Wanafunzi 713 washindwa kufanya mtihani kwa utoro...............


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,612
Likes
626,228
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,612 626,228 280
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Tarime; Tarehe: 9th December 2010 @ 21:00

WANAFUNZI 713 waliotakiwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu wilayani Tarime, wamekwama kufanya mtihani huo wa kuingia kidato cha kwanza kutokana na utoro.

Baadhi yao wamekimbilia katika machimbo ya dhahabu ya Nyamongo, Kibaga na Itandura, wengine wamekimbilia biashara ya magendo mipakani na wasichana wameolewa na wengine kupata ujauzito.

Ofisa Elimu wa Wilaya ya Tarime, Emanuel Johnson alisema wanafunzi waliosajiliwa walikuwa 9,463 na waliofanya mtihani mwaka huu walikuwa 8,744 kati yao wavulana 4,372 na wasichana 4,372.

Kati ya waliofaulu, wavulana ni 3,352 na wasichana 2,233 sawa na asilimia 38.3 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo waliofaulu walikuwa asilimia 43.9 na hivyo ufaulu umeshuka kwa asilimia 5.6.

Ofisa huyo alisema kati ya wanafunzi 713 ambao hawakufanya mtihani huo mwaka huu, wavulana ni 413 na wasichana 300 na kati yao wawili walishindwa kumaliza elimu hiyo kutokana na kupata ujauzito.

Kati ya shule za msingi kumi zilizofanya vizuri katika mtihani huo, saba zinatoka wilayani hapa ambazo ni Masafa yenye mchepuo wa Kiingereza iliyopo Sirari, Mudas Pach iliyopo Kibumaye, Keryoba na Mtakatifu Jude zilizopo Buhemba.

Pia ipo Gwitiryo, Nyabirongo, Kebweye, Mtahulo na shule ya msingi Tarime za mchepuo wa Kiingereza kutoka eneo la CMG, shule 10 ambazo hazikufanya vizuri katika mtihani huo ni pamoja na Nyantare, Kenyamanyori, Nyamerambaro, Mangucha, Nyansincha, Karagatonga, Matongo, Gibasuka , Kubiterere , Gibasisi na Kisangura.

Johnson ameonya walimu walevi, watoro na wanaojihusisha na siasa na biashara na kusahau kazi zao kutokana na kuchangia kushuka kwa elimu wilayani hapa.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,612
Likes
626,228
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,612 626,228 280
Baadhi yao wamekimbilia katika machimbo ya dhahabu ya Nyamongo, Kibaga na Itandura, wengine wamekimbilia biashara ya magendo mipakani na wasichana wameolewa na wengine kupata ujauzito.
Nilionavyo tatizo hapa ni umasikini wa wazazi wao.......Kwenda kuchapa kazi ni kujitafutia kipato........na kuolewa hivyo hivyo ni kukimbia hali ngumu ya kimaisha iliyopo majumbani kwa wazazi......................
 

Forum statistics

Threads 1,235,766
Members 474,742
Posts 29,234,444