Wanafunzi 8 mbaroni kwa kutaka kulipua ubalozi wa marekani Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi 8 mbaroni kwa kutaka kulipua ubalozi wa marekani Dar es Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, May 20, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  MAOFISA wa usalama wa taifa na polisi wanawahoji wanafunzi wanane wanaosoma shule moja ya sekondari kuhusu jaribio la kuulipua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

  Wanafunzi hao wa shule ya Biafra wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, walikamatwa jana saa tisa alasiri.

  Mtuhumiwa mkuu wa mpango huo wa kuulipua ubalozi wa Marekani, Nassib Zukheri alikamatwa Jumapili saa tatu usiku wakati akifungua koki ya tanki la mafuta katika ubalozi huo.

  Nassib ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Biafra, yupo polisi anahojiwa.

  Inadaiwa kuwa mtoto huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 15 hadi 17 aliingia katika ubalozi huo kwa kupitia geti namba tatu.

  Mkuu wa polisi kandaa maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema, jeshi hilo linatilia shaka ulinzi katika ubalozi wa Marekani nchini na kwamba upelelezi unaendelea kwa kushirikiana na maofisa wa usalama katika ubalozi huo.

  Kwa mujibu wa Kova, ulinzi umeimarishwa katika balozi zote nchini.

  Chanzo: Gazeti la Habari Leo
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tukisema ndugu zetu wana udini mara oh...mara eh.... sasa hii ni nini?? Lakini cha ajabu tena inakuwaje mtu aingie ubalozini tena wa USA unaolindwa kama nini na afanikiwe kufaya ma-uchafu yake?? Au na walinzi wanahusika??
   
 3. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kumbe wanatunyanyasa bure tu tukienda pale. Mimi nilidhani wako makini kumbe hamnazo.
   
 4. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hawana lolote hao zaidi ya kutafuta mbinu itakayo wawezesha kwenda kuishi
  katika magereza ya Malekani wameona maisha ya bongo na ilimu karirishi ni utata mtupu
   
 5. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Security lapse? at the world only superpower's premises?
   
 6. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Njama hizo wanataka wawalete nduguzao kutoka Marikani waje wawe walinzi eti walinzi wahapahapa wameshindwa. Hawa jamaa bwana! kaaaaaaaaaaaaaaazi kweykwey.
  Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ila ni kwa nini haya majina ya wajukuu za mtume yanatesa sana dunia? Ila tusishangae sana maana kwa zile phylosophy zao hata ukiwa mdogo unafunzwa kutetea maslahi yao!!!! Sasa safari ya maendeleo yao itasimama kwa muda usiojulikana!!! Ni faida gani hii? Ila ni lazima kuna master mind wao hapa Tz!!! Kweli sasa ukitoka nyumbani ukirudi salama hujakutana na mlipuko wa bomu la kujitoa mhanga unashukuru Mungu kabisa. Mungu epusha mbali yanayotokea Iraq, Afghanistan, Pakistan, etc! Tutakwisha maana hapa Tz hatujazoea misukosuko hiyo. Wenye nafasi tufanye maombi na kufunga ili shetani asindwe! Nisipigwe madongo kwa kutaja wajukuu wa mtume kwani kwa incidence zote za ughaidi ni wao, at least 99%!!!!
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kwa hisani ya Michuzi blog
   
 9. B

  Bull JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wavivu wa kufikiri utawaona, wataanza ku jump bila kujiuliza maswali, ripoti ilivyo jieleza kwa mtu mwenyefikra ataona na kuelewa tokeo zima ukianza tu msitari wa kwanza wa maelezo.

  Ngoja tuwaone wa upande wa kushoto walivyo kuwa wavivu wa kufikiri!!!!
   
 10. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mtoto wa nyoka si njiwa bali ni nyoka. Si duni akilinganishwa na mamaye/babaye
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  May 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Duu, wanafunzi kazi ipo?
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Unajua hawa watoto wajanja sana kosa limefanyika american soil, hivyo trial huenda ikawa marekani na jela wataserve USA watapewa visa bila bank statement na bila kukaa foleni ubalozini.
   
 13. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hili jamvi halina uvumilivu na kusemwa vibaya Marekani.Lakini ndugu zangu tuwe na ushujaa wa kusema na kukubali ukweli.Marekani kwa hadithi zake nyingi za mabomu yaliyoikosakosa inatia aibu.Mara kiatu,mara sigara.Leo chupa ya mafuta ya taa!.
  Mara Umar Abdul muttalib mara Nassib Zhuher.

  Kama kweli Nassib alitaka kuuripua ubalozi kwanini aende na mafuta ya taa,na kwa nini azitupe chini ya lori la maji!,si afadhali chini ya lori la petroli!.
  Familia iliyosafiri na Umar Abdumuttalib ikitokea Uganda ililibeza sana shambulio lile na kutoa ushahidi wa kutosha kwamba ilikuwa ni mchezo wa kuigiza.Ushadidi wao uliwatikisa wasukaji wa mpango ule uliokuwa na lengo la kupeleka jeshi Yemen. Pamoja na uroho wa madaraka Yemen waligundua na walikataa.
  Kila ushahidi ulipotolewa walibadili maneno kuficha kasoro.Moja ya ushahidi wa familia ile ni kuwa Umar alipopanda kwenye ndege alikabidhiwa kifurushi na mtu aliyevalia suti na bila kukaguliwa dakika za mwisho.Walipoteremka kulikuwa na mtu maalum aliyevalia nguo rangi ya machungwa kumpokea.
  Leo tena tunaambiwa katika bomu hili la mafuta ya taa na gari la maji polisi walifika sekunde chache na wala si dakika chache .Polisi walikuwa wapi wakisubiri kumkamata Nassib?.
  .................................................. .................................................. ....................
  TAARIFA YA UBALOZI WA MAREKANI DAR

  -----------------

  Siku ya Jumapili, tarehe 16 Mei, mnamo saa 2.30 usiku, mvulana mwenye umri wa miaka 15 alikimbia na kumpita mlinzi aliyekuwa mbele ya Ubalozi wa Marekani, akawasha moto kwenye chupa iliyokuwa na mafuta ya taa na kisha kuirusha chini ya moja ya malori mawili ya kubebea maji yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ukuta wa Ubalozi.

  Chupa hiyo ilivunjika lakini haikuweza kulipua moto. Walinzi wa Kampuni ya KK wanaolinda ubalozini hapo walimkamata mara moja kijana huyo kabla hajaweza kurusha chupa ya pili.

  Hakukuwa na mtu yeyote aliyejeruhiwa wala mali yoyote iliyoharibiwa katika tukio hilo. Askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania aliwasili sehemu ya tukio sekunde chache baadaye na kumkamata mtuhumiwa. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.

  Baadhi ya maelezo yanayotolewa kuhusu tukio hili si sahihi, yamekuzwa na kutiwa chumvi mno na yasiyo ya kweli, yakidai kuwa mvulana huyo aliingia ndani ya ubalozi. Hii si kweli. Hakukuwa na mtu yeyote aliyeweza kuingia ndani ya Ubalozi wa Marekani.

  Taratibu zetu za kiusalama za kuzuia wahalifu kuingia ubalozini zilidhihirisha ufanisi wake hapo Mei 16.

  Walinzi wa kampuni ya KK na Polisi wa Tanzania walishughulikia suala hili kwa weledi mkubwa. Tunawashukuru sana.


  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  SHEIKH MASOUD......! tetea watu wako bwana ...haiwezekani mtu arushe "home made explosive" halafu ushindwe kumtetea....! teteaneni wana wa "KUTISHIA DUNIA"
   
Loading...