Huyu "mwalimu" unayemquote mbona anarukia conclusions bila kuweka ground work yoyote? Relationship ya kusoma kwa Kiingereza na hiyo poverty iko wapi?
Kukaa ofisini kwa Engineer kunasababishwa na kusoma kwa Kiingereza kweli? Tuwe critical na hizi opinion jamani.
Tatizo lipo kwenye mfumo wa elimu kama nilivyosema mwanzo, haijengi creativity na out of the box thinking. Na culture ya kutothamini manual labour, ukikaa ofisini ndo unaonekana wa maana, ukipiga gazi "mbeba box".
Kaamua kulaumu poverty ya Naigeria kwa sababu ya lugha! Rushwa hajaiona? Ufisadi wa viongozi wao hajauona? Matatizo ya udini hajayaona? Vita wanavyopigana na waasi kwenye Delta hajaviona? Lugha is the least of their problems.
Sisemi umasikini hauchangiwi na kitu kimoja.Unachangiwa na vitu vingi.
Kitu ambacho ni common katika udhaifu wetu ni kwamba elimu yetu haitusaidii kudumisha mazingara yetu.Kuna sababu nyingi kwa hii sababu moja ni kwamba walimu hawafundishi vizuri, vilevile mfumo wa elimu ni duni,lakini ukweli ni kwamba lugha inachangia sana.Nimekuuliza angalia nchi zinazotumia lugha za kigeni Afrika zimefika wapi? Jibu kwanza hilo swali.Hizo nchi zimetumia English au French kwa miaka zaidi ya sitini sasa, sisi matumizi ya lugha zetu ni makubwa zaidi lakini manufaa yanaonekana katika amani na mambo mengine.
Ndio tuna uongozi mbaya pamoja na mafisadi umesdaidia kuleta umasikini lakini underlying reason ya kuwa duni katika sayansi na kushindwa uvumbuzi ni kuchukulia elimu kama kitu kigeni lakini tukiifanya ya kwetu na kusoima katika lugha zetu hata watu wa kijijini wataelewa na kufaidika zaidi.Kiingereza sio kitu.Jamaica na Haiti wana lugha zao za kigeni, kiingereza na kifaransa lakini wako wapi?
Mikaka ishirini ijayo tutafanya biashara zaidi ya China na vilevile brazil kuliko uingereza.Je itabidi tubadilishe lugha kwenda kireno au kichina?
Fikirieni zaidi!!