Wanafunzi Hanang wasoma kwa nadharia, shule nyingi za sekondari hazina maabara

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Wilaya ya Hanang’i iliyopo Kaskazini mwa Tanzania bado inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya maabara licha ya nguvu kubwa ya wananchi iliyotumika kujenga majengo ya maabara katika shule za sekondari.

Kulingana na Takwimu za Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) zinaonyesha kuwa Wilaya ya Hanang’i ina jumla ya shule za sekondari 33 zenye mahitaji ya vyumba vya maabara 99 kwa ajili ya masomo ya sayansi. Ujenzi wa maabara katika shule 11 kati ya 33 umekamilika .

Shule 10 zilizokamilisha ujenzi wa vyumba vya maabara kabla ya mwaka 2017 zilipewa vifaa vya maabara huku shule moja ikikosa kwa sababu ujenzi wake kutokamilika kwa wakati. Changamoto bado ipo kwa shule 22 zilizobaki ambazo hazina maabara na vifaa kabisa na wanafunzi wa masomo ya sayansi wanajifunza kwa nadharia.

Takwimu za TAMISEMI zinaonyesha kuwa Hanang’i imepokea milioni 253.9 kwa ajili ya ujenzi na ununuzi wa vifaa vya maabara tangu mwaka 2015. Licha ya kupeleka fedha hizo bado hazikidhi mahitaji yote ya wilaya hiyo ambapo shule 22 bado hazina maabara na vifaa, lakini fedha zinazotengwa sio zote zinafika kama zilivyokusudiwa kutokana urasimu uliopo katika mamlaka husika.

Zaidi, soma hapa => Wanafunzi Hanang’i wasoma kwa nadharia, Bajeti ndogo yakwamisha ununuzi wa vifaa vya maabara | FikraPevu
 
Hilo ni tatizo la nchi nzima ila wahusika utasikia wanajisifu jukwaani "tumejenga mashule"
Wanafunzi kadhaa wamefaulu masomo ya sayansi

Hizo shule zingekua nzuri basi tungeona watoto wal wakisoma humo.
 
Back
Top Bottom