Wanafunzi IFM wadakwa na mirungi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
POLISI wamewatia mbaroni wanafunzi wawili wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam, kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa na mabunda saba ya mirungi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga amesema, watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 11:30 jioni katika eneo la Coco Beach, Oysterbay.

Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Mohamed Abdullah (27) na Abdulatif Jabir (27).

Amesema, wanafunzi hao ni wakazi wa Bungoni Ilala, na kwamba watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Wakati huohuo, mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Chanika, Amani Mwera (12), amekufa baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara.

Mtoto huyo aligongwa juzi saa 12:40 jioni katika barabara ya Mvuti – Chanika, Ilala.

Gari lililomgonga lina namba za usajili T775 BDF Nissan Caravan, lilikuwa likiendeshwa na Shaban Juma (22), mkazi wa Buguruni,alikuwa anatoka Chanika kwenda Mvuti.

Polisi wamemkamata dereva huyo, maiti ya mtoto imehifadhiwa katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam.
 
Bora hicho chuo kihamishiwe hukohuko msata,
kikikaa mjini ni hatari tupu, vibitozi na visista du vya geti kali vinazibukia na kuharibikia hapo.
Ifm ni chuo cha kuharibu vijana wasio na akili.
 
Back
Top Bottom