Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,395
WANAFUNZI zaidi ya 400 wa Chuo cha Ualimu Moshi zamani Mong'are kilichopo Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro wamefunga barabara na kuzuia shughuli nyingine za usafirishaji wakishinikiza serikali kuingilia kati sakata la utapeli wa zaidi ya Sh.milioni 75 za malipo ya ada.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limeingilia kati maandamano hayo na kuwakamata wanafunzi waliokuwa wanaandamana kudai kulipwa zaidi ya Shilingi milioni 75 malipo ya ada wanazidai kutapeliwa na uongozi wa chuo.