Wanafunzi shule ya msingi kuwalimia waalimu mashamba yao.

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Salam wakuu.

Wakati tunatafakari juu ya ripoti za makinikia na kamati tarajiwa ya makubaliano dhidi ya mtifuano huo, tujikumbushe hili swala la wanafunzi wa shule za msingi kuwalimia waalimu mashamba yao.

Kumekuwa na katabia ka baadhi ya walimu hasa maeneo ya vijijini kuwalimisha watoto wetu mashamba yao kama sehemu ya stadi za kazi. Badala ya kuwalimisha kwenye mashamba ya shule ili wanafunzi nao wanufaike hata kwa uji au chakula cha mchana.

Mm nimelima sana mwanzoni mwa miaka ya 90 lakini nilikuwa nachukia sana. Haiwezekani ukanilimisha mraba kwenye shamba lako halafu mazao hakikomaa mwalimu anayapeleka nyumbani kwake.

Mbaya zaidi mpaka kuwabebea mazao shambani na kupukuchulia kabisa mpaka mikono inaota sugu. Halafu ukiwa shule ukikosea kidogo unatandikwa mboko na mwalimu huyohuyo.

Wasalaamu!
 
kwakweli binafsi pia nimelima sana na iliniuma sana . Ila kwa ulimwengu wa sasa walimu wanatakiwa kubadilika kwakweli sio kwa mateso hayo kws wanafunzi .
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
hebu wacheni kuwawenga walimu

katika mwanafunz kumfanyia kazi, mwanafunz hujitolea kwa upendo wake kumsaidia mwalimu kazi!

kwahiyo mtoa mada unatakaje sasa au ukamsaidie kazi za shamba wewe
 
Kwa waliowaelewa wala sio swala la kuwa na kinyongo nalo maana walimu watapata mazao ila kinachobakia kwa mwanafunzi ni kutoogopa kazi jambo litakalomfaa maisha yake yote yajayo!
WALE WALIOMALIZA LA SABA HUKO USWAHILINI KWENU TANDALE, MBAGALA, KIGOGO ETC. AMBAKO HAKUNA MASHAMBA SI UNAONA FANI WALIYOBAKIA NAYO, PANYA ROAD!
 
Sisi mwaka 2009 nikiwa form 5 pale Kisomachi secondary Kilimanjaro, tuliwahi kulimishwa boonge la shamba tukajua ni la shule, kumbe na walimu humohumo... Nakumbuka tulilalamika tukaita vyombo vya habari wakaja gazeti la mtanzania wapiga picha na kuripot ile habari. Mbona ile tabia iliisha siku hiyohiyo na mpaka sasa hivi ni amani tu.
 
Kwa waliowaelewa wala sio swala la kuwa na kinyongo nalo maana walimu watapata mazao ila kinachobakia kwa mwanafunzi ni kutoogopa kazi jambo litakalomfaa maisha yake yote yajayo!
WALE WALIOMALIZA LA SABA HUKO USWAHILINI KWENU TANDALE, MBAGALA, KIGOGO ETC. AMBAKO HAKUNA MASHAMBA SI UNAONA FANI WALIYOBAKIA NAYO, PANYA ROAD!
Na boda boda.. Ndo fani zao
 
Salam wakuu.

Wakati tunatafakari juu ya ripoti za makinikia na kamati tarajiwa ya makubaliano dhidi ya mtifuano huo, tujikumbushe hili swala la wanafunzi wa shule za msingi kuwalimia waalimu mashamba yao.

Kumekuwa na katabia ka baadhi ya walimu hasa maeneo ya vijijini kuwalimisha watoto wetu mashamba yao kama sehemu ya stadi za kazi. Badala ya kuwalimisha kwenye mashamba ya shule ili wanafunzi nao wanufaike hata kwa uji au chakula cha mchana.

Mm nimelima sana mwanzoni mwa miaka ya 90 lakini nilikuwa nachukia sana. Haiwezekani ukanilimisha mraba kwenye shamba lako halafu mazao hakikomaa mwalimu anayapeleka nyumbani kwake.

Mbaya zaidi mpaka kuwabebea mazao shambani na kupukuchulia kabisa mpaka mikono inaota sugu. Halafu ukiwa shule ukikosea kidogo unatandikwa mboko na mwalimu huyohuyo.

Wasalaamu!
Sasa wewe unachotaka nn? Mimi huwa na walimisha sana sana tena sana.kamwambie unae mwambia .maana walimu wamekukaa mdomoni sana. Hilo eneo linalokutoa povu huyo mwalimu siange kuwa katajilika.
MBONA HUONGELEI KWA WAALIMU WANATUMIA MUDA WA ZIADA KUWAFUNDISHA HAO WATOTO MUDA WAZIADA MFANO UNAKUTA ULISOMA PCB HAPO SHULENI UMELETWA KUFUNDISHA BIOS NA CHEM. LAKINI UNAKUTA HAKUNA MWL WA PHYSICS UNA JITOLEA KUFUNDISHA PHYSICS ILI WASIKOSE SOMO.MBONA HUONGELEI KUWAPA PONGEZI? ACHA ROHO YA WIVU NDUGU HAKUNA WATU WANAO JITOLEA KAMA WALIMU.KAMA UNA LAKO WW SEMA
 
Mpende mwalimu wako naye atakupenda zaidi,mchukie nae atakuchukia zaidi,hivyo ni juu yako kuamua.
 
Acha walimishwe mpk serikali itakapoona thamani ya walim hata ww inaoneka hukusomea ualim km ungesomea pia ungewafanyisha kazi hizi. Hakuna anachopata mwalm zaidi ya kujishughulisha na kilimo kwa kijjn na mjn vbiashara vya hapa na pale. Nguvu kazi ndio wanafunzi maana hela ya kuweka vbarua hana. Walimu limisheni tu
 
Back
Top Bottom