Wanafunzi vyuo vikuu Rais haja ahidi kuwapunguzia riba ya mkopo wa chuoni badala yake ataongeza idadi ya wanufaika

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Ni wakati wa wanafunzi kuwa wapole, walitegemea riba itapunguzwa imekuwa tofauti badala yake fedha zitaongezwa ili wengi wapate mikopo maana yake ni mtaji unawekezwa ili ukue kwa riba ile ile ya 15% .

ushauri wangu ni wazazi wajitahidi kutafuta pesa wawasomeshe watoto si kwa mikopo maana makato ni makubwa na hawataweza kunufaika na mishahara yao endapo itakuwa midogo badala yake wataifanyia kazi kwa muda mrefu sana.
 
Kikubwa wapate hayo mengine yatajisumbukia mbele ya safari. Kwa riba hiyo hiyo ya 15% watu wakikosa wanalaani mpaka basi.

Kama ulivyosema wazazi wapambane lakini kwakua nami ni mzazi wa tutoto kwasasa natakiwa niwaambie na wazazi wengine tupambane ili wanetu waje kutumia FEDHA ZA NDANI za kwenye familia zetu.
 
Wapunguze afu yale maviete yajazweje mafuta ?

Nikiwa rais kila mtz yoyote anae zaliwa mpka afikishe miaka 18 anakua analipwa laki 2 kila mwezi ila wamiliki viete watakoma
 
15% siyo ribs, ni rate ya kupunguza/marejesho ya mkopo. Kuna 6% ambayo ni adjustment
 
Back
Top Bottom