Wanafunzi udom waombe radhi waandishi wa habari. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi udom waombe radhi waandishi wa habari.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Baba Tina, Jan 10, 2011.

 1. B

  Baba Tina Senior Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natoa wito kwa uongozi wa serikali ya wanafunzi wa UDOM kutoa tamko la kuomba radhi kwa kitendo cha baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho kumshambulia mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi (kama ilivyo ripotiwa kwenye taarifa ya habari za channel ten na star tv). Japokua naunga mkono asilimia 100% harakati za wanafunzi hao kudai haki zao na kupingana na uongozi dhalimu wa chuo hicho lakini napinga na kulaani kitendo cha wanafunzi hao kumshambulia mwandishi wa gazeti la mwananchi akiwa kazini. Fahamuni kua mwandishi wa habari alikuja kwa lengo la kuripoti matatizo yenu ili umma na serikali uyafahamu. Mnapomshambulia mwandishi wa habari mnamaanisha malalamiko yenu yaishie hapo UDOM au nyerere square mlipokusanyika. Inawezekana hasira na mzuka viliwapanda hivyo mkajikuta mnamshambulia mwandishi huyo bila kufahamu. Narudie kusema UDOSO waombe radhi kwa waandishi wa habari kwa niaba ya wanafunzi wa UDOM kwa kitendo chao kisichokua cha kiungwana. Waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika jamii wakiamua kuwasusia vilio vyenu vyote vitabaki kapuni muulizeni mkuchika na omari mapuri watawaeleza yaliyowakuta.​
   
 2. W

  We can JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bila shaka kama wlifanya hivyo, ni mob psychology probl....
   
Loading...