Wanafunzi UDOM Wachanga laki 7 kwa wahanga wa Arusha...

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Wanafunzi wa chuo kikuu dodoma(udom) wameamka na leo hii walijitokeza kwa wingi ktk maandamano makubwa yaliyoandaliwa na chadema mkoa wa dodoma na kulaan mauaji ya arusha,sambamba na kuchangia laki 7,ela iliyotolewa na wanafunz wa chuo hicho.wanavyuo wa vyuo vyote vya dodoma walionekana wakilia kulaan mauaji ya arusha.
 
Kumekucha chuo cha kata! Bravo!! Hicho ndicho tunachotaka kusikia. Siyo eti kuchanga fedha za kumchukulia fisadi fomu za kugombea nafasi ya urais.
 
Kumekucha chuo cha kata! Bravo!! Hicho ndicho tunachotaka kusikia. Siyo eti kuchanga fedha za kumchukulia fisadi fomu za kugombea nafasi ya urais.

yule kijana wa UDOM aliyesoma waraka wa kulaani walkout ya wabunge wa chadema yupo wapi...?
 
Nimependa mshikamano wao na tunawaombeni sana kuendelea kuwa chachu ya mabadiliko ambayo kwa sasa ni muhimu sana katika harakati za kulikomboa taifa mikononi mwa mafisadi na wala rushwa ambao wananchi wa tanzania kwakutojua na kwamakosa wamewachagua kuwa viongozi.

Wanachuo kwa pamoja tutalikomboa taifa.
 
Wanafunzi wa chuo kikuu dodoma(udom) wa their edition of meamka na leo hii walijitokeza kwa wingi ktk maandamano makubwa yaliyoandaliwa na chadema mkoa wa dodoma na kulaan mauaji ya arusha,sambamba na kuchangia laki 7,ela iliyotolewa na wanafunz wa chuo hicho.wanavyuo wa vyuo vyote vya dodoma walionekana wakilia kulaan mauaji ya arusha.
Bravo brave students of The University of Dodoma (Hitherto dubbed by some as CCM Cadres University) Students from other Universities and institutes of higher learning should emulate this example to salvage the country from irresponsible leadership. On the other hand CHADEMA must do faster in releasing of a video on what actually transpired in Arusha on that fateful day of January 5th. This will counter the earlier one that was edited and released by the Police Propaganda Unit. Tanzanians have the right to know what actually happened in Arusha and not simple propaganda by CCM and Police (Who unfortunately are openly pro- CCM) that the dead and injured wanted to overrun the police Station. There is abundant evidence that some of the dead and injured were shot far from the said police station like the one in the story narrated in the weekly Raia Mwema newspaper edition number 168 that has so far never been refuted.
 
Vijana mko juu, nimewakubali sanaaaaaaaaaa!!!

Kumbe pale kuna watoto wa wakulima kama sisi ambao pia roho zinawauma nchi yetu inapotafunwa mithili ya mtu anayekula na kipofu hivi?????????

Vijana utaifa mbele kama tai mpaka wabaka uchumi wetu wote wafunge mlango kwa nje.
 
Nadhani sasa wameanza kupata akili ya kutambua mema na mabaya. Mimi nilishawatoa akilini mwangu. Sorry to say this, niliwaona wote kama watoto haramu na kuwasemehe tu kwamba kitanda hakizai haramu! Ila kama wameanza kutubu...tutawasamehe na kuwarudisha kundini!
 
Wanafunzi wa chuo kikuu dodoma(udom) wameamka na leo hii walijitokeza kwa wingi ktk maandamano makubwa yaliyoandaliwa na chadema mkoa wa dodoma na kulaan mauaji ya arusha,sambamba na kuchangia laki 7,ela iliyotolewa na wanafunz wa chuo hicho.wanavyuo wa vyuo vyote vya dodoma walionekana wakilia kulaan mauaji ya arusha.

God bless Tanzania. Saa ya ukombozi imefika!
 
Nilikuwa nimewatoa akilini lakini sasa naona wanaanza kuzaliwa upya.
 
Mimi ninasema asanteni Vijana wenzangu twendeni pamoja tuikomboe nchi mikononi mwa mafisadi wanaotafuna nchi bila hata ya kunawa. Baadaye kitaeleweka tu. Tunisia si wamekimbia wameiacha nchi.
 
Yaani baada ya kuncheleweshewa ela ndo wanaamka.
Na bado yatawakuta mengi sana
 
Mwl jk nyerere alipokuwa akidai uhuru na wenzie alikuwa kijana na aliwatumia sana vijana,.....hivyo shime jamani tusigeuke nyuma dhidi ya mijizi yanayoiibia nchi..watakuja na mbinu nyingi kama vile udini lkn tuwe makini kuyang'amua...
 
Songeni mbele, ni wakati ambao taifa limahitaji mchango wenu wa mawazo, muda nk, kuliko wakati mwingine wowote. Tanzania bila uporaji wa haki za raia na rasilimali zake inawezekana
 
Hongereni sana vijana, lakini je hakukua na coverage ya media mbona taarifa za habari hazisemi chochote kuhusiana na haya maandamano? Au ndo mafisadi wamevitishia?
 
Yaani baada ya kuncheleweshewa ela ndo wanaamka.
Na bado yatawakuta mengi sana

Kila kitu kina mwanzo wake, hata Tunisia kuna mtu alijiunguza kwa moto wa petroli na kujiua ndio mambo ya kumtoa nyoka pangoni yakaanza!
 
Nilisema mwisho tutakuwa pamoja tu hakuna anayekubali serikali yetu inavyotuburuza sasa
 
Kilichofanywa na vijana wenzetu wa UDOM should be replicated to other institutions of higher learning! It is all about critical thinking
 
Mimi langu ni hili, kwamba Cdm waendeleze haya makongamano, mijadala na makusanyiko anuwai katika jamii, ili kuendeleza spirit hii ya UASI WA KIAKILI(mental rebelion) miongoni mwa raia.
Moto huu uende hadi vijijini na mashambani.,Siasa za kutukana ziachwe kwa uvccm na cc yao.
Vijana wa Udom nawapongeza. Usomi ni kuelewa haki, na kuwa mzalendo zaidi.
 
Wanafunzi wa chuo kikuu dodoma(udom) wameamka na leo hii walijitokeza kwa wingi ktk maandamano makubwa yaliyoandaliwa na chadema mkoa wa dodoma na kulaan mauaji ya arusha,sambamba na kuchangia laki 7,ela iliyotolewa na wanafunz wa chuo hicho.wanavyuo wa vyuo vyote vya dodoma walionekana wakilia kulaan mauaji ya arusha.

Hakika, hawa wameungana na vyuo vingine vya elimu ya juu tanzania kutambua ukweli kuwa dira na mwelekeo wa taifa (roadmap) imeshawekwa na CDM kwa ajili ya kulikomboa taifa, kujenga uongozi thabiti, kupinga na kuondoa aina zote za dhuluma, uonevu na ufisadi.
Kwa kitendo chao kuunga mkono nguvu ya umma ktk kuendeleza ukombozi ni mwamko na wito kwa vyuo na taasisi zote za juu kitaifa na wale walio ktk taasisi kama hizo kimataifa kulitambua hili na kuunganisha nguvu na dira ya kitaifa ili kukamilisha ukombozi wa taifa letu hili.

Hongereni sana UDOM, mmeonyesha kuwa mioyoni mmeshakamilika na iliyobakia ni utekelezaji ambao ni mchakato unaoendelea siku kwa siku hadi siku sio nyingi 'umma kujitawala'.
 
Back
Top Bottom