Wanafunzi kumi bora kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha nne 2019

Mkuu, mtu kuwa mwanafunzi bora ni jambo kubwa sana na la kujivunia, hasa kibinafsi!

Lakini kibongobongo halina maana, kwa sababu woote hao wataenda A level hizi hizi za kwetu, na baadaye vyuo hivihivi, baadaye wanakuwa watu tu wa kawaida, ambao hata kwenye jamii wanaweza wasitusaidie sana kutatua changamoto zetu.

Kwa mfano, kuna viongozi fulani wa serikali ambao inasemekana walikuwa vichwa sana, lakini mbona ndio wanaongoza kwa kutoa 'boko'!?

Hivyo, kibongobongo, kuwa miongoni mwa wanafunzi bora, ni jambo la kujivunia muhusika, ila jamii tusidhani kuwa anaweza kuwa msaada sana!!


Sent using Jamii Forums mobile app
Endelea kujidanganya.
 
Hivi mtoto anayepata Div I ya 7 shule ya kata tunamuweka kundi gani

Tujaribu kuapreciate hata hawa watoto wa shule za kata wanaofanya vizuri
Kuna shule inaitwa Igaganulwa ipo Simiyu shule ya kata dogo kapata DIV I ya point 7
 
Bravoo madogo wa kutoka seminary mmetuwakilisha vyema kaka zenu , ahahahah dogo denis , dogo erick hongereni sana .
 
Wakuu napenda kuwaletea majina ya Wanafunzi kumi bora kidato cha nne 2019 kitaifa.

1. Joan Ritte (St Francis Girls Mbeya)
2. Denis Kinyange (Nyengezi Seminary Mwanza)
3. Erick Mutasingwa (Sengerema Seminary Mwanza)
4. Rosalia Mwidege (St Francis Girls Mbeya)
5. Domina Wamara (St Francis Girl Mbeya)
6. Mvano Cobangoh (Feza Boy’s- Dar es Salaam)
7. Agatha Mlelwa (St Francis Girls Mbeya)
8. Sarah Kaduma (St Francis Girls Mbeya
9. Shammah Kiunsi (St Francis Girls Mbeya)
10. Luck Magashi (Huruma Girls Dodoma)

=====
Tutaishitaki NECTA kwa kupendelea hayo majina. Ha ha ha ha . Anzia shule mpaka majina yenyewe 9. Hilo moja la kumi sijajua jina lenyewe liko upande upi. Pole sasa mama kipenzi Ndalichako maana walikupiga mawe sana kuwa unapendeelea wa kwako. Sasa ulitoka mbona mambo ni yale yale na kuzidi?

Wakubwa elimu ni kusoma kwa bidii ndiyo mpango mzima. Hivyo mambo ya kulialia tuache. Hivyo vichwa vinasoma na shule zina mikakati ya kusomesha na kufaulisha.
 
Back
Top Bottom