Wanafunzi udom waombe radhi waandishi wa habari. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi udom waombe radhi waandishi wa habari.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Baba Tina, Jan 10, 2011.

 1. B

  Baba Tina Senior Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natoa wito kwa uongozi wa serikali ya wanafunzi wa UDOM kutoa tamko la kuomba radhi kwa kitendo cha baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho kumshambulia mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi. Japokua naunga mkono asilimia 100% harakati za wanafunzi hao kudai haki zao na kupingana na uongozi dhalimu wa chuo hicho lakini napinga na kulaani kitendo cha wanafunzi hao kumshambulia mwandishi wa gazeti la mwananchi akiwa kazini. Fahamuni kua mwandishi wa habari alikuja kwa lengo la kuripoti matatizo yenu ili umma na serikali uyafahamu. Mnapomshambulia mwandishi wa habari mnamaanisha malalamiko yenu yaishie hapo UDOM au nyerere square mlipokusanyika. Inawezekana hasira na mzuka viliwapanda hivyo mkajikuta mnamshambulia mwandishi huyo bila kufahamu. Narudie kusema UDOSO waombe radhi kwa waandishi wa habari kwa niaba ya wanafunzi wa UDOM kwa kitendo chao kisichokua cha kiungwana. Waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika jamii wakiamua kuwasusia vilio vyenu vyote vitabaki kapuni muulizeni mkuchika na omari mapuri watawaeleza yaliyowakuta.
   
 2. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nani huyo? Habel Chidawali?
  Aah! kupiga waandishi nia aibu!
   
 3. P

  Popompo JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  poleni wanahabari.plse UDOM ombeni msamaha haraka kwa waandishi
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  HIVI HAWA WATOTO NI MANUNDA ENH................sasa waandishi wa habari wakiamua kuwafungia milango yote ya kutangaza vilio vyao itakuaje?
   
 5. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Even a dog don't bite the hand that feeds it!!!!! What's wrong with UDOM students?????!!! How outrageous!!?
   
 6. T

  Teroburu Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BABA TINA kinavunwa kilichopandwa. Waandishi wa habari ni wapenzi wakubwa wa maandamano. Waandishi wa habari hupewa taarifa za maandamano awali kabla hata ya polisi kuombwa kibali na ndio maana wanakuwepo katika maandamano hata pape unashangaa walipataje taarifa za kuwepo kwa maandamano.
  Polisi wanapoonya maandamano yasifanyike kwa ajili ya usalama nyie waandishi wa habari ndio wa KWANZA kuwalaani polisi. Tunakumbuka Jenerali Shimbo alipotoa onyo (kwa niaba ya vyombo vya ulinzi na usalama) kwa wale waliokuwa wanatoa kauli kuwa damu zitamwagika wakati wa uchaguzi ni akina BABA TINA ndio waliolaaani na kumlaani Jenerali Shimbo. Leo hii kuilaani na kuilamu serikali ndio imekuwa kama uhai wa magazeti na waandishi wa habari......

  BABA TINA huwezi kusema unaunga walichokuwa wanadai hao wanafunzi wa UDOM ilhali wakati huo huo unapinga uhalifu walioufanya dhidi ya mwandishi wa habari wakati wa maandamano batili. Wale wote wanaochochea kuwepo kwa maandamano na migomo wanaipeleka Tanzania kubaya. Tayari wamesema kuwa nia ni kuhakikisha kuwa nchi yetu haitawaliki.

  BABA TINA eeeeh nchi yetu inatawalika na tusikubali wale wanaotaka kujenga mazingira ya kuvunjika kwa utawala wa sheria kwa manufaa yao ya kisiasa ya muda mfupi. Kwa matamshi yao, hawa wanafunzi wa UDOM hawana shukran. Wanaimba kuwa Chuo Kikuu sio majengo. Wanaimba kuwa vyoo ni vichafu kwa sababu za maji. Kama hawataki kusoma katika mazingira ya UDOM warudi nyumbani kwenye maji ya bomba yanayotiririka na kwenye vyoo vizuri. Ni Tanzania tu ambapo anayeomba MKOPO wa masomo anadai apewe huo mkopo kwa fujo na maandamano.
   
 7. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wewe ndio msemaji wa serikali?
  Maandamano ni matokeo ya wao kushindwa kazi na si unavyojaribu kusema hapa.
  We unafikiri watu hawana sababu ya kudai haki zao>?
   
 8. T

  The Future. Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashindwa kuelewa, walimshambulia vipi?kwa maneno au walimpiga?kama walimpiga basi wamekosea sana.
   
 9. T

  Teroburu Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAKI wanayodai waliitaja katika CHANNEL 10 TV:

  Kijana mmoja wa ambaye ni ‘Kiongozi wa wanafunzi wa UDOM' alionekana katika Channel TEN TV akieleza sababu za wanafunzi kufanya maandamano batili. Nilisikitika sana kuwa upeo wa wanafunzi wa sasa ni mfinyu kiasi nilichokiona. Kwa kweli kama taifa letu linategemea vijana kama wa UDOM wasio fahamu kuwa HAKI inatafutwa Mahakamani na sio kupitia maandamano batili basi Tanzania itakuwa hatarini hapo baadaye.
  Ni ajabu kuwa wanafunzi wa UDOM wanatumia maandamano batili eti kudai maji yapatikane katika vyoo. Wanafunzi wanasahau kuwa MIKOPO sio HAKI na kama ingekuwa ni haki kila mwanafunzi anayemaliza kidato cha sita angedai hiyo haki.

  Ushauri kwa PROF MLACHA: Wanafunzi wanaogoma warudishwe nyumbani haraka na ili kurudi wapewe masharti stahili. NA Hao wahadhiri wanaogoma pia wachululiwe hatua za kinidhamu kwa kuwa migomo ya wafanyakazi inaongozwa na sheria kupitia TRADE UNIONS. WEngi wa wahadhiri hawa walibembeleza walipooomba kazi. Wakati ni muafaka kuruhusu wahadhiri kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na hata India waje wafanye kazi ili watanzania ambao hawana nidhamu ya kazi waone wenzao wanavyofanya kazi kwa nidhamu na bidii.
   
 10. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,078
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
  terebo nn sijui! 'kwa manufaa yao muda mfupi kisiasa.' kina nani hao,wanafunzi au hao wanaokitawala chuo? maana wanafunzi ni wanafunzi kama tunavyoelewa mimi na ww,ila wanaokiongoza chuo wana vielment vya siasa. kwa hiyo inawezekana hao jamaa ndio manufaa yao. so kwa nini wanafunzi wasiwagomee. sijui kama nimekuelewa vibaya. thank wanajamii wote.
   
 11. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135


  Huna hoja. Hivi unaona ni sawa kabisa kwa wanafunzi kusoma katika mazingira yanayohatarisha afya zao?
  Naamini wangekupa ume VC wa chuo hicho ungewaambia wanywe mkojo wao. Tuone hoja. Baba TINA ametoa hoja ya msingi. UDOM waombe msamaha kwa haraka.
   
 12. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45


  Hivi hawa UDOM si ndo waliandamana kumuunga mkono JK alipochakachua matokeo? Kinachofanya waandamane ni nini hasa? Hayo ni matokeo ya ushabiki wa kumchagua Rais asiye na mapenzi mwema kwa taifa lake.
  Wao waliisifu mvua, sasa inawanyeshea
   
 13. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Nakusikitikia sana. Sina uhakika sana na elimu wala upeo wako wa kuelewa mambo kama unakufaa kuwa humu. Nadhani ndio maana una-statistic ya ajabu kwa kulinganisha muda wako JF na status yako.

  Unataka kuniambia hujui hata mahusiano kati ya taaluma na mazingira yanayozunguka taaluma husika? Hivi wewe unajua madhara ya kutumia vyoo vya muundo na aina ya UDOM (Sina uhakika kama umefika ukaona) pamoja na uwingi wa wanafunzi wa UDOM huku kukiwa hakuna maji? hata vyoo vya shimo vyenyewe vinahitaji maji.

  Tofauti na hili, unadhani haya matatizo ya maji ambayo kwako unayaona madogo (nahisi unakaa magogoni na hujui nini maana ya kukosekana maji) hawa vijana wameanza kuyalalamikia leo? fuatilia historia utaelewa kuwa walianza muda mrefu na serikali ya Mkwere wako imeyapigia kimya kwa sababu wao vyoo vyao vina maji 24/7/365.

  Badala ya kumshauri Mlacha wako atimue wanafunzi, mshauri Mkwere na serikali yake watekeleze madai ya wanafunzi hawa maana fedha zipo (kama unadhani hakuna nenda muulize Ngeleja). Maana kama wanafunzi watakaa kimya, ni kweli hawatafukuzwa lakini watakufa kwa kipindupindu halafu TUTAWAONA WAJINGA ZAIDI kwa wasomi wazima kutumia vyoo vikiwa havina maji
   
 14. kauzu

  kauzu Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  wa jamaa ni MPUMBAVU kwani kila tukijitahidi kukueleza ishu ya udom na ccm ilivyo hauelewi sijui,ok we ulikuwa unashauri nini sasa?
   
 15. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,200
  Likes Received: 942
  Trophy Points: 280
  Nakushukuru kwa kumsaidia mwanaJF mwenzetu ki ukweli jamaa anaonekana yeye mwenyewe haelewi anachosema!!Better education should be provided at better environment physicaly,socially,psychologically and economically!!
   
 16. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  teroburu,
  Huwa wanasema nyumba usiyoikaa huwezi kujua kunguni wake. hebu njoo UDOM afu uishi wiki moja tu. tukupe course work, na tukupe madumu ya MAJI YA UHAI yaliyo matupu ukapange foleni cafteria usubiri foleni ya maaji. tatizo hujui kilichopo udom. na unasikia sikia juu juu tu.

  ngoja nikwambie sasa kwanini mwandishi alipigwa.
  mwandishi wa MWANANCHI alipigwa bahati mbaya, kwani yeye alijificha katikati ya polisi. sa wakati wanafunzi wanapigwa mabomu na polisi,
  ili wao kujitetea walikuwa wanawarushia polisi mawe. Tatizo jamaa alisahau kama amejichanganya na wapambanaji huku wenzake (maaskari ) wamevaa helmenti. na magwanda huku yeye yuko kavukavu. hata hivyo habari za huyo mwandishi kupigwa tumezisikia kwenye magazeti wala hatukujua kama tulimdungunyua. kimsingi tunjiaandaa jinsi ya kuwaomba radhi msijali.
  Ila mbona hawajasema kuhusu mwandishi wa TBCCM TULIVYOTOA NDUKI?
  TULIMTIMUA NYERERE SQUARE kwa sababu zifuatavyo.
  1. tulipogoma tarehe 20/12 walikuwa bias (walitoa taarifa kiupendeleo) waliuhoji uongozi peke yake huku wanachuo wakiwachakachua.
  2. tbc tangu alipotimuliwa (mwandishi wa ukweli)TIDO hatuna imani nao wengi wanafuata matakwa ya ccm so wanapika taarifa.
  3. tarehe 10/ 01 (jana) walichakachua taarifa ya MGOMO WA UDOM NA MAANDAMANO YAKE. ETI walioandamana ni 500 wakati watu miatano ni sawa na BLOCK MOJA LA UDOce. MENGINE 17 waliyapeleka wapi? kumbuka udoce ina wanachuo wasiopungua 7500.
   
 17. S

  Simeon Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  tatizio hawajazoea migomo hawa watoto wa ccm,mwanzoni walidhani wanapewa kipaumbele na ccm,wakajitenga na vyuo vikongwe,sasa mambo yametight,wanadunda hadi wanahabari,haya jitangazeni wenyewe sasa
   
 18. I

  Ilonza Senior Member

  #18
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mmeisha ambiwa udom siyo sisiemu amsikii kilichobaki nikutumia falsafa.mjinga akifundishwa anaelewa lakini mpumbavu hawezi sielewi kwa nini ata amuelewi mkiambiwa. Mgomo utaendelea kama sirikari haita sikiriza mdai yetu. Waandishi wengine hawana taaruma ndo maana wanadundwa awajui effects za kuchakachua taarifa.
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hawajui ethcs za migomo wala maandamano,waandish huwa hawapigw bali husictizwa kuripoti kile kilchojir,bila kupunguza wala kuongeza,ndivyo udsm walivokua+wanavofanya
   
 20. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,477
  Likes Received: 1,214
  Trophy Points: 280
  mwandishi alikuwa upande wa polisi na mawe yalilegwa kwa polisi pole sana mwandishi kwani unafanyia chombo huru ila ingekuwa gazeti la uhuru,mzalendo na magazeti ya rostam ingekuwa shwari kupigwa kwani huwa wanachakachua habari
   
Loading...