Wanafunzi mabibo kufunga barabara: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi mabibo kufunga barabara:

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RanMarwa, Jun 10, 2009.

 1. R

  RanMarwa Member

  #1
  Jun 10, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawapongeza sana wanafunzi wa mlimani na waishio mabibo kwa kuamua kutumia nguvu zao wenyewe ili wasiendelee kugongwa kama kuku hapo barabarani.

  Unajua hapo njia panda ya kwenda hostel wanafunzi wengi sana wamegongwa na kuuawa tangu hostel zilipojengwa.

  Nakumbuka ni ule uongozi wa julius mtatiro uliofanya matuta zawekwe kwa mara ya kwanza katika historia ya barabara ya mandela.

  Nakumbuka siku hiyo niliona kwenye taarifa ya habari ya ITV , MTATIRO akisisitiza kwamba kama serikali haiweki matuta ndani ya siku tatu yeye mwenyewe angeongoza wanafunzi wengine kulala barabarani na akasisitiza serikali ichague moja,kuweka matuta ndani ya siku tatu au kuandaa askari wengi wenye silaha wakapambane na wanafunzi wengi wasio na silaha lakini watakaokuwa wakitetea maisha yao na ya wenzao bila kuwaogopa polisi ambao kwa mujibu wa mtatiro polisi ni wahanga wa vifo hivyo vya wanafunzi kwani wanaogongwa pia ni ndugu zao.
  Baada ya siku mbili nakumbuka matuta yalijengwa na watu wengi sana nikiwamo mimi tulimpigia simu mtatiro kumpongeza na hata siku moja nilienda kutembelea mlimani na nikakuta makala nyingi za kumsifu mtatiro eti ana EXTRA POWER.

  Tangu mtatiro ahitimu nadhani ni mwaka umetimia,na ndio serikali ikaona itoe tu matuta na tayari kuna mwanafunzi amegongwa tena na kufariki kwani hakuna tena mtu anayeitisha serikali na anayeweza kuwatetea wanafunzi nchi nzima kwa sasa tangu mtatiro amalize,kama mtu huyo yupo basi bado yuko sekondari.

  Wanafunzi wamefanya juhudi nzuri hata kama hawana viongozi imara kama enzi za mtatiro.Keep it up udsm.

  Yeyote mwenye namba ya mtatiro anifowadie nasikia amejiunga na chama fulani cha siasa,nijulishwe ni chama kipi,nisaidieni.
  ranmarwa /cologne-germany.
   
Loading...