Wanafunzi Chuo cha Mahakama watiwa mbaroni na vyeti feki

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
10th February 2010
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta)
Wanafunzi tisa wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) wanashikiliwa na Polisi wilayani Lushoto mkoani Tanga, baada ya kubainika waliwasilisha vyeti vya kughushi wakati walipojiunga na chuo hicho Septemba, mwaka jana.
Hatua ya kukamatwa kwa wanachuo hao inatokana na utaratibu ulioanzishwa na Uongozi wa chuo wa kuvifikisha vyeti vya wanafunzi kwenye Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kwa ajili ya uhakiki kufuatia kuwepo kwa tatizo sugu la kughushi vyeti kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Ntemi Kilekamajenga, amesema jumla ya wanachuo 413 walijiunga na chuo hicho Septemba mwaka jana ambapo 248 walikuwa wa kozi ya Stashahada ya Sheria na 165 walikuwa wa ngazi ya Cheti na kueleza kuwa kati ya hao tisa ndio waliothibitishwa na Necta kuwa walighushi vyeti.
Kilekamajenga aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Faida Mulunga, Esther Said, Sofia Mjembe, Gideon Mgombela, Mohamed Said, Bastian Risso, Joyce Joseph, Ally Mganga na Victoria Shomari.
Alisema miongoni mwa wanachuo hao wanaotuhumiwa kughushi vyeti wengine walidanganya matokeo ya ufaulu, wengine walitaja vituo vya mitihani ambaavyo kwa wakati huo havikuwepo sambamba na kubadili majina kwa kutumia majina yasiyo ya kwao kwenye vyeti hivyo.
Kabla ya kukamatwa kwa wanachuo hao, Afisa Upelelezi wa Wilaya ya Lushoto, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Madafu Abdallah, aliwafeleza watuhumiwa hao sababu za kukamatwa kwao.
CHANZO: NIPASHE
 
Sasa kama mpaka wakili/hakimu mtarajiwa anadiriki kufoji cheti mnategemea nini huko tuendako?
 
Back
Top Bottom