Wanafunzi Vyuo Vikuu Tanzania Hawawazi zaidi ya Boom?

Tz Asilia

Member
Oct 30, 2009
45
1
Wanafunzi Vyuo Vikuu Tanzania Hawawazi zaidi ya Boom? imekuwa ni jambo la kawaida kusikia na kuona kwenye vyombo vya habari wananafunzi vyuo vikuu tanzania wakigoma, mandamano kisa Boom halijatema,leo UDSM,kesho UDOM, keshokutwa TUMAINI,mara IFM sina maana kwamba wasomi wetu wasidai haki zao ila misingi yanyu ni kwamba ni lazima tu iwe boom ndio wasomi wetu wagome na kuandamana? kama kioo cha jamii wasomi wetu wanatakiwa kuwa mifano hai wa kuigwa na jamii ya Kitanzania,hivyo wawe wanagoma na kuandamana na kutoa matamko mbalimbali kwa vitu vinavyo gusa jamii kwa ujumla endepo serikali na taasisi zake zimelega au kushindwa kutekeleza au mf: Constitution review bill, Richmond, Dowas, Loliondo Land issue, Kupanda kwa gharama za maisha to mention but a few. Wasomi wetu badilikeni.
 
kaka tulienda kujadili muswada wa katiba tulifukuzwa kwa risasi za moto na mbomu...!
 
Hawawazi zaidi ya Boom, sijakupata hapa? unamaanisha nini? liswahili hiki au kinyarwanda
 
hahaha Ivuga " boom" ni ile meal and accomodation allowance wanayopewa wanafunzi wa elimu ya juu nchini!
 
boom ndilo linalowaweka chuo ili waweze kusoma, ni haki yao kudai kwa maandamano lakini kwa kuandamana kudai mambo mengine kutawapotezea muda wa kusoma.nakumbuka nkiwa chuo ile tumeingia 2000 tukatimuliwa kisa tulidai ongezeko la boom na baada ya muda tukaongezewa 500 tu. Kwa wanaojua maisha ya vyuo siwapingi ila kudai mengineyo kunapoteza muda wao. unadhani watakuwa na mwamko wa kudai mengineyo wkt sheria zinawabana??nani yuko radhi kufukuzwa chuo tofauti na madai yao kama wanafunzi?
 
kumbe kutokuwaza ndio kigezo cha kujiunga vyuo vikuu...na mie naanza leo kutokuwaza labda nitapata udahili.
 
Inauma uchungu kuona mnanyimwa hela ndogo hivyo wakati mabilioni yanatumika kuandaa hafla za kupongezana na kutolea salam za pongezi magazetini na maredioni(kama ilivyoripotiwa majuzi). Halafu kama ni mkopo si tupewe tunaotaka halafu tutalipa... Aaaaaagh.....
 
Kwahiyo we unavyowaza 'maandamano ndiyo yanayoonyesha mtu akiwazacho??'.... Kwahiyo wasingeandamana kwaajili ya boom ungesema hawawazi kitu!??...
Ivii.. unajua mawazo ninini??
 
Wanafunzi Vyuo Vikuu Tanzania Hawawazi zaidi ya Boom? imekuwa ni jambo la kawaida kusikia na kuona kwenye vyombo vya habari wananafunzi vyuo vikuu tanzania wakigoma, mandamano kisa Boom halijatema,leo UDSM,kesho UDOM, keshokutwa TUMAINI,mara IFM sina maana kwamba wasomi wetu wasidai haki zao ila misingi yanyu ni kwamba ni lazima tu iwe boom ndio wasomi wetu wagome na kuandamana? kama kioo cha jamii wasomi wetu wanatakiwa kuwa mifano hai wa kuigwa na jamii ya Kitanzania,hivyo wawe wanagoma na kuandamana na kutoa matamko mbalimbali kwa vitu vinavyo gusa jamii kwa ujumla endepo serikali na taasisi zake zimelega au kushindwa kutekeleza au mf: Constitution review bill, Richmond, Dowas, Loliondo Land issue, Kupanda kwa gharama za maisha to mention but a few. Wasomi wetu badilikeni.

Ulishahamasisha wananchi wangapi waandamane hapo unapoishi au na wewe unawaza mshahara tu.
 
Back
Top Bottom