Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,552
Salam wakuu.
Wakati tunatafakari juu ya ripoti za makinikia na kamati tarajiwa ya makubaliano dhidi ya mtifuano huo, tujikumbushe hili swala la wanafunzi wa shule za msingi kuwalimia waalimu mashamba yao.
Kumekuwa na katabia ka baadhi ya walimu hasa maeneo ya vijijini kuwalimisha watoto wetu mashamba yao kama sehemu ya stadi za kazi. Badala ya kuwalimisha kwenye mashamba ya shule ili wanafunzi nao wanufaike hata kwa uji au chakula cha mchana.
Mm nimelima sana mwanzoni mwa miaka ya 90 lakini nilikuwa nachukia sana. Haiwezekani ukanilimisha mraba kwenye shamba lako halafu mazao hakikomaa mwalimu anayapeleka nyumbani kwake.
Mbaya zaidi mpaka kuwabebea mazao shambani na kupukuchulia kabisa mpaka mikono inaota sugu. Halafu ukiwa shule ukikosea kidogo unatandikwa mboko na mwalimu huyohuyo.
Wasalaamu!