Wanafunzi MAKUMIRA waambiwe ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi MAKUMIRA waambiwe ukweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, Jan 26, 2011.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa nikifuatilia michango mbalimbali kuhusiana na mgamo wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini MAKUMIRA. Wengi waliochangia wameonekana kuwapongeza wanafunzi hao kuwa ni mashujaa wanaopigania haki zao.

  Taarifa walizotoa wanafunzi hao ni kwamba wanagoma kwa sababu ya kucheleweshewa pesa za mkopo toka bodi ya mikopo. Hata hivyo, kinachoshangaza ni kwamba wanafunzi hao waliamua kufunga barabara ya Moshi-Arusha kwa mawe na kufanya vurugu katika maeneo ya barabara hiyo.

  Mgomo huu uliotokea siku moja baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe kufungua tawi la chama hicho chuoni hapo umefanyika KIHUNI. Madai ya wanafunzi ni ya msingi na ni LAZIMA yashughulikiwe, lakini wanajamii tunawajibika kuwafundisha vijana hawa kuwa ovu moja haliwezi kuhalalisha ovu lingine. Kitendo cha kuzuia watumiaji wa barabara wasiendelee na safari zao si cha kistaarabu na kisijirudie tena. Watumiaji wa barabara nao wangeamua kuonyesha hasira zao kwa wanafunzi hao ni wazi kuwa pangetokea mapigano. Yangekuwa mapigano kati ya wanafunzi na watu ambao hawahusiki vyovyote vile na kucheleweshwa kwa mikopo.
  Nawashukuru waliozuiliwa na wanafunzi hawa kwa kuonyesha moyo wa uvumilivu - mmeonyesha uung'wana wa kitanzania.

  Katika kupigania haki zenu, msikubali kutumika kwa maslahi fulani ya kisiasa ya watu fulani.

  Tuendelee kujenga Taifa letu.
   
 2. sidhani kama unacoongea ni ukweli na sina uhakika kama umefanya synthesis ya kutosha kuhusiana na suala hilo. unavyosema baadhi yake ni sawa lakini conclusion unayo jaribu kuitoa au unavyo jaribu kufanya watu waamini sidhani kama nisahihi. Kwanza hebu fikiria serikari na taasis /asasi zake/watendaji(all its organs)wameambiwa mara ngapi na hawasikii? Kabla ya mapinduzi huko ulaya utawala haukuweza kuwasilikiza watu. Lakini WATU WALIPO CHOKA HAWAKUSITA KUDAI HAKI ZAO KWA KUSHINIKIZA ZAMBO FULANI KWA NGUVU
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo kushinikiza kupewa mkopo ni sahihi kufanyike kwa kuziba barabara kwa mawe? Je wasafiri nao wakijinyakulia haki yao kwa kuwatoa wanafunzi habarabarani kwa nguvu, nini ingekuwa matokeo yake?
  Wanafunzi wana haki ya kupata mkopo na wasafiri wana haki ya kusafiri. Tusifike mahali tukadhani haki ya fulani ni muhimu kuliko haki ya mwingine.
   
 4. M

  Msindima JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Naomba unieleweshe hapo nilipo-highlight na red color,sijakupata vizuri ina maana huo mgomo una uhusiano na ufunguzi wa tawi la CDM hapo chuoni?
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ndio, una uhusiano. hata hivyo swala la kuwa na uhusiano na CHADEMA siyo tatizo. Tatizo ni jinsi mgomo ulivyofanyika.
   
 6. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  unauhusiano gani? bado hujajibu swali
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Je unaweza ukathibitisha vipi huo uhusiano wa kufungua tawi na watu kugomea mabo ya bodi ya mkopo?????????!
   
 8. M

  Msindima JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kivipi? naomba unieleweshe zaidi huo uhisiano.
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kama kawaida ya viongozi wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe alitoa hotuba ya kuwachochea wanafunzi kufanya vurugu ili nchi isitawalike. Hii ndio agenda mpya ya CHADEMA.
  Vinara wa ufunguzi wa tawi hilo la CHADEMA ndio walikuwa vinara wa kuongoza mgomo huo wa wanafunzi.
  Hata hivyo, narudia tena kuwa swala la u-CHADEMA siyo la msingi. Wangeshawishiwa kama walivyoshawishiwa na Mbowe na Lema halafu wakagoma bila kuingilia uhuru wa wasiohusika na mgogoro huo, kama wenzao wa Iringa, sote tungewaunga mkono.
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwenye red hapo, ina maana taarifa za kiintelejensia hazikuwepo ili kudhibiti uhuni ambao ulifanywa na mwenyekiti wa CDM? na sijafahamu unazungumzia uhuni wa namna gani mkuu..
   
 11. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Can you cite precisely sehemu ya hotuba iliyochechea mgomo na kufanya nchi isitawalike? Au na wewe ndo uko kwenye siasa za kwenye dampo?

   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kabla hujajisumbua kutafuta uhusiano huo kwanza tafuta uhusiano kati ya watumiaji wa barabara na kucheleweshwa kwa mikopo.
   
 13. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  HTML:
  
  
  Mimi nadhani hapa Zemarcopolo unachangaya mambo, wanafunzi waliogoma ni mwaka wa kwanza, wanachogomea ni kutopata mikopo yao hadi sasa.

  Tawi la CDM lilifunguliwa Jumapili, wanafunzi wanachama si wa mwaka wa kwanza peke yake. unachotaka tuamini ni kwamba CDM iliwaagiza vijana wagome kitu ambacho si kweli. Madai ya wanafunzi ni ya msingi na wangegoma hata kama CDM isingefungua tawi pale. Labda kinachokusumbua ni kwa nini CDM inakubalika kwenye vyuo vikuu kwa sasa.

  Issue hapa ingekuwa kwa nini walifunga Barabara, lakini si kuhusisha ufunguzi wa tawi la CDM na Mgomo.
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Unataka jibu au unataka kuzogoana? Kama unataka majibu kuwa mstaarabu kwenye jinsi unavyuliza maswali yako.
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Saharavoice,
  hivi kuna mahali katika thread hii mimi nimesema kuwa kuna tatizo kwa wanafunzi kushawishiwa na CHADEAMA? Mimi sina tatizo na hilo, tatizo langu ni jinsi mgomo ulivyofanyika KIHUNI. Soma thread vizuri utaona hilo.

  Correction: Imeripotiwa kuwa waliogoma ni mwaka wa kwanza, lakini kwenye field hali haikuwa hivyo. Na hilo siyo tatizo pia, hata wanafunzi wa mwaka wa tatu au hata raia wema wengeshiriki si tatizo. Tatizo ni kuingilia haki ya wengine katika kudai haki yao.
   
 16. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ina maana huu ni mgomo wa kwanza kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini??,
   
 17. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  walifunga barabara ili wananchi waelewe na wafahamu kilio chao, na hakuna hata abiria mmoja aliyekasirika na kitendo hicho cha wanafunzi, mimi nawaunga mkono kabisa kabisa, maana bila mgomo hakuna haki nchi hii..
   
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sio wa kwanza na kitendo cha vinara hao wa CHADEMA kuongoza mgomo si tatizo. Tatizo ni kuziba barabara, jambo ambalo linaingilia uhuru wa wasiohusika na mgogoro huo.
  Ni jukumu letu kuwafundisha wanafunzi hawa na wafuasi wote wa CHADEMA kwa ujumla kuwa katika kutaka haki zao ziheshimiwe ni wajibu wao kuheshimu haki za wengine. Hiyo ndio essence ya hii thread.
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ZeMarcopolo
  Najua CDM inawanyima usingizi kwani hata UDOM mlisema CDM imeshinikiza.
  ulitaka waandamane kwenda wapi bodi ya mikopo (sijui kama wana ofisi hapa Arusha), je unauhakika gani kama wasingeambiwa wanataka kuteka sehemu husika....
  tangu 11/2010 wako chuo hawajapewa mikopo yao lakini limekuja swala la DOWANS haraka haraka wanataka kulipwa, wakati wao wanachindia maembe na mikate hapo kuna mtu ataonyesha ustaarabu wake au CCM mnataka ustaarabu upi watanzania wauonyeshe?
  hebu onyesheni ustaarabu wa kuwajibika kwanza harafu ndiyo mhoji na ustaarabu wa mnao watawala ingawa ni kwa mabavu...
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ulitaka ufanyikaje?
   
Loading...