Wanafunzi Primary, Secondary waandamana: FFU yawazuia kwnda ikulu!!!

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,393
12,977
FFU yazuia wanafunzi kwenda Ikulu Send to a friend Thursday, 10 March 2011 20:47 0diggsdigg


wanafunzimgomo.jpg
Wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango karikaoo jana wakati wakiandamana kupinga ongezo la nauli za daladala, wakidai kwamba nauli mpya ni kubwa mno hawataimudu wakitaka wapunguziwe. Picha na Robert Ben-Baya

Nora Damian
KIKOSI cha Kutuliza Ghasia cha Jeshi la Polisi (FFU) jana kilitawanya maandamano ya wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam waliokuwa wakielekea Ikulu kupinga ongezeko jipya la nauli za daladala.
Kundi la kwanza la wanafunzi hao lilijikusanya katika Viwanja vya Mnazi Mmoja majira ya mchana na kuanza maandamano hayo yaliyokuwa na lengo la kumfikishia ujumbe Rais Jakaya Kikwete wa kutoridhishwa na ongezeko hilo la nauli. Kundi jingine la wanafunzi lilianzia maandamano hayo katika Uwanja wa Karume.
Mwandishi wa habari hii alipofika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja aliwakuta wanafunzi hao wakijipanga kuanza maandamano hayo huku wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali. Baadhi ya mabango hayo yalisomeka: ‘Kama ni maji ya pilipili, hayawezi kuwa suluhisho la migomo.’
Baadhi ya wanafunzi walisema wameamua kupinga nauli hiyo mpya kwa maandamano ili kuishinikiza serikali iifute wakitaka kurejeshwa kwa ile ya zamani ya Sh100 ili kuwapunguzia mzigo wazazi wao kuwasomesha.
“Sisi wengine kwa siku tunapanda magari matatu hadi kufika shule na hapo bado hujala. Sasa kwa hali hii kweli tutasoma?" Alihoji mmoja wa wanafunzi hao.
Mwanafunzi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Habib Juma alisema nauli ya Sh150 kwa mwanafunzi ni kubwa mno kuimudu akisema kipato cha wazazi wengi ni duni na baadhi yao wanashindwa hata kutoa michango mbalimbali ya shule.
Hata hivyo, jitihada za wanafunzi hao kufikisha ujumbe wao Ikulu ziligonga mwamba baada ya kudhibitiwa na FFU muda mfupi tu baada ya kuingia barabarani.Askari hao waliokuwa na pikipiki walitanda barabarani na kuwatawanya wanafunzi hao na baadaye waliwashikilia wanafunzi wawili wa kiume baada ya wenzao kukimbia. Wanafunzi hao walipakiwa kwenye gari la polisi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Msimbazi.
Nauli hizo mpya za daladala zilizotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), wiki iliyopita zilianza kutumika rasmi jana.Ofisa Mfawidhi wa Sumatra katika Kanda ya Dar es Salaam, Conrad Shio alisema nauli hizo zimegawanywa katika makundi matatu kwamba wanafunzi watatozwa Sh150 kwa safari, kundi la pili ni njia zenye nauli moja ya Sh300 na la tatu ni la njia zenye nauli zaidi ya moja na kwamba nauli hizo zimeongezeka kwa Sh50 katika nauli za awali, katika kila safari moja.
Shio alitoa mfano akisema kwa njia ambayo abiria wake walikuwa wanatozwa nauli ya Sh250 kwa safari, sasa watatozwa Sh300.Alisema katika Kanda ya Mashariki nauli ya juu zaidi itakuwa Sh1,700 kwa safari kati ya Kigamboni na Pembamnazi, eneo ambalo awali nauli yake ilikuwa Sh1,300.

Sumatra imeongeza nauli hizo baada ya kupokea maombi ya wamiliki wa mabasi mwishoni mwa mwaka jana wakilalamikia kupanda kwa gharama za uendeshaji.


Source: Mwananchi.

My take: Wakati JK anazurura huko kutatua matatizo ya wenzetu!! Mwisho wa mwezi asituletee tena hizi hotuba za oh... Chadema..... Oh... wanataka kupindua serikali.......... Wakati wananchi wanafanya wao wenyewe kutokana na ukali wa maisha. Naona sasa msg wanaipata taratibu.
 
Tunasubiri kusikia chadema inachochea Maandamano haya!!maana kila siku CDM...CDM!!safi wanafunzi kwa kuonyesha hisia zenu!!mmewazidi hata wazazi wenu kwa hili maana sisi wazazi wenu huwa tunaishia kunung'unika afu tunakubali matokeo.Hao FFU waliozuia maandamano yenu na kukamata baadhi ya wenzenu nadhani hawana uzazi na hata hiyo std 7 hawakumaliza.:lol:
 
Back
Top Bottom