Wanafunzi Chuo Kikuu cha Ardhi wajawa hofu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,849
Wanafunzi Chuo Kikuu cha Ardhi wajawa hofu

2008-07-28 16:02:48
Na Job Ndomba,Jijini

Wanafunzi zaidi ya 150 wa Chuo Kikuu cha Ardhi wamejawa hofu ya kukosa sifa za kuendelea na masomo baada ya matokeo yao kushikiliwa kutokana na kiasi cha pesa wanachodaiwa na chuo.

Imeelezwa kuwa hofu hiyo ya kupoteza sifa za kuendelea na masomo chuoni hapo, inazidishwa na ukweli kuwa baadhi ya wanafunzi hao ambao matokeo yao yameshikiliwa hadi sasa, wanadaiwa hadi Sh. 800,000, ambazo kutokana na hali zao kiuchumi, ni wazi kwamba hawataweza kuzilipa ili kupata matokeo yao hayo.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho cha Ardhi, Bw. Anthony Massawe, amesema hali bado si shwari chuoni hapo, kwani bado wanafunzi wengi wanahofia kukosa masomo.

Bw. Massawe amesema ni wanafunzi wachache tu ambao wanatarajiwa kupewa matokeo yao na wengine wengi wanahofiwa kukosa, licha ya kutakiwa kukata rufaa kwavile wanatakiwa kurudi vijijini walikozaliwa ili kupata taarifa zaidi kutoka kwa viongozi wa vijiji.

Amesema hadi sasa, ni wanafunzi 84 tu ambao wameshapewa matokeo yao na wengine zaidi ya 150 wameanza kukata rufaa baada ya kutakiwa kufanya hivyo kwakuwa tayari Bodi ilishaamua kutowaonesha matokeo yao.

Aidha, Bw. Massawe amesema dalili zinaonesha kuwa watakoathirika zaidi ni wale wa mwaka wa kwanza na wa pili.

Taarifa nyingine zinaeleza kuwa migogoro kama hiyo, pia imevikumba vyuo vingine kadhaa na hivyo Umoja wa Serikali za Vyuo Vikuu, TAHLISO kuamua kutoa tamko lao rasmi, hasa kuhusiana na baadhi ya vigezo vinavyotumiwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini ambavyo vimetakiwa viondolewe, kwani vinawakosesha mikopo wanafunzi wengi wanaostahili kupata mikopo hiyo.

``Mpango uliopo ni kuishinikiza Serikali kutoa mikopo kwa asilimia 100 kwa wanafunzi wote wanaochaguliwa katika vyuo vya elimu ya Juu,`` imeelezwa na chanzo kimoja toka TAHLISO.

SOURCE: Alasiri
 
Naam masharti ya IMF na WB hayo ambayo hayana maslahi yoyote kwa nchi yetu lakini viongozi vichwa maji wakiambiwa na wazungu wa kutoka IMF na WB wafanye chochote kile basi nao wanakifanya bila kuangalia athari yake kwa nchi. Sasa watoto wa mafisadi wanapata elimu poa nje na wale wa walala hoi hawapewi mikopo na matokeo yake watakosa elimu na hivyo kuwa na uwezo mdogo wa kufanya lolote la maana katika maisha yao na Tanzania kwa ujumla.
 
Mkapa huyo
 
wanafunzi wanalia na mikopo wakati juzi hapa tumeambiwa wanafunzi 10,000 wamepewa mikopo mara mbili kutoka bodi ya mikopo.

huu uzembe wa aina hii utamalizika lini? .....
mtu anatakiwa alipe laki nane kwa mwaka.....atazitoa wapi na yeye anatoka kijijini ambako mzee wake chakula hana sawa sawa?

dhuluma tanzania sijui itaisha lini kwa kweli
 
Wanafunzi Chuo Kikuu cha Ardhi wajawa hofu

2008-07-28 16:02:48
Na Job Ndomba,Jijini

Wanafunzi zaidi ya 150 wa Chuo Kikuu cha Ardhi wamejawa hofu ya kukosa sifa za kuendelea na masomo baada ya matokeo yao kushikiliwa kutokana na kiasi cha pesa wanachodaiwa na chuo.

Imeelezwa kuwa hofu hiyo ya kupoteza sifa za kuendelea na masomo chuoni hapo, inazidishwa na ukweli kuwa baadhi ya wanafunzi hao ambao matokeo yao yameshikiliwa hadi sasa, wanadaiwa hadi Sh. 800,000, ambazo kutokana na hali zao kiuchumi, ni wazi kwamba hawataweza kuzilipa ili kupata matokeo yao hayo.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho cha Ardhi, Bw. Anthony Massawe, amesema hali bado si shwari chuoni hapo, kwani bado wanafunzi wengi wanahofia kukosa masomo.

Bw. Massawe amesema ni wanafunzi wachache tu ambao wanatarajiwa kupewa matokeo yao na wengine wengi wanahofiwa kukosa, licha ya kutakiwa kukata rufaa kwavile wanatakiwa kurudi vijijini walikozaliwa ili kupata taarifa zaidi kutoka kwa viongozi wa vijiji.

Amesema hadi sasa, ni wanafunzi 84 tu ambao wameshapewa matokeo yao na wengine zaidi ya 150 wameanza kukata rufaa baada ya kutakiwa kufanya hivyo kwakuwa tayari Bodi ilishaamua kutowaonesha matokeo yao.

Aidha, Bw. Massawe amesema dalili zinaonesha kuwa watakoathirika zaidi ni wale wa mwaka wa kwanza na wa pili.

Taarifa nyingine zinaeleza kuwa migogoro kama hiyo, pia imevikumba vyuo vingine kadhaa na hivyo Umoja wa Serikali za Vyuo Vikuu, TAHLISO kuamua kutoa tamko lao rasmi, hasa kuhusiana na baadhi ya vigezo vinavyotumiwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini ambavyo vimetakiwa viondolewe, kwani vinawakosesha mikopo wanafunzi wengi wanaostahili kupata mikopo hiyo.

Mpango uliopo ni kuishinikiza Serikali kutoa mikopo kwa asilimia 100 kwa wanafunzi wote wanaochaguliwa katika vyuo vya elimu ya Juu, imeelezwa na chanzo kimoja toka TAHLISO.

SOURCE: Alasiri
Lipeni Ada
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom