Wanafunzi 9,011 wamepata ujauzito kwa mwaka 2021 - 2022

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,067
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, #OmaryKipanga amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), #HawaMchafu aliyetaka kujua ni Wanafunzi wangapi wamerejeshwa Shuleni baada ya Agizo la #RaisSamia.

Kwa mujibu wa Waziri Kapanga idadi hiyo ni ya Wanafunzi 1,554 wa Shule za Msingi na 7,457 wa Shule za Sekondari waliopata Ujauzito huku waliorejea kuendelea na Masomo ya Sekondari ni 1,692.

Aidha, Kipanga amesema kwa upande wa Shule za Msingi, Serikali inaendelea kukusanya taarifa za Wanafunzi waliorejea Shuleni baada ya kukatiza masomo kwa sababu ya Ujauzito..

=================

Jumla ya wanafunzi 9,011 wa shule za msingi na sekondari walipata ujauzito katika kipindi cha kati mwaka 2021 hadi 2022.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga ameyasema hayo leo Jumanne Januari 31, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Hawa Mchafu.

Katika swali lake la msingi, Mchafu amehoji ni wanafunzi wangapi waliokuwa wajawazito na wangapi wamerejeshwa shuleni baada ya agizo la Rais Samia Suluhu Hassan wanaojifungua kupata fursa ya kurejea shule.

Akijibu swali hilo, Kipanga amesema katika kipindi cha mwaka 2021 na 2022 wanafunzi wa shule za msingi waliopata ujauzito ni 1,554 na Sekondari ni 7,457.

Amesema hadi kufikia Januari 2023, wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatiza masomo kwa sababu ya ujauzito na kuendelea na masomo ya elimu ya sekondari ni 1,692.

Aidha, Kipanga amesema kwa upande wa elimu ya msingi, Serikali inaendelea kukusanya taarifa za wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatiza masomo kwa sababu ya ujauzito.

MWANANCHI
 
Aisee, ni wengi sana. Aidha elimu ya uzazi na jinai haitolewi kwa ukamilifu au watoto wetu hawaelewi
 
Too much, hii ni kuviendekeza sasa, wangepewq elimu yao tuu katika makundi yao,
 
Back
Top Bottom