Wanafunzi IFM wanatarajiwa kuandamana leo

Mchapaji

Member
Mar 22, 2010
26
1

4275342.jpg

Thursday, March 25, 2010 10:52 AM
IMEDAIWA kuwa zaidi ya wanafunzi 300 wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), leo wamepanga kuandamana kutoka chuoni hapo hadi Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kufikisha kilio chao cha kupandishiwa ada.Hatua hiyo imefikiwa na wanafunzi hao baada ya bodi hiyo kuweka bayana kuwa haitaweza kuwalipia wanafunzi nyongeza ya ada iliyotangazwa na IFM

Moja ya malengo ya kufanya maandamano hayo hadi Bodi ya mikopo ni kuiomba bodi hiyo kuwasaidia kulipa ada hiyo ya nyongeza iliyoongezwa na chuo hicho.

MBali na hilo pia wanatarajia kumuona Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ili kumueleza kuhusu ongezeko la ada chuoni hapo, ambalo limezua utataw mkubwa kati ya uongozi wa chuo na wanafunzi
 
shida ya chuo hiki , kinawanafunzi waoga saana, wanaanzaga vizuri harakati zao za kudai maslahi yao na haki zao zingine.
kweli wanaanza vyema pale freedom square......mpambano ukinoga utawaona watoto wawakubwa wakichomoka na kujitenga na walalahoi......wanahoja ila hawana umoja.
 
Back
Top Bottom