havipo tofauti na vinavyofundishwa vyuo vingine kama UDSM, TIA, IFM, Mzumbe, n.k. Sasa hapa nani anaanzaje kumzidi fulani kwamfano?

Kazini sijaona chochote kinachohusiana na elimu ya chuo kinachomfanya fulani wa chuo fulani awe bora kuzidi fulani wa chuo fulani, unajua kwanini?

Nimeshajibu kwamba walochofundishwa chuo A, B, C ndicho nilichofundishwa, sasa utofauti wa huu uongo wa kuiva unatoka wapi, labda kuna vile vyuo kama huko TEKU ndio nasikiaga watu wanafundishwa na walimu wasio hata na CPA wala Masters na walimu hucheleweshewa mshahara

Kwenye kuzidiana sanasana ni jitihada zako binafsi tu za kuwa mchapa kazi maana kuna vipanga wa chuo wakijaga kupiga mzigo kazini vile vitabia vya kutoka toka nje, uvivu, kusingizia kuumwa, n.k vinamfanya mtu mchapa kazi mwenye cheti feki aonekane kaiva.

Binafsi nina expert skills za kutumia compiter kuanzia excel, kupiga window, kutengeneza software, n.k kwa kiwango ambacho kinawashangaza wengi mno ofisini, kuna wakati nachanganywa kwamba mi ni IT, nikiri tu kwamba panapotokega kukwama kwenye computerized accounting basi mimi ndio huwa naitwa, na wengi kuanza kuanzisha mijadala ya kipuuzi kwamba wanafunzi wa chuo nlichosomea wameiva kumbe ni jitihada zangu binafsi maana kuna niliosoma nao formula tu za excel hadi wagoogle na si ajabu hata vyuo vingine hali ipo hivyo.

Kwa hiyo ndio hivyo, huu upuuzi wa wanafunzi wa chuo flani wameiva sijauona kiuhalisia, kazini wanakujaga hapa wanafunzi wa vyuo vinavyodharaulika kimakosa kama CBE wakidhaniwa hawana uwezo ila wakianza kuchapa mzigo wanawatoa knock out wenzao wa vyuo vingine, kazi ni jitihada sio kulala mbongo wa uliposomea.

Chapa mzigo ndio utaonekana umeiva,
 
Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
7,871
2,000
kwenye Interview umesema wanaangalia uliposoma(ambako wanasema wameiva)..sasa ambao hawajaiva(wrong perception) watapitaje?
 
GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
4,472
2,000
Kazini tunahitaji skills sio vyeti.

Vyeti ni sawa, lakini tunahitaji maarifa na tuone kweli maarifa hayo yanatumika na yanajithibitisha!
 
Oct 15, 2019
40
125
Mimi nashangaaga hii dhana aliianzishaga nani, yani yanageuka hadi kuwa malumbano sasa πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ Sijui wanafunzi wa X wameiva na mwengine anatetea kwamba wanafunzi wa chuo Y wameiva, na ni mara nyingi sana kila mmoja kanywa maji ya bendera.

Binafsi nikiwa kama muhasibu nijitolee mfano tu. Nimesoma Chuo cha Uhasibu Arusha, pale Njiro. Nimesoma vyote anavyotakiwa kuvijua muhasibu kuanzia ratios, kuandaa financial statements, kufuata sheria za IAS, ukaguzi, ethics za kazini, financial management, nimesoma sheria za kodi na hesabu zake, na vingine vingi tu, hivi vitu nlivyosoma pia havipo tofauti na vinavyofundishwa vyuo vingine kama UDSM, TIA, IFM, Mzumbe, n.k. Sasa hapa nani anaanzaje kumzidi fulani kwamfano?

Kazini sijaona chochote kinachohusiana na elimu ya chuo kinachomfanya fulani wa chuo fulani awe bora kuzidi fulani wa chuo fulani, unajua kwanini?

Nimeshajibu kwamba walochofundishwa chuo A, B, C ndicho nilichofundishwa, sasa utofauti wa huu uongo wa kuiva unatoka wapi, labda kuna vyuo kama huko TEKU ndio nasikiaga watu wanafundishwa na walimu wasio hata na CPA wala Masters.

Kwenye kuzidiana sanasana ni jitihada zako binafsi tu za kuwa mchapa kazi maana kuna vipanga wa chuo wakijaga kupiga mzigo kazini vile vitabia vya kutoka toka nje, uvivu, kusingizia kuumwa, n.k vinamfanya mtu mchapa kazi mwenye cheti feki aonekane kaiva.

Binafsi nina expert skills za kutumia compiter kuanzia excel, kupiga window, kutengeneza software, n.k kwa kiwango ambacho kinawashangaza wengi mno ofisini, kuna wakati nachanganywa kwamba mi ni IT, nikiri tu kwamba panapotokega kukwama kwenye computerized accounting basi mimi ndio huwa naitwa, na wengi kuanza kuanzisha mijadala ya kipuuzi kwamba wanafunzi wa chuo nlichosomea wameiva kumbe ni jitihada zangu binafsi maana kuna niliosoma nao formula tu za excel hadi wagoogle na si ajabu hata vyuo vingine hali ipo hivyo.

Kwa hiyo ndio hivyo, huu upuuzi wa wanafunzi wa chuo flani wameiva sijauona kiuhalisia, kazini wanakujaga hapa wanafunzi wa vyuo vinavyodharaulika kimakosa kama CBE wakidhaniwa hawana uwezo ila wakianza kuchapa mzigo wanawatoa knock out wenzao wa vyuo vingine, kazi ni jitihada sio kulala mbongo wa uliposomea.

Chapa mzigo ndio utaonekana umeiva,
Ndugu nakuunga mkono kwa asilimia zote.
Ni ushamba ambao watu wa chuo flan wanao. Yaani huko kujisifu kwao ndio kunaonyesha ni kiasi gani hawajaelimika na hawajui Nini maana ya elimu.
Inasikitisha kuona wasomi ambao kichwani ni empty na wanajitapa kuwa wako vizuri.
 
Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,219
2,000
Bandugu nakuunga mkono kwa asilimia zote.
Ni ushamba ambao watu wa chuo flan wanao. Yaani huko kujisifu kwao ndio kunaonyesha ni kiasi gani hawajaelimika na hawajui Nini maana ya elimu.
Inasikitisha kuona wasomi ambao kichwani ni empty na wanajitapa kuwa wako vizuri.
Yani watu wamekunywa maji ya Bendera aisee, na wengi wao wanakuaga ni wanafunzi au wahitimu ambao bado hawajaajiriwa.
 
Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,116
2,000
Na huku kitaani wote tunachapwa na maisha hatari. "Akili nyingi hupoteza maarifa"
 
mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,338
2,000
Umetaja vyuo vyote ni bora na wanafunzi wanaotoka wanakuwa sawa.Hapohapo umewaponda TEKU kwa habari za kusikia tu zisizo na uthibitisho sasa huoni kuwa na wewe unaingia mkenge uleule.?
Lakini twende mbele turudi nyuma ukweli ni kwamba ubora wa vyuo ni unatofautiana japo wanafunzi wa chuo A anaweza kuwa bora kuliko wa chuo B kutokana na uwezo binafsi.Huwezi kulinganisha mtu aliyesomea sheria SAUT na aliyesomea Oxford au Harvad au mtu aliyssomea muhimbili na aliyesomea John Hopkins kisa tu eti wote wamesomea kwenye upasuaji wa figo.Utofauti upo na Mungu mwenyewe muumba wa mbingu na nchi ndiye aliyeweka utofauti.
Kuna mimea ni dawa na kuna mimea ni sumu hivyohivyo katika vyuo vyetu na maisha yetu kwa ujumla,utofuti upo.Ushawahi jiuliza wale wa Tabora boys,Ilboru,Kibaha,st.Fransis ukifika chuo unakuta wote mliosoma st.Kayumba na waliosoma shule kubwa hapa nchini wote mnapata Coursework ya kuungaunga?Lakin pia wapo wanaokuwa vizuri tangia chekechea hadi kazini hadi wakiwa wazee bado wanakuna na high intelligence.Hizo ni tofauti tu.Mambo ya kutambiana vyuo ni ushamba na ujinga tyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki chuo kilikuwa chini ya taaluma na ndio maana kimeshafungiwa kudahili wanafunzi wa degree kama Mara tatu hivi, hata branch ya dar imefungiwa kabisa kudahili hata diploma na cheti.

Mkuu hapo teku sijaropoka, ni Mara kwa Mara walimu wamekuwa wakilalamika kucheleweshewa mshahara kitu kinachofanya ufanisi upungue, hii unaweza kupelekea kuanza kuomba rushwa kwa wanafunzi ili wapite mitihani.ikumbukwe kipindi flani walimu walifanya mgomo mpaka Ffu wakaja.

pia kuna kuna lecturers wanaofundisha degree nao ni wahitimu wa degree hiki ni kituko.
 
Top Bottom