Wanafunzi UDSM wadaiwa kuuza miili kukidhi mahitaji yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi UDSM wadaiwa kuuza miili kukidhi mahitaji yao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ngoshwe, May 24, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Wednesday, 23 May 2012 | Mwananchi

  KAMATI ya Bunge ya masuala ya Ukimwi imeelezwa kwamba ukosefu wa mikopo na uhaba wa mabweni, unasababisha baadhi ya wanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wauze miili yao na hivyo kuwa katika hatari ya kuambukizwa Ukimwi.

  Hatua hiyo imekuja baada ya kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Rosweeter Kasikila kukutana na Uongozi wa Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam na Mzumbe ili kujionea hali ya Ukimwi katika vyuo hivyo.

  Waziri wa Afya na Chakula wa Serikali ya wanafunzi wa UDSM, Cosmas Nzowa aliiambia kamati hiyo jana jijini Dar es Salaam kwamba , wanafunzi wengi wanaonekana kwenye sehemu za starehe wakijiuza kwa sababu wameshindwa kuendesha maisha yao.

  "Wamefika chuoni wakitokea mikoani wakakuta hakuna mikopo wala mabweni ya kulala na hawana ndugu hapa jijini, unategemea wafanye nini, sasa wengi wanajiuza ili kujikimu, ukitembelea sehemu nyingi za starehe utawakuta," alisema Nzowa.

  Alisema , mchana wanakwenda chuoni lakini usiku wanakuwa na shughuli nyingine za kujiongezea mapato.

  Aliongeza kuwa hata wanafunzi wanaume wanapokosa mikopo na mabweni ya kulala vyuoni huwa katika wakati mgumu na kulazimika kuishi na wanawake waliowazidi umri huko mitaani.

  " Sasa huku hatufahamu kama wanafunzi hawa watakuwa salama katika maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwani ni jambo la kawaida kukuta kijana mdogo wa chuo kikuu akiishi na shugamami mtaani," alisema Nzowa.

  Alisema ili kurekebisha hali hiyo utaratibu wa utoaji wa mikopo hauna budi kubadilishwa ili wanafunzi kabla hawajafika chuoni wawe wanafahamu kama watapata mikopo au la.

  Aliongeza kuwa ,serikali iweke kipaumbele kwa kuongeza idadi ya mabweni inayolingana na wanachuo 15,000 waliopo hivi sasa.

  " Ili kuwasaidia wenzetu ambao wamekosa maeneo ya kuishi na hawana fedha, inabidi tuishi watu wanne kwenye vyumba vidogo na hivyo kusoma katika mazingira magumu," alisema Nzowa anayesomea Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Jamii na Kiswahili.

  Aliwaambia wabunge hao kwamba, wanafunzi hao wako katika hatari ya kupata maambukizo ya virusi vya ukimwi kutokana na mazingira magumu wanayoishi.

  "Tunaiomba kamati hii itutembelee chuoni ili isikilize kilio cha wanafunzi hao,"alisema.

  Mratibu wa Ukimwi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo aliieleza kamati hiyo kwamba, maambukizo katika chuo hicho baada ya kupima mwaka 2011 ni asilimia 2.3.

  Makamu Mwenyekiti wa kamati, Kasikila alitaka uongozi wa chuo hicho kuwasilisha mbele ya kamati hiyo taarifa yenye kueleza matatizo mbalimbali yanayokwamisha mapambano dhidi ya Ukimwi chuoni hapo.

  "Tukipata taarifa yenye changamoto mbalimbali itawasaidia wabunge kutetea Bungeni hasa katika suala zima za upatikanaji wa fedha za shughuli za Ukimwi," alisema Kisikila.

  Akichangia, Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdalla Salim alisema mavazi wanayovaa wanafunzi wa UDSM yanahamasisha ngono.

  " Wanafunzi wa kike katika chuo hiki hawatofautishi mavazi ya disko na ya darasani, wanatembea nusu uchi hebu jifunzeni kwa wenzenu wa Chuo cha Biashara (CBE) wamedhibiti hilo," alisema.Naye Mbunge wa Busega, Dk Titus Kamani alisema
   
 2. M

  Mzalendowetu Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ukosefu wa mikopo + Kuvaa Nusu Uchu + Uhaba wa mabweni + Kuonekana kwenye Sehemu za Starehe = Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI?
   
 3. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,506
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ayaaaaa huyo demu si ndio anasoma sociology 1st yr? ayaaaaa baaaaaaaassssiisiiiiiiiii kwisha habari
   
 4. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Dah! na hii njema inasoma becom third yr tena anaishi paleee dah noma kweli!!
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Halafu tazama shingo ya huyo demu, anaonesha ni mchafu wa kutupa. Shingo imejaa bacteria wa uchafu.
   
 6. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Kweli kukosekana kwa mikopo ina athiri sana maendeleo ya Wanafunzi vyuoni;

  Lakini mimi binafsi sioni kuwa ni sababu ya wao kujiingiza katika vitendo hivi ambavyo ni aibu na pia ni hatari kwa maisha yao.

  Ninapata taabu sana kukubaliana na mawazo yao kwa sababu siyo wanafunzi wote wanaopewa mikopo, kuna wanafunzi ambao wanajitegemea lakini wanasoma!!!!!!

  Ni fundisho gani wanalitoa kwa wadogo zao ambao wanasoma shule za secondary za bweni!!!! kwamba nao wajiuze endapo kama wazazi watachelewesha kuwatumia pesa za matumizi!!!!!

  Ni fundisho gani wanalitoa kwa dada zao ambao wameolewa!!!! endapo ndani hakuna pesa ya matumizi basi atoke nje kutafuta pesa kwa njia hii!!!!

  Ni fundisho gani wanatuonyesha maisha yao yatakavyokuwa hapo baadaye!!!! Wakioa au kuolewa wataweza kweli kuvumilia ndani ya ndoa!!!!


  BADO napata TAABU SANA KUKUBALIANA NAO.

  WANAFUNZI JIREKEBISHENI MAISHA ni MAGUMU NA HIVYO MNAVYOFANYA SIYO SHORTCUT YA maisha. BALI NI SHORTCUT ya KWENDA KABURINI.  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 7. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Vipaumbele kama taifa hatuna!! Chuo kinazidiwa na shule za sekondari kimazingira mazuri ya kusomea! I was frustrated when I joined the university for the first time about 8 years ago from Mwanza, the same problem has existed for more than 2 decades now. Licha ya kutokuwa na hostel za kutosha, hata mazingira basi ya kutolea hiyo elimu nayo yanashindikana kuwa kwenye emergency plan? Walimu hawatoshi, vifaa vya kufundishia, Ofisi za walimu, majengo hayatoshi its really sad to see such an old university being in such condition. Ukiuliza, utaambiwa jibu "suala hilo liko kwenye mipango ya chuo" miaka nenda rudi.
   
 8. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hivi wanajipanga wapi?
  natamani kuwaona.
   
 9. Manager

  Manager JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 532
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hili suala si tu la kisiasa (Chama Tawala) tu, bali ni la kimaadili (wahusika) na kiu-ongozi (UDSM)pia!
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Maisha ya wanachuo kwa kweli yanasikitisha sana, lakini sidhani kama wakiongezewa posho watabadilika.
   
 11. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  ngoshwe hii picha umebandika tu ilishatoka kwenye udaku kitambo kidgo
  tutafutie picha za hao vimodo wa udsm pale hongera, joly pub au K bar kama upo dar
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Unawahitaji??
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  uzushi mtupu...
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Kujiuza kwa ajiri ya kukosa mikopo au kujiuza kwa ajiri ya kupewa mikopo! Halafu shule ikimalizika itakuwa kujiuza ili kupata kazi. Kamati ya bunge itabidi isiishie hapo....
   
 15. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM na wabunge wao ndio wa kulaumiwa kwa dhambi hii na hakika itawatafuna milele.
   
 16. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  E bana si mchezo nasikia mateja pia wapiga debe wanazichanga za kutosha debe then jioni wanaenda mwenge kt mabaa kujipumzisha katika mashine za kisomi za buku mbili mbili, duh jiji ili kweli siliwezi na limepinda
   
 17. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,716
  Likes Received: 1,626
  Trophy Points: 280
  wamejaa karabash, kama shida ni ya kweli mbona wanaulizaga, unataka chakula gani wanasema chips kuku na bia ya Heikein au tropical
   
 18. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  waacheni watoto waonyeshe vipaji vyao ..kwa nini lakini ??
   
 19. King2

  King2 JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kawaida yao hao. Si ndio hawa hawa wana iangamiza nchi hii kwa ufisadi na Kupiga piga Picha na Wahuni kama 50 cent, Beckham, Steven sigel, Boy2men n.k.
   
 20. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  MUNGU tunusuru,maana taifa linawategemea
   
Loading...