Wanafunzi Bungu Sekondari walia Kutofanya Mtihani wa Kidato cha Pili

Mpamo

Member
Dec 8, 2012
94
0
Ili kudhibiti udanganyifu katika usajili wa wanafunzi shuleni, serikali kupitia Wizara ya elimu na Mafunzo ya Ufundi imewazuia wanafunzi walioko Kidato cha Pili ambao hawana TSM 9 fomu kutofanya Mtihani wa Kidato cha pili. Hatua hiyo imelallamikiwa sana na wazazi wa watoto walioathirika na hatua hiyo. Wanadai kuwa wanafunzi hao walichaguliwa kihalali kujiunga na shule na wamekuwa wakilipa ada na michango yote lakini wameshindwa kuelewa sababu za watoto wao kutofanya mtihani kwani wao kama wazazi hawahusiki na suala la la kutunza TSM 9 forms.

Shule nyingine ambazo wanafunzi wake wameathirika na uamuzi huo ni pamoja na Patema na Mfundia Sekondari.

Source Mtanzania Desemba 7 2012.

Swali langu kwa Wizara, wanakuwa wapi kukagua uhalali wa wanafunzi hadi wakati wa mitihani ndiyo wanawatimua? Maskini atakomboka vipi wakati kila anapojaribu anaambulia maumivu kutokana na uzembe wa watendaji
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom