kigugumizi
Member
- Sep 10, 2009
- 11
- 4
wanafunzi wa shahada ya Uzamili - Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Dar wapo mbioni kufungua kesi ya kikatiba katika mahakama kuu dhidi ya Serikali ya Tanzania kwa kuzuia uhuru wa kutoa maoni/kujieleza kwa watanzania kwa kuruhusu watanzania wajieleze kwa lugha ya kiingereza, na dhidi ya sera onezi ya lugha mwigo wa ukoloni.
PIA WANADAI + KUSEMA + KULAANI:
PIA WANADAI + KUSEMA + KULAANI:
- Wanasema kuwa hakuna Nchi duniani iliyoweza kuendelea kwa lugha za watu wengine.
- wanalaani mauaji ya halaiki ya watoto wa kitanzania katika fikra zao kwa kusoma katika mazingira yao kwa lugha za wakoloni/wageni.
- wanalaani viongozi wenye mamlaka makubwa ya kisera kuutukuza ukoloni mkongwe na vipamba ukoloni mkongwe huo ikiwemo lugha, mintaarafu lugha ya kiingereza.
- Wanazidi kusubiri na kukumbushia ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitia mwezi wa saba UDSM kwenye ufunguzi wa TATAKI (IKS) kuwa lugha ya kiswahili itumike kama chombo cha kufundishia.
- Wanaalani sana kuwa ni sawa na watu waliotupwa katika kisiwa ombwe- kifikra, hivyo kukosa utamaduni wao madhubuti na kitambulisho chao sahihi katika uwanja wa Taifa na kimataifa.
- Wanasema - China, Urusi, Uturuki, Sweden, Uingereza, Norway, Ubelgiji wameendelea kwa lugha zao wenyewe.
- Wanakubali umilisi na umahiri wa lugha ya kiingereza kwa watanzania kama lugha yoyote ya ujuzi na utambuzi zaidi, lakini isiwe lugha ya ukuzaji wa fikra pembuzi kwa watanzania.
- wanadai kuwa maamuzi haya yatapelekea kujuta na kusababisha kifungo cha roho kitakachoplekea kuwa omba omba siku zote kama hali hii inavyoongezeka siku hadi siku kwa watanzania.
- Fikra bebuzi hutokana na ujuzi wa lugha mama (fact), uletao maendeleo ya kiuchumi.