Wanafunzi udom waendelea kugubikwa na ksahifa za utovu wa nidhamu na makosa ya jinai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi udom waendelea kugubikwa na ksahifa za utovu wa nidhamu na makosa ya jinai

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by hengo, Dec 26, 2011.

 1. hengo

  hengo JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ikiwa ni takribani siku nne tu kupita baada ya vyombo vya habari kuandika na kutangaza tukio la wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma kitivo cha Elimu kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa kosa la kupatikana na misokoto ya bhangi kinyume cha sheria, wanafunzi wengine wa chuo hicho wakumbwa na kashifa ya ulaghai na utapeli wa fedha taslimu kiasi ambacho bado hakijafahamika kutoka kwa wananchi wakazi wa mkoa wa Dodoma.

  Utapeli huo umefanywa na baadhi ya wanachuo hao wakishilikiana na wanachuo wa chuo cha Mipango Dodoma hasa waishio Furaha hostel kwa kuutangazia na kuuchangisha pesa taslimu umma wa mji wa Dodoma kwa madai kuwa Waambaji maarufu wa kwaya ya SDA kutoka Rwanda wanafika mkoa wa Dodoma na kwamba wengetumbuiza siku ya tarehe 25.12.2011kuanzia mida ya saa moja jioni kwa nyimbo katika ukumbi wa Chimwaga ulioko katika maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma, hivyo baadhi ya wanafunzi waliohusika katika tukio hilo walishiriki kutangaza na kukusanya pesa taslimu kutoka kwa wanchi mbalimbali hasa wapenzi wa nyimbo za injili ambapo walichangishwa Tsh.10,000= kwa jukwaa la kawaida naTsh.15,000/=kwa VP.

  Baada ya kujikusanyia pesa kwa muda usiopungua wiki moja hadi kufikia jana,muda uliotegemewa kwa ajili ya onyesho hilo kuanza ulifika na waaimbaji hao hawakufika na hakuna maelezo yoyote ya msingi yaliyotolewa na wahusika ndipo wananchi waliofika ukumbini katika ukumbi huo walihamaki na kutaka kutembeza vichapo kwa matapeli hao kabla ya askari polisi kuingilia kati na kushauri tukio hilo lifatiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi, hivyo wahusika walitiwa mbaroni kwa tuhuma za Kujipatia pesa mkwa njia ya udanganyifu.

  SOURCE:pERSONAL OBSERVATION
   
 2. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  ndo jana police walikuja chimwaga kuweka mambo sawa.
   
 3. s

  semako Senior Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bumu bado
   
 4. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  inawezekana mpango huo wa hao Ambassador of Christ kufika hapo Dom ulikuwepo, sasa kitendo cha kutofika ni kingine: hivyo ilitakiwa wapenzi wawe na subira kwa vyovyote vile mkwanja ungerudishwa, sasa vurugu za nini??? ni mambo ya kukaa na kujadili.
   
Loading...