Wanafunzi Vyuo Vikuu epukeni aibu hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi Vyuo Vikuu epukeni aibu hii

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by TUKUTUKU, Nov 28, 2010.

 1. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Serikali ya shirikisho la wanafunzi wa chuo kikuu Dodoma (UDOSO) imekanusha taarifa iliyotolewa na msemaji wa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Dodoma na waziri wa sheria na katiba wa chuo kikuu cha Dodoma kwa tamko la kukitaka chama cha democrasia na maendeleo (CHADEMA) kiombe radhi kwa kitendo cha kususia hotuba ya rais Kikwete bungeni.Tamko la serikali ya shirikisho lililosainiwa na katibu mkuu wa UDOSO bw.Marwa Joseph linaweka wazi kwa umma kwamba Bw.Thobias Mwasiga sio msemaji wa vyuo vikuu kanda ya Dodoma kama alivyojinadi na pia sio waziri wa katiba na sheria wa chuo kikuu cha Dodoma.Kwa mujibu wa habari hizo Bw.Mwasiga ni waziri katika chuo cha sanaa,lugha na sayansi ya jamii moja kati ya vyuo vinavyounda chuo kikuu cha Dodoma.Kwamba hata chuo chake hakikumtuma kusema alivyosema na kuandikwa na gazeti hili toleo lake la tarehe 20/11/2010 kwa kichwa cha habari “vyuo vikuu Dodoma wataka CHADEMA iombe radhi”.
  Tamko hilo liliongeza kwamba serikali ya wanafunzi ina majukumu yake ya kikatiba na haijihusishi kabisa na masuala ya siasa za vyama hivyo limesikitishwa sana na kitendo cha kiongozi huyu na kusisitiza kwamba taarifa hiyo haikuwa ya kweli kwa vile sio maoni wala mtazamo wa serikali ya wanafunzi.
  Serikali ya wanafunzi haina mpango wa kutoa tamko lolote kuhusiana na kilichotokea bungeni.Aidha ieleweke kwamba kiongozi huyo alitoa tamko lake kwa maoni na mtazamo wake binafsi kwa vile hakutumwa na mamlaka yeyote.(Chanzo cha habari hii:Majira, 28/11/2010,pp.3)

  My take
  Inasikitisha sana kuona wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni kioo cha jamii wanakuwa mara kwa mara wakitoa habari za kushangaza jamii, na jamii kuanza kutilia shaka uwezo wa kuchanganua mambo wa wanafunzi hawa wa vyuo vikuu katika miaka ya hivi karibuni. Hatukatai kuwa wanafunzi hawa wana haki ya kikatiba ya kutoa maoni yao ilimladi tu wasivunje sheria za nchi,lakini ni matumaini ya wanajamii kupata maoni ya mawazo yaliyopevuka kwa kuwa ni wasomi ambao wanapaswa kuwa kioo cha jamii.Nakumbuka wakati sisi tulipokuwa tunasoma chuo vikuu,jamii ilikuwa ikiheshimu sana maoni yetu kwa kuwa tulikuwa makini sana.Lakini katika miaka ya hivi karibuni utasikia wamesema hivi mara vile,wamekuwa kama bendera ambayo daima hufuata upepo na kukosa msimamo thabiti hii ni aibu kubwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.Cha kuziuliza ni kwamba wanafunzi hawa wanatumiwa na wanasiasa?wananjaa ndiyo maana wanatapata sana?au ndiyo maendeleo ya sayansi na teknolojia?au ni uwezo mdogo wa kizazi cha sasa? au ni mmomonyoko wa maadili?Wadodo zangu epukeni aibu hii, tujenge nchi yetu kwa kutoa mawazo yatakayotatua matatizo ya nchi yetu mbalimbali.
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hwa Viongozi wamefanya vema kuweka ukweli peupeeee! Aibu ya mawakala wa ccm walioko vyuoni, badala ya kusoma wanakalia mambo yanayowazidi
  Hongereni UDOSO
   
 3. jyfranca

  jyfranca JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aibu kwa wanafunzi wapumbavu kutumiwa kisiasa, wamefanya wengi wetu tukidharau UDOM
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Watu kwa kujipa ujiko eti ni waziri wa Sheria na Katiba kumbe ni waziri wa Sanaa, CCM watakutumia kama toilet paper na kukuflash, ingekuwa enzi zetu pale mlimani mzee punch angekushughulikia, shame on you Mwasiga .
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Pumba....fu kabisa!!
   
 6. n

  niweze JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nafikiri Uchanga wa Demokrasia Unaonekana Sasa. Demokrasia ni Uhuru wa Kufikiria na Hakuna Sheria Yeyote Iliowazuia Wabunge wa Chadema Kutoka na Kutosikiliza Hotuba ya JK. Kama Hio Sheria Ipo ya Kuzuia Chadema Kutomsikiza JK Bungeni Tunaomba Tuione na Waende Mahakamani. Wananchi Wengi Tunajua JK Kaiba Kura na Hio Kitu Inaitwa Katiba Haina Njia za Kupinga Matokeo Unafikiri Wananchi Wakae Kimya na Kumkubali Mwizi. Tusiwe Naive Hivyo Kwani Hao Wanaompa Jk Heshima ya Uzee na Mweshimiwa Haitoshi. Tusilazimishwe Kukubali Vitendo Visivyo na Haki za Binadamu. Wananchi Inchini Tutaendelea Kuexpress na Kuprotest Haya Matokeo ya Uraisi kwa Muda na Kila Nafasi Tutakayopata. Kama CCM Haitaki Kuonyesha Tume Ilifikia Vipi Katika Kutangaza Hayo Matokeo (details) na Bunge Kuzungumzia Marekebisho ya Hii Katiba ya Chama Kimoja, Hii Miaka Mitano Itakuwa ni Michungu kwa JK. Demokrasia Inazungumzia Haki kwa Kila Mwananchi na Chama Chochote Kile Sio CCM Peke Yao.
  "CCM Wameshajiwekea Kichwani Kuwa Wao Ndio Peke Yao Wanaweza Kuongoza Inchi ya Milioni 43. Kama Walifanikiwa Kubadilisha Inchi Mbona Elimu, Afya na Uchumi ni Mzuri Only Ikulu, Oysterbay, Mikocheni, Mbezi na Ranch Zao?"
   
 7. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Pia alietoa tamko hilo atachukuliwa hatua za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine kwa mujibu wa Tangazo la Udoso lililopo Chuoni kabla ya kutolewa katika gazeti. Pia niwakumbushe wananchi hata ule uvumi uliotangazwa wakati wa kampeni eti udom wamemchangia JK 1 Milioni ya kuvuta form ulikuwa uzushi kama huu huu, mimi nipo udom sikuwahi kuona mchango wowote wa kumchangia JK ukipitishwa, tukashangaa inatangazwa ktk vyombo vya habari, Kipindi hicho haikukanushwa kwani Serikali ya wanafunzi iliyokuwepo wakati huo haikuwa imara sana na ndio maana wakati wa uchaguzi wa chuoni tukaiangusha chini. Fedha zile zilitolewa na kada mmoja wa CCM then ikatangazwa eti wamechanga wanafunzi wa udom. Inasikitisha sana hawa vibaraka wanavyohadaa uma wa Tanzania na kudharaulisha Udom, ila kwa sasa mwisho wao umefika.
   
 8. jyfranca

  jyfranca JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Amesababisha madhara makubwa kwa UDOM, wengi wamewatoa watoto wao UDOM na kuwapeleka vyuo vingine kwa aibu aliyotoa huyo mwanafunzi njaa
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wadogo zangu kuweni makini,jengeni UDOM mpya ambayo itakuwa inaheshimika kwenye jamii,mnaweza kufanya hivyo kwa kutotoa kauli ambazo hazilisaidii taifa hili kuondokana na matatizo mbalimbali!Bado tuna imani na nyinyi!
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mchango wako ni mzuri sana,lakini kwa bahati mbaya hii siyo mada yake!
   
 11. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  matawi ya vyama vya siasa vyuoni ndio source
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kama ni hivyo,hii ni mbaya sana kwa ustawi wa vyuo vikuu vyetu!wanasiasa tuachieni vyuo vikuu vyetu,vifanye yale yanayostahili kufanywa na vyuo vikuu!
   
 13. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfuatilieni huyo jamaa na atiwe mbaroni mara moja
   
 14. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Ikiwezekana achinjwe!
   
 15. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Duh, hii kiboko. Kuna ushahidi wa hili?
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  wakuu kama mgemj ua kijana uyo_THOBIAS mwesiga,wala msingejisumbua kumjibu. Huyu dogo nakumbuka wakati tuko Seminari alijiunga pale na kufukuzwa ndani ya miezi 8 ya upadre,kisa ni kiburi na kuropoka,si lolote. Uyu dogo na kundi lake walipewa nusu saa kuwa wametoweka seminarini yani 'Summary dismissal'. Aliyekuwa gombera,padre medard weyemere alisema "hawa vijana ni sumu kwa taifa,waondoke ndani ya nusu saa wafunge mizigo" yani yule dogo ni kama mwendawazimu pia amelaaniwa. Wakuu mkitaka kumjua vizuri niulize mimi.
   
 17. jyfranca

  jyfranca JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  UDOM tangu lini ikawa na wasomi?
   
 18. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kazi kwao Udm, unajuwa hawa vijana hawajitambui, hawajui ile kauli yao itakuwa na impact gani ktk nafasi ya ajila, mimi naahidi , kama tutatokea kuajili hivi karibuni, kwa kwel4 nikiiona barua ni ya kijana toka Udm, kwa kweli h4yo sitaijali, wala hapati ajila. Na nitaendelea kuene9a 7umu hii kwa waajiri wote.WUDMwaende wakaajiriwe na Ccm
   
 19. r

  rmb JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh kaka kweli unahasira! usiwafanyie hivyo siyo wote wenye mtazamo kama wa huyo kibaraka na naamini kuna vichwa UDOM ila bahati mbaya vimepotea kwa kwenda chuo cha kata
   
 20. upele

  upele JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  atakufa na umasikini wake mjinga njaa itamsabishia afanywe vibaya na watu wenye msimamo
  Conquest-kusoma chuo ni moja ya ubishoo siku hizi na sio kuelimika:embarrassed:
   
Loading...