Wanafunzi sekondari ya kata waandamana kudai elimu bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi sekondari ya kata waandamana kudai elimu bora

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Luteni, Mar 16, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Mwanagati iliyo Kata ya Kitunda wilayani Ilala jana waliandamana kupinga elimu duni inayotolewa katika shule hiyo ya serikali iliyofunguliwa mwaka 2006, lakini walitulizwa na polisi waliofyatua risasi hewani.

  Hata hivyo, wanafunzi hao hawakuweza kutimiza nia yao ya kuandamana hadi ofisi za Wizara ya Elimu baada ya kuzuiwa na polisi kabla ya kufika Kitunda na hivyo kubadili njia na kwenda ofisi ya kata.

  Shule hiyo ni moja ya sekondari nyingi za kata zilizofunguliwa na serikali katika mpango wa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, wanapata nafasi ya kuendelea na masomo, lakini mpango huo unaonekana kukumbwa na tatizo la ukosefu wa ubora wa elimu inayotolewa kwenye shule hizo.

  Maandano hayo yalianzia shuleni hapo na wakati wakianza kuteremka bonde kwenda eneo la Kitunda Shule (zaidi ya kilometa moja kutoka shuleni kwao), walikutana na magari ya polisi ambao waliwazuia kwa nguvu na kulazimika kufyatua risasi hewani.
  Badala yake polisi hao waliwapeleka kwenye ofisi za kata zilizoko nyuma ya Zahanati ya Kitunda.

  Wakizungumza mbele ya diwani wa Kata ya Kitunda, Johanes Kasejo, wanafunzi hao walidai kuwa tangu wafungue shule Januari mwaka huu, walimu wameingia darasani karibu mara tatu tu, jambo ambalo walisema litasababisha wasipate elimu waliyokusudia.

  Walidai zaidi kuwa walimu wao huwa hawaonekani shuleni mara kwa mara na kwamba hata mkuu wao wa shule hajaonekana kwa karibu miezi miwili sasa, lakini wakadai kuwa alionekana jana baada ya kusikia kuwa wanafunzi wanaandama.

  Pia wanafunzi hao walidai kwamba licha ya kutofundishwa hawajatekelezewa mahitaji yao ya msingi kama sare, vitambulisho, nembo za kwenye sare na nguo za michezo.

  Walifafanua kuwa licha ya kulipia gharama za mahitaji yote, wamepewa sare aina moja badala ya mbili na hawajapewa nguo za michezo na kwamba hadi sasa hawajaelezwa lolote na uongozi wa shule hiyo.

  Wanafunzi hao walidai zaidi kwamba hata ripoti za mitihani ya mwisho mwaka jana hawajapewa mpaka sasa, jambo ambalo walidai linawatia mashaka wazazi hao kuwa hawahudhurii masomo.

  Walilalamika kuwa hali ya elimu shuleni kwao ni duni na ya kusikitisha na kutoa mfano wa matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana ambayo walisema shule yao ilishika mkia, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na serikali kurekebisha hali hiyo.

  Pia walidai kuwa serikali ilitoa Sh500,000 kwa ajili ya kuboresha baadhi ya miundombinu ya shule hiyo, lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika kwa kuwa hata wahusika hawaonekani shuleni.

  Mkuu wa shule hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Fusoo alikiri kwamba elimu wanayotoa ni duni kwa sababu shule nzima ina walimu wanne tu, wastani wa mwalimu mmoja kila kidato.

  Fusoo alisema kama walimu wataongezwa hali ya ufundishaji itakuwa bora zaidi, lakini hakueleza sababu za kutofika kwenye kituo chake cha kazi kama wanafunzi wanavyodai.

  Baada ya kuwasikiliza, Diwani Kasejo aliwaomba wanafunzi hao warudi shule, lakini wakakataa na akalazimika kuwaambia warudi majumbani kwao.

  Lakini wakamgomea tena wakipiga kelele kutaka diwani huyo azungumze mbele yao wote kwa sababu masuala hayo yanawahusu wanafunzi wote.

  Diwani Kasejo alisisitiza kuwataka warudi nyumbani na kwamba atazungumza nao shuleni na ndipo wanafunzi walipolainika na kukubali kuondoka.
  Mkazi mmoja wa Kitunda ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema: “Hata mimi nasikitika kwani mtoto wangu sijui anasoma nini; haandiki chochote na wala haleti taarifa za maendeleo. Nikimuuliza anasema hawasomi na sijui kwa nini shule hiyo ilifunguliwa wakati hakuna walimu."
   
 2. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Yah,naifaham hiyo shule,ilianza kwa mikwara sana,mara wajenge mabweni,mabasi ya shule.matangazo mara kumi kumi kwenye TV,kumbe hakuna chochote.hawa watoto walitakiwa wapate support toka kwa wazazi wao,wakazi wa maeneo yale ya kwa mfipa,wote wangeandamana
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kaaz kwelikweli. Sasa kaa Ilala mambo yako hivo, huko mbali na uso wa dunia hali ikoje?
   
Loading...