Wanafunzi 584 watumia madarasa mawili - HabariLeo 23/12/2010

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
MKUU wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Stanley Kolimba, ameshtushwa na taarifa kuwa Shule ya Msingi Mbuyuni katika Kata ya Kigwa, ina wanafunzi 584, walimu sita, vyumba vya madarasa viwili na vyoo sita.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya kata hiyo yenye kijiji kipya, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuyuni, Emmanuel Mwanamiwa, alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa kwani tangu ilipoanzishwa mwaka 2004 na kusajiliwa 2008.

Alisema kutoka wakati huo shule hiyo ina vyumba viwili vya madarasa, wanafunzi 584, walimu walikuwa watatu, na Oktoba mwaka huu, wameongezeka wanne na madawati ni 19 tu.

Mwalimu Mwanamiwa alisema hali ya wanafunzi jinsi wanavyosoma ni mbaya hasa ukizingatia kuwa wakati mwingine wanapeana zamu ya kusoma ndani ya darasa moja, darasa la kwanza na la pili.

Alisema njia nyingine ambayo huwa anaitumia katika kufundisha, ni wanafunzi wengine wanawekwa nje chini ya miti na kwamba vimetengenezwa vibao mithili ya mbao za semina na wanafunzi kukalia.

Alisema kipindi cha masika inaponyesha mvua, wanafunzi wanaosomea chini ya miti hulazimika kurejea katika madarasa yaliyojengwa kwa msaada wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), na kujificha, na ikitokea wanafunzi waliokuwa madarasani, masomo yanakufa kwani chumba hujaa wanafunzi takriban 200.

Katika hotuba yake, DC Kolimba alisema ni hali ya ajabu na imemsikitisha hasa katika kipindi hiki ambacho serikali imelivalia njuga suala la elimu, hivyo aliagiza mwenyekiti wa kijiji hicho kuitisha mkutano na wananchi wake na kupanga mikakati ya namna gani watakavyojenga vyumba vya madarasa na nyumba za walimu.

Mkuu huyo wa Wilaya alichangia Sh 500,000 na kuwasihi wananchi nao kila mmoja kuchangia ili kuisaidia shule hiyo.
 
Hali inasikitisha kweli, lakini Mkuu wa Wilaya kusema kuwa serikali imelivalia njuga suala la elimu ni kichekesho. Kuna magari zaidi ya 300,000 ya bei za kutisha ambazo wamepewa wakubwa watanue wakati serikali inaruhusu hali kama hii? Wakati serikali makini duniani wanawekeza katika elimu, sisi tunawekeza katika ujinga, tunawekeza katika kuvimbisha matumbo na mifuko ya wachache. Kwa mtaji huu watanzania tumekwisha.
 
Back
Top Bottom