Wanafunzi kufaulu mwakani ni asilimia ndogo sana kutokana na

Jul 29, 2012
52
4
Jamani nina hisi wanafunzi wengi watafeli sana mwakani. Kwa kuanzia kudodosoa nianze na hawa wa kidato cha pili wengi hawana sifa za kuwepo katika kidato hicho kwasababu zifuatazo, wengi hawana uwezo wa kusoma au kuelewa lugha ya kiingereza. Wengi wao hawawezi kuumba herufi yani hata neno likaeleweka. Pia Mihula ya mwaka huu Imetawaliwa na likizo za hapa na pale, shughuli za sensa kupelekea walimu wengi kutomaliza sylabus kwa muda muafaka. Kwa asilimia kubwa wanafunzi hawaja pewa elimu ya kutosha kujibu mitihan yao kutokana na Mgomo wa walimu ulioanza toka kipindi chini kwa chini. Kunamapungufu nimeyaona katika baadhi ya shule, utayar wa waalimu kutoa material kwa wanafunzi umekuwa dhaifu kutokana na haliduni ya hawa walimu wetu kutothaminiwa na utayari wa wanafunzi wenyewe katika usomaji ambapo wengi wamebweteka sana na kukata tamaa. Serikali inabidi itazame upya suala la kuboresha vitendea kazi mashuleni. Kuna wakati serikali itakosa wasomi wenye sifa kwa kufumbia macho mkanganyiko huu. Naishahuri serikali ifanye mtazamio upya wa Tanzania yetu kwa miaka ya sasa hadi mingineyo kwa kipindi cha miaka 50 baadae, kwamba walifanyalo sasa kwa manufaa ya wakati ujao kwa ajili ya kumkomboa mwalimu na kuikomboa nchi katika misingi ya elimu kama nyenzo kuu ya taifa. Na ikilitafakari hili jambo kisiasa kwa miaka mitano mitano ya uongozi hakutakuwa na maendeleo katika suala la elimu maana itabaki ni MADESA tu, bali kutakuwa na uozo ndani ya taifa kwa watu wasioelewa kuchambua na kupembua mikataba, ufisadi wa fedha za walipa kodi na uchukuaji wa rushwa na kuchakachua baadhi ya masuala. Na kupata msiba na majanga ya kuhujumu uchumi na mengineyo. Tujipange jamani!
 
Well said...lakini kikubwa sana katika hili ni kwamba serikali unayoitaka ichukue hatua siyo sikivu ki hivyo japo wanajinasibu kila siku kuwa serikali ya ccm ni sikivu...me sijauona usikivu huo. Viongozi wamekuwa wabinafsi na wanaojali familia zao tu. Kila mmoja yupo hapo alipo kwa maslahi yake binafsi na kwa maslahi ya chama chake. Hasa hawa ccm, wamekuwa kiccm sana. Hakuna UZALENDO TENA. Ndiyo maana mimi (Mwalimu) tangu nimalize chuo, sina muda wa kukaa na wanafunzi na kuwasaidia zaidi ya muda ninaokuwa darasani. Nimegundua umaskini ni wangu na njia ya kujikomboa na hali hii ni kufanya kazi kwa bidii. Mshahara hautoshi, hakuna fedha nyingine yoyote nje ya mshahara, unafanya nini kama siyo kutafuta alternative out of teaching? Nimekuwa MJASILIAMALI. Kama kuna siku nimekaa shule hadi saa sita, sina kumbukumbu hiyo. Kwa hiyo ni kweli, mwakani tunajitahidi kutoa zero nyingi zaidi za kidato cha nne ili serikali ijue kuwa hali ni mbaya, kwa sababu ya mgomo, lakini maisha magumu na hatuwezi kukaa shule tukicheka na wanafunzi huku tunakufa maskini wao wanalipana 200000 huko bungeni. USHENZI TU. NANI AKAE SHULENI? SIFANYI KAZI HIYO.
 
100% matokeo ya mwaka huu form two na four lazima yashuke,mbaya zaidi wanafunzi wenyewe wanahisi kuwa watu wenye bahati sana mwaka wao wa masomo kuisha kwa mugongano wa matukio kama migomo,sensa na mengine mengi,tanzania kiukweli tunatakiwa na mtazamo chanya juu ya swala zima la elimu.
 
Back
Top Bottom