Wanafunzi Dar wafanya maandamano kupinga ongezeko la nauli. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi Dar wafanya maandamano kupinga ongezeko la nauli.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jakubumba, Mar 11, 2011.

 1. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  My note! mimi hii nimeipenda sana,kama hawa watoto wameamua kuandamana itakuwa ni njia nzuri sana ya kuwafungua macho wazazi mbumbumbu na kuhamasisha vijana wote wa Tanzania kudai na kutetea haki zao.
  Source, mwananchi

  FFU yazuia wanafunzi kwenda Ikulu Send to a friend
  KIKOSI cha Kutuliza Ghasia cha Jeshi la Polisi (FFU) jana kilitawanya maandamano ya wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam waliokuwa wakielekea Ikulu kupinga ongezeko jipya la nauli za daladala.

  Kundi la kwanza la wanafunzi hao lilijikusanya katika Viwanja vya Mnazi Mmoja majira ya mchana na kuanza maandamano hayo yaliyokuwa na lengo la kumfikishia ujumbe Rais Jakaya Kikwete wa kutoridhishwa na ongezeko hilo la nauli. Kundi jingine la wanafunzi lilianzia maandamano hayo katika Uwanja wa Karume.
  Mwandishi wa habari hii alipofika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja aliwakuta wanafunzi hao wakijipanga kuanza maandamano hayo huku wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali. Baadhi ya mabango hayo yalisomeka: ‘Kama ni maji ya pilipili, hayawezi kuwa suluhisho la migomo.’
  Baadhi ya wanafunzi walisema wameamua kupinga nauli hiyo mpya kwa maandamano ili kuishinikiza serikali iifute wakitaka kurejeshwa kwa ile ya zamani ya Sh100 ili kuwapunguzia mzigo wazazi wao kuwasomesha.
  “Sisi wengine kwa siku tunapanda magari matatu hadi kufika shule na hapo bado hujala. Sasa kwa hali hii kweli tutasoma?" Alihoji mmoja wa wanafunzi hao.
  Mwanafunzi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Habib Juma alisema nauli ya Sh150 kwa mwanafunzi ni kubwa mno kuimudu akisema kipato cha wazazi wengi ni duni na baadhi yao wanashindwa hata kutoa michango mbalimbali ya shule.
  Hata hivyo, jitihada za wanafunzi hao kufikisha ujumbe wao Ikulu ziligonga mwamba baada ya kudhibitiwa na FFU muda mfupi tu baada ya kuingia barabarani.Askari hao waliokuwa na pikipiki walitanda barabarani na kuwatawanya wanafunzi hao na baadaye waliwashikilia wanafunzi wawili wa kiume baada ya wenzao kukimbia. Wanafunzi hao walipakiwa kwenye gari la polisi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Msimbazi.
  Nauli hizo mpya za daladala zilizotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), wiki iliyopita zilianza kutumika rasmi jana.Ofisa Mfawidhi wa Sumatra katika Kanda ya Dar es Salaam, Conrad Shio alisema nauli hizo zimegawanywa katika makundi matatu kwamba wanafunzi watatozwa Sh150 kwa safari, kundi la pili ni njia zenye nauli moja ya Sh300 na la tatu ni la njia zenye nauli zaidi ya moja na kwamba nauli hizo zimeongezeka kwa Sh50 katika nauli za awali, katika kila safari moja.
  Shio alitoa mfano akisema kwa njia ambayo abiria wake walikuwa wanatozwa nauli ya Sh250 kwa safari, sasa watatozwa Sh300.Alisema katika Kanda ya Mashariki nauli ya juu zaidi itakuwa Sh1,700 kwa safari kati ya Kigamboni na Pembamnazi, eneo ambalo awali nauli yake ilikuwa Sh1,300.

  Sumatra imeongeza nauli hizo baada ya kupokea maombi ya wamiliki wa mabasi mwishoni mwa mwaka jana wakilalamikia kupanda kwa gharama za uendeshaji.
   
 2. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nchi ishauzwa hii!!
   
 3. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa tufanyaje. wazaziwenu na nyie wenye si mmewapenda CCm kama vipi tukutane Mnazimmoja kama mnauchugu tumtoe Mkwere na chama chake ndiyo sorce ya matatizo yote. AYO NDIYO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA
   
 4. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mie mnazi mmoja siji!! sihitaji kupigwa virungu kwa sasa, wakati bado.
   
 5. Tisha-TOTO

  Tisha-TOTO JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 1,173
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  JK atatoa speech tena ya kulaani haya maandamano ya "uchochezi" yanayofanywa na hawa watoto. Atasema wanataka kuvunja amani yetu!
   
 6. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisuy kama unaogopa virunguje ukiona midege si utachimba shimo? basi kubali kuburuzwa wengine wale kilaini( shika pembe wengine wakamue maziwa). Mm sitakubali kamwe mpaka kieleweke
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kila kukicha kunaibuka jambo jipya, nchi hii sidhani kama tutafika 2015!!
   
 8. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Msikilize sokwe,au mamba jioni,watasema yanavunja amani,na YAMETUMWA NA CHADEMA!
   
Loading...